mageuzi1992
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 2,503
- 252
Kunasiku tutaandamana watakimbia offisi zao
basi nadhan warushe mpaka radio one...ili wakikata umeme tutumie hata redio kwenye simu zetu.Endapo umeme utakatwa kwa sababu yeyote ile kweli itakuwa ni mchezo mchafu unachezwa. Lets wait and see
Mungu ibariki Tanzania
Mkuu Mkjj, miye nakuomba usisubiri hao mafisadi walipwe, kama unaweza kuyaweka mahojiano hayo hadharani kabla ya malipo hayo kufanywa basi unaweza kabisa kwa namna moja au nyingine kuinusuru nchi yetu kulipa malipo ya kifisadi ya mabilioni ya shilingi.
Hapana; kwa miaka mitano tumewalilia kuhusu watu hawa hawa na sasa wamekuja na kututhubutisha; sasa watawala wetu wawalipe ili tuwaoneshe jinsi gani utawala wao ulivyo mbovu na Watanzani waliowachagua wajue wametuchagulia madudu gani. Walipeni tu. Nitawekeza dokezo la interview hiyo Jumanne.
Kwenye viambatisho vya hukumu ya ICC, kama ilivyosajiliwa Mahakama Kuu ya Tanzania, zipo nyaraka
zinazoonyesha kwamba mwanasheria aliyeishauri TANESCO kuvunja mkataba na Dowans – kwa kusema
kwamba sio mkataba halali na kwamba hakuna madhara ya kisheria kuuvunja – ndiye huyo huyo pia aliyeishauri
Benki ya STANBIC kutoa mkopo wa dola za Kimarekani milioni 20 kwa Dowans – kwa kusema
kwamba ni kampuni halali, inakopesheka na ina mkataba halali na TANESCO. Na ndiye huyo huyo aliyeiwakilisha
TANESCO kwenye kesi iliyofunguliwa na Dowans, kesi ambayo imetokana na ushauri wake, na,
baada ya hukumu, ndiye huyo huyo, kwa mujibu wa maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati ya terehe 6 Januari
2011, aliyetoa ushauri kwamba hakuna njia nyingine zaidi ya kuilipa Dowans.
Nimeipata hii hivi punde...Kuna anayeweza kuthibitisha haya!?
umepotoka? uombe radhi wna Jf?