Mjadala: Nini kingetokea Serikali isingeingilia biashara ya zao la korosho?

Upuuzi huu ungeusema mbele za umma wakati uko Lindi au Mtwara leo jioni hii ungelala Mochwari.
Halafu acha uongo, eti walanguzi walijipanga kulipa 1500-1700 Shs. Unaongea vitu usivyovijua kabisa. Hivi mnatatizo gani nyie vijana wa CCM?
Ni ukosefu wa ajira , mitaji au akili?
 
Kwa hiyo ni bora waneachwa walipwe shilingi 1,500 kwa kilo?
Hakuna mnada uliowahi kutaka kununua korosho kwa tshs. 1,500. Bei oliwahi kufikiwa kwenye minada ni kuanzia tshs. 2,500 hadi 2,700.

Naona umeleta mjadala wa kitu ambacho hukielewi. Tshs. 1,500 ilikuwa bei elekezi na sio bei ya solo.

Hivyo kama siasa isingeingia wakulima wangeuza kuanzia tshs. 2,500 na kuendela huku wakilipwa cash.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatokuelewa hata kidogo sawa na unampigia mbuzi mziki acheze kitu ambacho hakiwezekani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ilifanya vizuri kuingilia mchakato. Hata hivyo, ilivuka mipaka tofauti na uwezo wake. Ilitakiwa kuishia pale ambapo wanunuzi walipatikana kwa bei ya 3000+, hapo ndipo wangenufaisha wakulima na wananchi wa kusini. Hatua walioendelea nayo haikuwa sahihi na imeleta na italeta athari kubwa. Asante
Mdogo wangu alitarajia apate pesa aanzishe biashara kilichotokea sasa pesa hajapata ameishia kukopa mpk muda huu!pesa ya korosho ikitoka ana elf 30 mkononi!!

Inatia huruma na inasikitisha sanaa
 
Hakuna mnada uliowahi kutaka kununua korosho kwa tshs. 1,500. Bei oliwahi kufikiwa kwenye minada ni kuanzia tshs. 2,500 hadi 2,700.

Naona umeleta mjadala wa kitu ambacho hukielewi. Tshs. 1,500 ilikuwa bei elekezi na sio bei ya solo.

Hivyo kama siasa isingeingia wakulima wangeuza kuanzia tshs. 2,500 na kuendela huku wakilipwa cash.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujui kitu
 
Mjadala: Nini kingetokea Serikali isingeingilia biashara ya zao la korosho?

Kumekuwa na mjadala mkubwa tangu serikali ilipotangaza kuzuia wanunuzi wa zao la korosho ambao walijipanga kulipa wakulima wastani wa shilingi 1,500-1,700/- kwa kilo badala ya bei ya angalau shilingi 3,300 ambayo serikali inaamini wakulima wanapaswa kulipwa.

Ikumbukwe, kabla ya serikali kuingilia kati waliibuka wanasiasa wakiongozwa na Zitto Kabwe wakipaza sauti wakiitaka serikali inunue korosho kutoka kwa wakulima ili kuwakinga na hasara kutokana na wafanyabiashara waliotaka kuwanyonya wakulima. Japo kwa sasa ameibuka na kuyapinga maneno yake ya mwanzo.

Hoja kubwa ya kujadili ni nini kingetokea kama serikali isingeingilia biashara ya korosho? hali za wakulima ingekuwaje? wanasiasa leo wangesema nini dhidi ya serikali?

Ni kweli kuwa zoezi la serikali kununua korosho limekuwa taratibu kuliko ilivyokadiriwa. Lakini, ukweli unabaki wakulima na wadau halali wa korosho wananufaika zaidi na hatua ya serikali kuliko wangeachwa wanyonywe na walanguzi.

Zaidi ya wakulima kunufaika, unamuzi wa serikali umeweka nidhamu kwa walanguzi na wanunuzi wa korosho kutotumia mwanya wa kuungana na kupotosha soko kwa kutoa bei zisizo halisi.

Pamoja na wengi kupiga ramli kuwa ''katika msimu ujao wanunuzi wa korosho hawatakuja'' ulozi huu hautatimia kwani hata sasa baadhi ya wanunuzi halisi wanaoomba serikali na wako tayari kulipa bei iliyopendekezwa ambayo itamnufaisha mkulima, kinyume na ramli za akina Zitto kuwa serikali inapoteza dola milioni 600.

Hitimisho, Wakulima wangekuwa na hali mbaya zaidi kama serikali isingeingilia kati biashara ya korosho.

Rejea;
View attachment 992451
Wafanyabiashara waiomba Serikali inunue korosho za wakulima - JamiiForums
Kwani nini kinatokea kwa Serikali kutonunua Mazao mengine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom