Mjadala: Nini kingetokea Serikali isingeingilia biashara ya zao la korosho?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Mjadala: Nini kingetokea Serikali isingeingilia biashara ya zao la korosho?

Kumekuwa na mjadala mkubwa tangu serikali ilipotangaza kuzuia wanunuzi wa zao la korosho ambao walijipanga kulipa wakulima wastani wa shilingi 1,500-1,700/- kwa kilo badala ya bei ya angalau shilingi 3,300 ambayo serikali inaamini wakulima wanapaswa kulipwa.

Ikumbukwe, kabla ya serikali kuingilia kati waliibuka wanasiasa wakiongozwa na Zitto Kabwe wakipaza sauti wakiitaka serikali inunue korosho kutoka kwa wakulima ili kuwakinga na hasara kutokana na wafanyabiashara waliotaka kuwanyonya wakulima. Japo kwa sasa ameibuka na kuyapinga maneno yake ya mwanzo.

Hoja kubwa ya kujadili ni nini kingetokea kama serikali isingeingilia biashara ya korosho? hali za wakulima ingekuwaje? wanasiasa leo wangesema nini dhidi ya serikali?

Ni kweli kuwa zoezi la serikali kununua korosho limekuwa taratibu kuliko ilivyokadiriwa. Lakini, ukweli unabaki wakulima na wadau halali wa korosho wananufaika zaidi na hatua ya serikali kuliko wangeachwa wanyonywe na walanguzi.

Zaidi ya wakulima kunufaika, unamuzi wa serikali umeweka nidhamu kwa walanguzi na wanunuzi wa korosho kutotumia mwanya wa kuungana na kupotosha soko kwa kutoa bei zisizo halisi.

Pamoja na wengi kupiga ramli kuwa ''katika msimu ujao wanunuzi wa korosho hawatakuja'' ulozi huu hautatimia kwani hata sasa baadhi ya wanunuzi halisi wanaoomba serikali na wako tayari kulipa bei iliyopendekezwa ambayo itamnufaisha mkulima, kinyume na ramli za akina Zitto kuwa serikali inapoteza dola milioni 600.

Hitimisho, Wakulima wangekuwa na hali mbaya zaidi kama serikali isingeingilia kati biashara ya korosho.

Rejea;
1547292367487.png

Wafanyabiashara waiomba Serikali inunue korosho za wakulima - JamiiForums
 
Hizi porojo za kuwaridhisha watawala wenu, zipigeni mkiwa mikoa ya kusini.
Msipige ramli kwenye maisha ya watu.

Wanafunzi hawajenda shule hadi sasa, walioenda ni wacheche kuliko wengi walioko nyumban....

Acheni siasa na maisha halisi ya watu
 
Labda utukumbushe mwaka juzi ambapo serikali haikuingilia nini kilitokea mh Naibu wa Sindimba?!
Kijana, nitakita kukujibu swali lako na si ramli; Miaka mitatu iliyopita wafanyabiashara walitoa pendekezo la bei zilizoakisi ukweli kwenye soko la dunia.
 
Hizi porojo za kuwaridhisha watawala wenu, zipigeni mkiwa mikoa ya kusini.
Msipige ramli kwenye maisha ya watu.

Wanafunzi hawajenda shule hadi sasa, walioenda ni wacheche kuliko wengi walioko nyumban....

Acheni siasa na maisha halisi ya watu
Endeleeni kupoteza muda, kwa sasa jielekeze kwenye hoja.
 
Ni afadhali wale wahindi waliokuwa wananunua 2,500 hadi 2,700 kwa kilo ambapo wakulima walikuwa wanalipwa kwa wakati. Lakini toka Jiwe aingilie kati kukusanya korosho, wakulima wanaishi maisha ya shida sana.

Walio wengi wameshindwa kuwapeleka watoto shule hadi kufikia leo. Ni wakulima wanaokadiriwa kufikia 80% hawajalipwa pesa zao hadi leo.

Serikali ya Jiwe inalaaniwa sana katika mikoa ya kusini. Serikali imebaki kuwaongopea watanzania kwamba wakulima wote wamelipwa huku waliolipwa hawafiki hata robo ya wakulima wote.

Ni heri wangeacha wahindi waendelee kununua.
 
Ni afadhali wale wahindi waliokuwa wananunua 2500 hadi 2700 kwa kilo ambapo wakulima walikuwa wanalipwa kwa wakati. Lakini toka Jiwe aingilie kati kukusanya korosho, wakulima wanaishi maisha ya shida sana. Walio wengi wameshindwa kuwapeleka watoto shule hadi kufikia leo. Ni wakulima wanaokadiriwa kufikia 80% hawajalipwa pesa zao hadi leo. Serikali ya Jiwe inalaaniwa sana katika mikoa ya kusini. Serikali imebaki kuwaongopea watanzania kwamba wakulima wote wamelipwa huku waliolipwa hawafiki hata robo ya wakulima wote. Serikali hii ni ya kitapeli ni heri wangeacha wahindi waendelee kununua.
Kwa hiyo ni bora waneachwa walipwe shilingi 1,500 kwa kilo?
 
Serikali ilifanya vizuri kuingilia mchakato. Hata hivyo, ilivuka mipaka tofauti na uwezo wake. Ilitakiwa kuishia pale ambapo wanunuzi walipatikana kwa bei ya 3000+, hapo ndipo wangenufaisha wakulima na wananchi wa kusini. Hatua walioendelea nayo haikuwa sahihi na imeleta na italeta athari kubwa. Asante
 
Hoja nzuri, kuna mengi mazuri yanaendelea, kumbuka waliokuwa wanufaika wa mfumo wa unyonyaji dhidi ya wakulima wapo nao wanapotosha mengi.
 
Shule za sekondari Nanyamba, Nitekela, Mnyawi, Mnima na Mtiniko katika Halmashauri ya Mji Nanyamba pamoja na shule za sekondari za Namikupa, Naputa, Nandonde, Luagala, Ngunja, Salama na Dinduma zimepokea wanafunzi wa kidato cha kwanza wasiofikia robo tangu shule ifunguliwe hadi kufikia jana Ijumaa. Tatizo kubwa ni ukosefu wa pesa za kuwaandaa wanafunzi kwa vifaa vya shule. Mwambieni Jiwe atembelee kusini ajionee hali ilivyo si kukalia propaganda za kijinga humu mtandaoni.
 
Si kweli.
 
Kwa hiyo ni bora waneachwa walipwe shilingi 1,500 kwa kilo?
Heri ya moja nenda, kuliko kumi nenda rudi. Maaamuzi ya pamoja ni jambo muhimu sana, WAKUDADAVUA. Zito aliposhauri,hakushauri kulikurupukia suala hili. Serikali ilitakiwa ilipeleke bungeni ili lijadiliwe na ukumbuke wakati ule bunge lilikuwa na vikao,ili kuona pesa zinapatikanaje na wapi? Hali isingekuwa hii iliyopo sasa. Kubalini kushuka kimawazo huko mlikojiweka,ili tusaidiane kujenga nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo maoni yako ni kuwa Zitto yupo sahihi? unaweza kuonyesha jinsi gani ya kulishighulikia suala hili au ni twitter sms za kupotosha na kujikana?kusema ni rahisi kuliko kutenda.
 
Back
Top Bottom