Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,392
- 7,863
Kichaa anaweza kutembea ovyo tu na kuokota chochote anachokiona hata jalalani na kula lakini huwezi kusikia akilalamika tumbo linauma sasa jaribu wewe ambaye upo normal uone kama hujahamia toi...What is the reason behind?
----------------
----------------
Tatizo la ulimwengu wa leo watu wanasafisha mno kila kitu, kwa kuchemsha au kupika kila kitu au kwa kusafisha kwa madawa ya kuua vijidudu.
Ukweli ni kwamba jambo hilli linadhoofisha uwezo wa mwili wa kujikinga na mashambulizi ya vimelea
Vichaa wengi hawanyi maji ya kuchemsha na wala hawaogi mara kwa mara wala hawatumii neti za kujikinga na mbu hivyo miili yao hujenga kinga imara sana dhidi ya magojwa.
Pia vichaa wengi wanatembea mchana kutwa na hivyo hupata zoezi kubwa la mwili ambalo huimarisha miili yao na kuwapatia afya tele tofauti na watu wengi wenye akili zao ambao hufikiri wanajipendelea kwa kutembelea magari au pikix2 siku nzima. Hawa ndio utawasikia wakiugua kila siku
Vichaa wengi hawana hela za kunywa pombe na kula vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi. Wenye akili zao wanajiona wamefanya vyema sana kujaza sahani zao kwa kuku, kiti moto na keki
Vichaa wengi hawana majukumu kama waungwana walivyo na hivyo hawana mawazo mengi kama madirecta na mameneja wanaokufa kwa msongo wa mawazo
Vichaa hawana akili na utashi na kwa hiyo ni kama watoto wadogo mbele ya Mungu hivyo hawana hatia, hata katika mahakama za kidunia kichaa hawezi kuhukumiwa kwa kosa lake. hivyo hawana dhambi na ni moja kati ya mambo yanayowafanya wasiugue hovyo
Kichaa akilala hata kama ni chini usingizi wake ni mkubwa na humwongezea kinga ya mwili na afya
Vichaa hawana mali kama ilivyo wengi wa matimamu na hivyo hawana stress zozote zitokanazo na kupanda au kushuka kwa kipato
Vichaa wengi hawana mahusiano ya kingono na hivyo wengi hawapati ukimwi na magonjwa ya zinaa kama wajanja wenye wapenzi kila kona
Vichaa hawana marafiki na hivyo hawapati mifadhaiko inayotokana na kusalitiwa na marafiki
Vichaa hawaishi maisha ya kufikirika (ideal life) huishi maisha halisi na hivyo kila kitu chao huwa halisi ikiwa ni pamoja na afya zao
Vichaa hawafikiri kuhusu kesho na hivyo huishi kikamilifu maisha ya wakati huu na kuyafurahia