Kwahio mkuu tuchukulie mumeo alikuwa na fedha Ila baadae akafilisika au kufariki alafu wewe ndo hivyo majukumu yake huyawezi, yaani ulikuwa golikipa na Sasa umeachiwa watoto... Unafanyaje kuendesha gurudumu au ndo utaanza kudanga? Maana majukumu yote yatakuangalia wewe tu mwanamke?
Haya maisha ni hayatabiriki. Kuna jamaa mmoja alikuwa anafanya kazi na mkewe ni mama wa nyumbani. Juzi juzi kafukuzwa kazi . Mbaya zaidi akapelekwa polisi. Hela alizokuwa nazo inabidi azitumie ili aweze kuachiwa. Sasa hivi hana hata mia, yaani ni shida tupu nyumbani. Hata kama mume ana hela jitahidi sana na wewe kujua namna ya kuzitafuta pamoja na mumeo. Huwezi jua kitatokea nini kwenye haya maisha.
 
Mie hayanikuti sababu siwezi ruhusu upuuzi wa kutembea na mwanamke maskini wa roho na akili!Hawa wanakuwaga pretenders sana.

A woman with a rich heart loves for real!
Mkuuu nakuamini katika kutoa elimu kwaumma,hebu nielimishe Kua masikini wa Akili naroho Nimwanamke wa Aina gani,japokua naunga mkono hoja ya Kua to most women ndoa ni Ajira aisee,huu kiukweli usiopingika naunakuta kabisa mwamba before marriage alikua fresh Tu lkn, after marriage anakumbana nahatima mbaya Yamaisha yake Kwa mgongo wawatoto
 
Kwahio mkuu tuchukulie mumeo alikuwa na fedha Ila baadae akafilisika au kufariki alafu wewe ndo hivyo majukumu yake huyawezi, yaani ulikuwa golikipa na Sasa umeachiwa watoto... Unafanyaje kuendesha gurudumu au ndo utaanza kudanga? Maana majukumu yote yatakuangalia wewe tu mwanamke?
Nahitaji MTU ajibu Hili swali ambalo ndio msingi wakua mwanamke hapaswi kukaa Tu kama golikipa Bali aaangali shuguri yoyote yakumuingiza kipato nakujua halo yauchumi inaendaje
 
Oa halafu ishi maisha yako hataki aende ....hafuti unavyo taka aende....anakuletea jeuri wakati una mlisha aende ...usisingizie watoto wataishije na bla bla zingine ....Kuna watoto wanazaliwa tu na mama zao wanapoteza uhai ..mkwani hao wanaishije ....?

Hakuna tuzo utakayo pewa ya kusumbuana akili na mwanamke mpuuzi ......piga chini
Typical alpha male,nazidi kufyonza elimu adimu ambayo hata viongozi wangu wadini wasingenipatia
 
Mkuuu nakuamini katika kutoa elimu kwaumma,hebu nielimishe Kua masikini wa Akili naroho Nimwanamke wa Aina gani,japokua naunga mkono hoja ya Kua to most women ndoa ni Ajira aisee,huu kiukweli usiopingika naunakuta kabisa mwamba before marriage alikua fresh Tu lkn, after marriage anakumbana nahatima mbaya Yamaisha yake Kwa mgongo wawatoto
Mwanamke maskini wa akili huwa anaamini kuwa mwanaume yupo kwa ajili ya kumfurahisha yeye tu.
She think a man owes her the world, hataki kuwa responsible in anyhow.

Maskini wa roho maana yake ni kukosa utu to the deadend. Mwanamke maskini wa roho anafikiria pesa ndio thamani zaidi ya utu. Atatanguliza maslahi in every aspect bila kujali utu. This is the worst kind of partner ever sababu tamaa yake itamfanya ashindwe kusettle siku zote na ubaya wa hawa wahivi huwa pia hawapendi wengine wapate.
 
Nafikiri sio mbaya ilimradi mmekubaliana tuu. Kwasababu mwanaume ana wajibu wa kumtunza Mwanamke kwahiyo Sio Ajira ndio mfumo ulivyo.. sasa akuzalie tuu watoto iwe halafu yeye ajitegemee impossible . Maana ya kuwa mime your responsible

Hii lugha ya “akuzalie Mtoto au watoto inatokana na nini?

Siielewagi!

Kwani inatumika surrogate procedure?

Je mwanamke anaweza kubeba mimba peke yake bila mbegu za Mwanaume?!
 
Kwanza ashukuriwe bwana Mungu wetu kwa kutupa kibali Cha kuiona Leo hii tena.

Kwa harakaharaka tena bila kupepesa macho nitaushika usukani wa uzi huu nikiwapeleka moja kwa moja katika mada hii ya ufumbuzi au hoja juu ya maisha yetu ya mahusiano baina yetu Sisi wanaume na wenzetu wanawake.

Mimi ukiniuliza Mapenzi ni nini kwa kifupi nitajibu mapenzi ni upendo, Na ukiniuliza upendo ni nini nitakuambia ni hisia njema au matendo mema tuyafanyayo kwetu sisi na mazingira yaliyotuzunguka, Upendo wa kweli unaanzia kwenye hisia ndipo kwenda katika akili inayotuongoza kuufanya Upendo.

Ukiniuliza kuoa/kuolewa ni nini nitakujibu ni maridhiano baina ya watu wawili me na ke kuamua kuishi pamoja Kama mume na mke, Na pia ukiniuliza ndoa ni nini nitakujibu ni kiapo baina ya watu hao wawili walioamua kuishi pamoja Kama mume na mke, Kiapo hicho hufanyika kwa taratibu maalumu na kuhusisha mashahidi.

Sasa leo nataka kuwachambua Hawa wanawake wa kisasa ambao wamegeuza Mapenzi/Kuolewa/Ndoa Kama chanzo cha kujiingizia kipato au kufanya maisha yao yaende, ni hivi kwa Sasa kusema ukweli kasi ya watu kuoana imepungua kwa kasi sana. Nasema hayo kwa utafiti wa harakaharaka nilioufanya kwa mfano: Kundi kubwa linalohudhuria kwenye maombi kwa yule Mchungaji wa Kawe, Asilimia kubwa ya wanawake wanaokwenda pale wanachokwenda kukifuata ni Muujiza wapate Kuolewa, Sasa mimi nilifikiri maybe wanataka kuolewa kwa lengo la Upendo na Kuijaza dunia pekee kumbe wanataka kuolewa kwa kuwa maisha ni Magumu (So sad kwa kweli)

Yaani ndio maana unakuta mwanamke anafanyiwa ukatili kwenye ndoa na mumewe, Anapigwa anacheatiwa lakini anavumilia kwa kuwa mwanaume ana hela, Mwanamke anaona bora avumilie mateso ila asiachwe na mtu mwenye hela, Ukifuatilia background ya mwanamke alishakutanaga na mwanaume mwenye Upendo wa kweli kwake Ila akamdump kwa kuwa mwanaume hakuwa na hela

Ubaya ni kuwa wanaume wameshagundua hilo that's why wanaume wa sasa washaona kuwa wanawake wote wapo kimaslahi tu, Ni ngumu kumkuta mwanaume anaefahamu tabia za wanawake wa kisasa akioa, Ukiona mwanaume anaoa ujue kakubali kujishusha, karogwa au umri umekwenda, Ila kwa dalili zinapoelekea naona ukosefu wa ndoa kabisa, Na haya yote yanasababishwa na wanawake wenyewe imagine wao ndo wapo wengi kuliko wanaume alafu badala akipata kampenzi kake atulie na akubaliane na hali ya maisha ya mpenzi wake yeye atataka kwenda na ukisasa ambao utamshinda mpenzi wake kumhudumia hali itakayomfanya mwanamke aamue kwenda kutafuta mwenye kuweza kumtimizia mahitaji yake, Yaani kiufupi wanawake wa sasa hawataki mwanaume mwenye Upendo bila pesa, Wao wapo radhi apate hata wa kumlala tu na kumpa pesa akakidhi mahitaji yake Mahitaji yao Sasa Kusuka, Kuosha kucha, Nguo nzuri, Vyakula vya Take Away KFC, Outing Vacation yaani wadada wa sasa hivi nisikufiche unavyomuona Gigy Money, WemaSepetu na Uwoya na wengine wengi wasanii ndivyo wadada Hawa wanataka kuishi kama wale kitu ambacho Ukifuatilia hao watu wanaishije utagudua kuwa Kweli Decor Bysco anasema ukweli, Technology imekuja kuua Upendo wa kweli kwa Sasa Upendo wa kweli ni kwenye vitu tu, Uliobaki wote ni fake. Tuanaamini upendo Kupitia Machapisho, likes na comments Ila in reality all are fakes.

Ewe kijana unaetaka kuoa kwa muda huu jiandae kisaikolojia Mimi kijana mwenzenu naongea Kupitia experience maana nimeshuhudia wanandoa wengi wanaume wakituchekea uwongo tulio single, Utamsikia " Ndoa tamu kijana jitahidi uoe" Ukimcheki ndevu zake kazisusa nywele zipo rafu kiufupi kajisahau mzee wa watu, Anajiproud mbele yenu Ila ukimchungulia kwa dirishani akiwa amekaa barazani kwake muda mwingi kashika tama alaf kaduwaa Ila mwanamke kanawiri kazi kubadili vijora na kuudhuria shughuli za mitaani, Ile mistari ya kibibilia iliyosema "Ishini nao kwa akili" hao walikuwa wanawake wa zamani, Wanawake wa zamani ilikuwa ukitumia tu akili unamuwin Ila wa sasa Cha kwanza unatakiwa Uwe na hela, ha pili zisiishe, Cha tatu ndo utumie Akili Cha nne ujitahidi sana kumuomba Mungu wako akuepushe na roho za mauti.

Majuzi ni kama niliona chapisho wale watu wa haki za wanawake wakidai ipitishwe sheria ya wanaume kuwalipa wanawake zao mshahara nikacheka sana maana waliotoa Hilo wazo ni wanawake hawahawa, Nilicheka kwa kuwa niliona kuwa sasa wamechoka kujificha kuonesha kuwa Malengo ya wao kukubaligi kuolewa ni kujiingizia kipato Sasa wanakuja kidada wa kazi Au nisemeje wanajamvi? Sasa mtu ukimlipa Hadi mshahara hivi huyo atakuwa hata na mamlaka ya kukuuliza Jana ulilala wapi, Yaani unaanzaje kuniuliza Mimi boss wako nililala wapi?

Anyway sijakatisha mtu tamaa Ila nimeona tusimalize huu mwaka bila kuwakumbusha tu kuwa Kuoa na Kuolewa kumedondosha wanaume wengi chini, Sisi tuliobaki embu tujitunze na tuanze kuringa maana Hawa viumbe wapo wengi sana kwa sasa, We na kiherehere chako unajifanya unaoa are you sure umeridhika na huyo? Are sure Ni akili zako na hujarogwa? Are you sure hatutokupoteza? Hawa tunatakiwa tuwasuse Hadi wajifunze ili anapopata mume wamuheshimu, Maana wao wanahisi kwa kuwa kila anapopita anapigiwa mluzi ndo anapendwa kumbe wengine wapitaji tu.

Utamsikia "Oooh unasema hivyo kisa huna hela" narudi palepale wewe Kenge unamaanisha kabla ya hela hakukuwa na Mapenzi? Au kisa wewe nimekugusa niliposema hujui kutofautisha Upendo wa mtu na vitu? Hapa nimezungumzia ule Upendo wa kweli ndo maana mnapoapa kiapo cha ndoa wanasema "Shida na Raha" na sio "Umasikini na Utajiri".

Decor Bysco
 
Mwanamke maskini wa akili huwa anaamini kuwa mwanaume yupo kwa ajili ya kumfurahisha yeye tu.
She think a man owes her the world, hataki kuwa responsible in anyhow.

Maskini wa roho maana yake ni kukosa utu to the deadend. Mwanamke maskini wa roho anafikiria pesa ndio thamani zaidi ya utu. Atatanguliza maslahi in every aspect bila kujali utu. This is the worst kind of partner ever sababu tamaa yake itamfanya ashindwe kusettle siku zote na ubaya wa hawa wahivi huwa pia hawapendi wengine wapate.
Nashukuru Sana mkuu,Kwa ushauri uliojaa misuli,zaidi usoache kutupia shule whenever you get time!
 
Kijana husika na kichwa hapo juu.

Kumekuwa na wimbi kubwa Sana la vijana wa kileo nikiwemo Mimi kwamba katutaki kuoa kutokana na masekeseke mengi waliyonayo hawa mademu.

Ila ukweli mchungu ni kwamba tutaoa Tu.. tutake tusitake tujiandae tu Kwa hilo hakuna namna sasa.

Narudia tena... TUTAKE TUSITAKE TUTAOA TUUU.

NI WAY OUT.
 
Nilipoona unaongeza bia tu nikajua zikikolea utaanza mada zako za ajabu ajabu
 
Acha kutia kichwani maandishi ya humu ndani, kumbuka hii ni JamiiForums watu wanaropaka ropoka tu nyuma ya keyboard. Ukifuatilia zaidi wao wameoa ama wako kwenye michakato ya kuoa. Kikubwa za kuambiwa changanya na zako, simple tu.

Back
Top Bottom