Jamaa mmoja hivi. Tulikuwa marafiki wa karibu sana wakati tupo Secondary school.
Tukahitimu secondary. Baada ya maisha ya skonga kufika tamati, na urafiki wetu ukaanza kupungua.
Tukapotezana. Baada ya miaka mitatu, nikasikiaga kuwa mwana yupo chuo 'mlimani' anakata kitabu. Nikapata contacts zake. Mimi nipo kitaa naunga unga, life la manati. Nikawa namtafuta mwana ili kumjulia hali, kila napopiga simu... ananiuliza: "wewe nani?" namjibu, then tunapiga story mbili tatu. Kila nikimpigia, the same shitt: "wewe nani"? namba yangu ni ile ile. Nikimtext kumpa Hi, hajibu SMS. Nikaona uduwanzi, nikadelete namba yake, na nikamu-erase out of my memory. Nikam-unlist from my folks list.
After miaka kadhaa, majuzi kati hapa (3 months back) nikakuta misscall. Kabla sijaitwangia iyo namba, gafla nikapata SMS kutoka kwake...
Yeye: "Hi kiongozi. Ebana habari za masiku tele. daaah long time kitambo"
Mimi: Fureshii barida. eeh wewe nani? naona namba mpya
Yeye: "Mimi fulani (akataja jina), mshikaji wako. Vipi pande zipi siku hizi? nimekucall ila naona hukupokea simu"
Mimi: Eeh nambie, unasemaje? sorry, sikusikia simu... nilikuwa bize kujiburudisha na headlines za media house bongo juu ya faru john, chato international airport, mauzaUza ya Ben Saa9, n.k. Akadabla'kadablah nyingi nchi hii.
Yeye: "ebana Mkuu, mwezi December mie naoa. Mie nachukua jiko kaka. Nipo katika maandalizi ya harusi.
Mimi: So what? nifanyeje. Au unataka niwapeleke Chato wewe na mkeo mkale honeymoon? maana usafiri upo, siku izi namiliki Dreamliner.
Yeye: "Hahahaa. Mchango wako kaka. Nahitaji support yako, as my best friend. Si unajua haya mambo bila support hayaendi kaka."
Mimi: Acha ufala. Ingekuwa msiba au majanga ningechangia, but not shangwe kama hiyo. BTW, am I still your best friend? Acha ufala.
Yeye: ... kimyaaa mpaka leo hakujibu.
My take: Watu wakiwa na shida ya kuchangiwa harusi ndipo hukumbuka mpaka friends zao oldi skuli. Uduwanzi kishenzzi.
-Kaveli-