Mjadala juu ya taaluma ya ualimu

SaintErick

Member
Aug 7, 2013
56
12
Najua humu kuna walimu wa ngazi mbalimbali na wenye elimu na uzoefu kutoka seheme mbalimbali. mimi ngependa kujua kwanini taaluma ya ualimu ni tofaut saana na taaluma zingne kama sheria na udaktri?? Je, ni kweli taaluma ya ualimu inadharaulika?? ni ya watu waliokosa seem ya kukimbilia ndo imekua kwa sehem ya kujificha??
kwa siku nying saana walimu tumeonekana kama n watu flan au wafanyakaz wa kujitolea tuu na maslahi ya mwalim yamekua kama ya kuhurumiana na sio haki yake. chanzo cha tatizo ni nini? ni kasumba,dharau za waz au ni nini? tunaona wote walikua "wajinga" kwa mda flan, mwalim akawaelimisha wakaelewa wakawa welevu lakin baadae wamekuja kumkanyaga mwalim!!!! Inaumiza saana watendeayo walim..lakin je ni kweli mwalim anastahili anachokipata?? Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kiko kwaajili ya nan?? kila siku mshahara tuu,, mbona mwalim haendelezwi ile taaluma yake?? kwa hio kaz nn?? Tunaweza kufanya mwalim akaheshimika kama mwanasheria,daktari,mhandisi,mhasibu n.k lakin tuu kwa kujikomboa kifikra na kubadili kwa baadhi ya mifumo ya kizaman juu ya walim. EDUCATION FIRST, TEACHERS FIRST FOR LITERACY WORLD. PRAISE TEACHERS DONT UNDERMINE THEM.
 
Unaijua sheria yankwanza kabisa ya ualimu?? "UALIMU NI WITO" arguments zako zoote ziwe arround hii basic principle of ualimu ndo tuanze mjadala sasa..
 
Tataizo umejiuliza maswali na kujijibu mwenyewe hapo mwishoni ulipoandika kwa herufi kubwa.
Mkuu tafiti na mapendekezo mengi yalishatolewa kuhusu hicho unachotaka tujadili. Tatizo HAKUNA UTASHI WA KISIASA kubadili hali dhoofu ya taaluma na wanataaluma wa kada hiyo.
tutapiga kelele sana, tutajaza server kwa mapovu hapa lakini utashi wa kisiasa haupo.
 
ni kweli lakin nakumbuka wakat Aristotle akianzisha shule ya kwanza pale athens mwaka 387BC kipindi hiko wao ualimu haikua kama wa sasa hivi kwa kua kulikua hakuna shule ya ualiamu!!! ila sasa hivi sisi ualimu ni taaluma, na kwa kua taaluma ni jamii ya wasomi bas walipaswa kujiwekea mising kma jamii nyingne za kisomi. hivo bas ualimu ndio n wito,lakin kama ni wito maisha yakoje?? tunajua kwa kua kwa maana ya taaluma ilianza kama n wito lakin baadae tukaacha kua wito pekee kutokana na mahitaji kua makubwa mno!!
 
aah bas tunapaswa kuwafanya walim wanasiasa tena kwa mara nyingne tena, maana tushaongozwa na walim na walim walishaheshimika siku hizo zilizopita (1984-1994). kwa hio hio heshima ya miaka 10 itarudi. kuna mahali nililazimika kua najijibu maana daah
 
"UALIMU NI WITO"
haitoshi kuwafanya walimu wadharaulike hata siku moja.Kauli mbiu hiyo ililenga kuwafanya Walimu waipende kazi yao na kuifanya kwa moyo wote;ukizingatia inahusu makuzi ya mtoto.While haki zao na stahili zikiendelea kuboreshwa kwa kadri inavyo hitajika.
Siasa za Tanzania zimepelekea kudharaulika kwa kada hiyo ambayo itaigharimu nchi hii kwa kiasi kikubwa na kwa mda mrefu.
Walimu wamepuuzwa sana na kudharauliwa jambo ambalo halita waangamiza walimu pekee bali hata wale wanao wabeza.
Mshumaa unawaka lakini unakwisha,tusijiachie na kupuuza kilio cha walimu kwa hadaa za wanasiasa wachumia tumbo.Tujitafakari upya kuinusuru kada hii muhimu kwa maendeleo endelevu ya nchi.
 
Salam.
Nnashauri, mkiandika muwe mnatumia aya maana mkiunganisha maneno namna hii habari inakosa mvuto wa kuisoma.
 
Ualimu upo hivi karibia pande zote za dunia. Pia mwanzoni kabisa, wakufunzi au walimu walikuwa ni watu wa kujitolea, ila hapo za hizo walikuwa wanaitwa wasimulizi. Walikuwa wanafundisha na kuelekeza watu maswala tofauti kwa kujitolea. Baadae ndiyo mifumo ikabadilika na kuanza kupewa motisha kama hizi za malipo.
 
Sijajua hapa mwl hasa anayepigiwa kelele no yupi,maana kuanzia ngaz ya ukufunz was vyuo vya Cheri na dip kupanda wahadhir nama prof Wao s kama ss,sasa tunamlilia mwl yupi?pia nieendelee kwa utafit mdogo ndani ya wilay flank nloufanya exdentaly walim was msing baadh vyeti,si vyao engine ni div iv mbovu,ASA kwa kua ana mapungufu hawz dai khaki yake,niende mbali said afisa mmoja alisema ktk mgomo ambay vyet ni vyage agome,alikata main watu kweli,mtoa mada ni hay tu
 
Japo kuna sababu nyingi za kwa nini ualimu ni taaluma inayotazamwa kama ya chini kimaslahi, sababu kubwa kabisa ni walimu wenyewe wanaifanya taaluma idharaulike. Mfano: walimu wengi ni wapambe wapambe wa mambo ya hovyo.hovyo ya serikali, yaani hutumika katika kazi hata zisizokuwa za profession zao. Pili, wengi hawajiamini kiuchumi, kitaaluma na kimaamuzi (waoga). Tatu, kama taaluma imekosa dira kutokana na kutawaliwa na watu wanaokata tamaa ya maisha (labda sasa hivi ambapo wengi wameanza kujikwamua kwa kufanya shughuli binafsi za kiuchumi). Nne, kukosa maamuzi ya kimsimamo wa pamoja katika kuamua mambo yanayowahusu, mfano: masuala mtambuka yanayohusu kada hii yanaamuliwa na tume ya utumishi wa umma ama TSD alhali hakuna chombo rasmi cha kuamua kuhusu masuala nyeti ya kitaaluma na kimaslahi ya walimu.

Mbali na sababu za ndani ya taaluma, sababu zingine kubwa ni utashi wa kisiasa katika kuboresha taaluma hiyo na mazingira yake ya kazi toka kwa watawala.

Yapo mengi tu lakini kwa kumalizia nikwambie adui wa mwalimu ni mwalimu mwenyewe na mfumo. CWT haitokaa imkomboe mwalimu maana matatizo yanayowakabili walimu yakiisha, wale waajiriwa wa CWT waishi vipi? Ni kwa nini walimu wanapambana kuajiriwa kama makatibu wa wilaya na mikoa wa CWT? Kwa nini maslahi ni mazuri CWT tofauti na kazi ya ualimu?

Nukuu: "Ukioa Mwalimu una tabu kwelikweli" (Kikwete, J. M., 2015, May 1st. Mwanza)
 
Ualimu upo hivi karibia pande zote za dunia. Pia mwanzoni kabisa, wakufunzi au walimu walikuwa ni watu wa kujitolea, ila hapo za hizo walikuwa wanaitwa wasimulizi. Walikuwa wanafundisha na kuelekeza watu maswala tofauti kwa kujitolea. Baadae ndiyo mifumo ikabadilika na kuanza kupewa motisha kama hizi za malipo.

cindani.... coz kuna nchi kama uingereza waalimu wanathaminiwa sana...mfano kimaslahi.... pia status zao zipo juu kama ualimu kipindi cha miaka ya 60s-80s hapa tz
 
Ualimu upo hivi karibia pande zote za dunia. Pia mwanzoni kabisa, wakufunzi au walimu walikuwa ni watu wa kujitolea, ila hapo za hizo walikuwa wanaitwa wasimulizi. Walikuwa wanafundisha na kuelekeza watu maswala tofauti kwa kujitolea. Baadae ndiyo mifumo ikabadilika na kuanza kupewa motisha kama hizi za malipo.

Kweli kabisa madai ya walim wamekua n dunian kote ila kuna nchi zmefanya jitihada kubwa za kuwakomboa walimu,kwann sio Afrika? Kwann Sio TANZANIA??
 
Sijajua hapa mwl hasa anayepigiwa kelele no yupi,maana kuanzia ngaz ya ukufunz was vyuo vya Cheri na dip kupanda wahadhir nama prof Wao s kama ss,sasa tunamlilia mwl yupi?pia nieendelee kwa utafit mdogo ndani ya wilay flank nloufanya exdentaly walim was msing baadh vyeti,si vyao engine ni div iv mbovu,ASA kwa kua ana mapungufu hawz dai khaki yake,niende mbali said afisa mmoja alisema ktk mgomo ambay vyet ni vyage agome,alikata main watu kweli,mtoa mada ni hay tu

hapa mwalim anaezungumziwa ni kuanzia degree kushuka hawa wahadhir wao kidogo sio wa kundi hilo.hali ni tete kwa hapa wa cheti mpaka shahada.izo n changamoto za kitaaluma na ndio maana baada ya kupuuzwa si tuu kimaslahi bali pia kitaluuma ikaleta mkanganyikp na taaluma ya ualimu ikaharibiwa,. serikal ina mambo mawili ya kufanya,

1. kurudisha heshima ya taaluma ya ualimu
2. kubiresha maslahi ya wafanyakaz wa sekta ya elimu
 
Unaijua sheria yankwanza kabisa ya ualimu?? "UALIMU NI WITO" arguments zako zoote ziwe arround hii basic principle of ualimu ndo tuanze mjadala sasa..

Hata utabibu pia ni Wito, tafta theory inayo elezea kazi ambazo ni Volunteerism, ni teaching na utabibu lkn utabibu unajaliwa sana, hoja ya Wito hufia hapa
 
Back
Top Bottom