Mjadala juu ya taaluma ya ualimu

Mjadala juu ya taaluma ya ualimu

Japo kuna sababu nyingi za kwa nini ualimu ni taaluma inayotazamwa kama ya chini kimaslahi, sababu kubwa kabisa ni walimu wenyewe wanaifanya taaluma idharaulike. Mfano: walimu wengi ni wapambe wapambe wa mambo ya hovyo.hovyo ya serikali, yaani hutumika katika kazi hata zisizokuwa za profession zao. Pili, wengi hawajiamini kiuchumi, kitaaluma na kimaamuzi (waoga). Tatu, kama taaluma imekosa dira kutokana na kutawaliwa na watu wanaokata tamaa ya maisha (labda sasa hivi ambapo wengi wameanza kujikwamua kwa kufanya shughuli binafsi za kiuchumi). Nne, kukosa maamuzi ya kimsimamo wa pamoja katika kuamua mambo yanayowahusu, mfano: masuala mtambuka yanayohusu kada hii yanaamuliwa na tume ya utumishi wa umma ama TSD alhali hakuna chombo rasmi cha kuamua kuhusu masuala nyeti ya kitaaluma na kimaslahi ya walimu.

Mbali na sababu za ndani ya taaluma, sababu zingine kubwa ni utashi wa kisiasa katika kuboresha taaluma hiyo na mazingira yake ya kazi toka kwa watawala.

Yapo mengi tu lakini kwa kumalizia nikwambie adui wa mwalimu ni mwalimu mwenyewe na mfumo. CWT haitokaa imkomboe mwalimu maana matatizo yanayowakabili walimu yakiisha, wale waajiriwa wa CWT waishi vipi? Ni kwa nini walimu wanapambana kuajiriwa kama makatibu wa wilaya na mikoa wa CWT? Kwa nini maslahi ni mazuri CWT tofauti na kazi ya ualimu?

Nukuu: "Ukioa Mwalimu una tabu kwelikweli" (Kikwete, J. M., 2015, May 1st. Mwanza)



Ukweli n kwamba changamoto zilizopo n za kitaaluma na kiutawala.

Unajua mwalim asa hivi anajifanyia kinyume na alivotakiwa kufanya ila sio kwa msukumo wa ndan ya moyo wake, hapana n kwasabab ya utawala unalazimisha mwal afanye hvo.

Utawala ndio uloshikilia taaluma baadala ya wanataaluma wenyewe! xo ili kuleta heshima serilali ijitoe kua muongozaji na iwe muangalizi tuu,

Kauli za viongoz juu ya walim inaonesha fika jinsi gan waafrika mawazo yetu yalivo mgando, jamii borq cio nchi kua na uchum mzur ulostawi,kua n viwanda ving n.k hapana,,, jamii bora n ustawi wa jamii..afya na maarifa n nguzo za ustawi huo.

Tunahitaji kujikomboa kifikra ili kutatua matatizo haya ambayo kwa asili tuu yanahitaji akili,hekima na busara.
 
fanya kazi mkuu kwa bidii jikomboe kiuchumi hayo mengine utajipa pressure tu


Kufanya kazi kupo pale pale lakin unafanya kaz kwa nan na kwann?? unaweza kufanya kaz kubwa na kwa bidii ukanufaika kidogo saaana. Na si vema kua tunafumbia macho dhamb ambazo tunaziona..

Kuna mtu alishasema dunia haitaharibiwa na watu wanaotenda mabaya,ila na watu wema wanaoshuhudia mabaya na kuacha yatokee. namuunga mkono.

mwal Nyerere alisema inawezekana chukua nafas yako...hata mm basema kweli nikichukua nafas yangu na mwingne nafas yake bas ITAWEZEKANA.
 
Naamini kuwa watu ambao walifanya tafiti kuhusiana na ualimu,walimu na sekta ya Elimu,mmoja wapo ni Kipilipili au @xiexie
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom