Mjadala: Je, ni sahihi kuweka udhaifu na siri za ex wako hadharani?

Kweli kabisa
Kwanza ukimwambia mtu siri za ex wako ni sawa na kuvujisha pepa yani unampa majibu ya mtihani ambao hajaanza kuufanya.
Kwa hiyo kila mara ataepuka kufanya yaleee ulomwambia kuhusu ex wako na hatakuwa aishi uhalisia wake so pretending zitakuwa nyingi.

Ukiachana na mtu alafu ukapata mpya mwambie tu tulishindwana tabia tukaamua kuachana
 
Inakeraa eeh
Ni kawaida tu;kuna siku nilitoka na mchepuko tukaenda kupata moja baridi bahati mbaya x wake akafika katika ile centre akawa anakunywa pombe na kumtolea maneno machafu...mimi niko kimya tu,waungwana ndio wakaja kumtoa pale ili asilete fujo.Nilichogundua jamaa bado anampenda x wake ila ke ndio amtaki;nami nikamwambia ukweli jamaa bado anakuitaji,lakini ke akabaki kusema zilipendwa.
 
Habari wapendwa wa JF?

Leo naomba tujadili hili suala maana hata mimi nimekuwa muhanga namba moja wa kufanyiwa vitendo kama hivi.

Baada ya kuachana na mpenzi wako unashangaa anaanza kutoa maneno machafu juu yako anasema udhaifu wako.

Siri zote mlizoongea anazitoa.

Hata hapa JF uki-date na member baadae mkaachana kimya kimya baadhi hufikia stage ya kuja kutoa siri za wenza wao ambao ni member wa JF.

Hii inamaanisha nini? Ushamba au ujanja?

Aisee katika kitu siwezi ni kutaja madhaifu ya x wangu hata siri zake lakini wengine wamekuwa hawawezi kujizuia na kuamua kutoa madhaifu ya x zao.

Halafu kinachokera wanataja mpaka majina yaani unachafuliwa sana.

Najiuliza mtu anayefanya kitendo hiki huwa ana lengo gani?

Karibuni tujadili na tushauriane jinsi ya kukabiliana na kadhia hii.

Location: Kizundi Africana Dar.View attachment 1080661

Huo ni uzwazwa grade A+
 
Nimesoma comments zote, lakini sijaona sehemu mkielezea kuwa ni jinsia gani inaongoza kwa haka katabia.
Binafsi siwezi kutoa mapungufu ya x-wangu hiyo ni nadhiri nimejiwekea.

Kuna mdada nilikutana naye humu, tuliishi miaka kama 3 hivi baadae tukaja kuachana lakini mpaka leo na hakika hajui sababu kubwa ya kuachana nae ni nini. Alikua ni mdada mwenye heshima mpaka familia ilimkubali sana kiasi kwamba mara kwa mara wananiuliza kwa nini niliachana na lakini sijawahi kusema sababu hadi leo ni miaka kama 4 imepita.

Nikirudi kwenye maada, haka katabia wanako wanawake kwa asilimia kubwa. na mara nying ndio wanaaonza, usipokuwa mvumilivu utajikuta na wewe unaropoka.
 
Na wanaume piah nahisi ndio wanaongoza

Back
Top Bottom