Mimi ndio Baba na mimi ndio Mama. Je, ni sahihi?

DALALI MKUU

JF-Expert Member
May 7, 2022
1,484
2,731
Baba ni nini?

Baba ni mzazi wa Kiume wa mtoto. Baba mzazi ni mzazi wa Kiume wa mtoto yule aliyesababisha ujauzito. Kwa maneno Mengine ni yule ambaye Mbegu zake zilikutana na yai la mama na kutunga mimba.

Siku hizi kumekuwa na Trend ya wanawake wa Mjini hasa wenye matatizo na familia zako, au na upande mmoja wa mzazi mwenzake, au wenye uwezo mkubwa wa kifedha wanaohudumia watoto wao wenyewe Kujipa Cheo cha Ubaba Utasikia mimi ndio mama na mimi ndio baba, anataka kutuaminisha kuwa Yeye ndiye aliyejipa mimba mwenyewe

Aidha single Mother wengi walioolewa na wanaume wengine Wanasema kuwa anaymelea mtoto ndiye baba yake mzazi hata kama hakumzaa,Huu ni mtego kwa wanaume anayemlea mtoto kama si wake ataitwa baba mlezi,baba wa hiyari au baba wa kambo na sio baba huwezi kujimilikisha motto kwa kumnunulia ugali

Hakuna mwanamke anayeweza kujipa mamlaka ya baba kwa namna yoyote hii kauli inatakiwa kupingwa hadharani na kukemewa vikali kabisa.

Wala usimfundishe mwanao ujinga huo wa kumpa baba mwingine kwa sababu tu abba yake mzazi hana uwezo wa kumhudumia ama kwa sababu nyingine ikiwemo kukwepa majukumu ama tofauti zenu za ndani

Ukitengana na mumeo na akikataa kabisa kutoa mahitaji kwa mwanae, tafuta namna yoyote ya kufanya mumalize hizo changamoto kuna vitu vya msingi mtoto anakosa kwa upande wa baba yake

Na kwa wanaume tusipende kukwepa majukumu hata kama umetengana na mke wako jitahidi sana umhudumie mwanao kwa chakula,elimu,afya na mahitaji yake yote ya Msingi

Kama unajua kabisa huwezi kutoa huduma kwa mtoto usimtie mimba mtoto wa watu,unatengeneza laana kwenye kizazi chako

Baba bora ni yule anayejali watoto wake, na kumpenda pia mama wa watoto wake

Japo kuna wanawake wakitengana na wenza wao wanakata kabisa mawasiliano na kuhamia mji Mwingine na hata kumkataza kabisa mzazi mwenzake kuona watoto wake, tena anafikia hatua kabisa anamwambia mtoto baba yako alifia vitani, au alipotea n.k

Tunapandikiza laana ambazo hazina maana kwa watoto wetu

Nawe baba usiyemhudumia mwanao akifanikiwa acha kumsumbua kabisa mtoto wako maana ulimtenga mwenyewe

MWISHO BABA NI MZAZI WA KIUME, KAULI YA MIMI NDIO BABA NA MIMI NDIO MAMA IFE
 
Tuseme nini wakuu ngoja tusubiri tabiri zitimie

Wanamke watamfuata mwanaume nakuomba kuitwa kwa ubini wake ili kuheshimishwa
 
Wanawake ukiondoa hiyo papuchi ni watu wa Hovyo sana, kinachotuvutia kwao ni hiyo papuchi tu
 
Kusema yeye ndio baba na yeye ndio mama hiyo huwa ni lugha ya picha tu inayolenga kuweka msisitizo kwamba majukumu yote hususan yale ya kifedha na malezi anayatimiza mwenyewe pasipo kupata msaada wa mzazi mwenzie.
 
Hapana siyo sahihi, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom