Mjadala: Je, ni sahihi kuweka udhaifu na siri za ex wako hadharani?

Muzine

JF-Expert Member
May 4, 2017
32,366
60,406
Habari wapendwa wa JF?

Leo naomba tujadili hili suala maana hata mimi nimekuwa muhanga namba moja wa kufanyiwa vitendo kama hivi.

Baada ya kuachana na mpenzi wako unashangaa anaanza kutoa maneno machafu juu yako anasema udhaifu wako.

Siri zote mlizoongea anazitoa.

Hata hapa JF uki-date na member baadae mkaachana kimya kimya baadhi hufikia stage ya kuja kutoa siri za wenza wao ambao ni member wa JF.

Hii inamaanisha nini? Ushamba au ujanja?

Aisee katika kitu siwezi ni kutaja madhaifu ya x wangu hata siri zake lakini wengine wamekuwa hawawezi kujizuia na kuamua kutoa madhaifu ya x zao.

Halafu kinachokera wanataja mpaka majina yaani unachafuliwa sana.

Najiuliza mtu anayefanya kitendo hiki huwa ana lengo gani?

Karibuni tujadili na tushauriane jinsi ya kukabiliana na kadhia hii.

Location: Kizundi Africana Dar.
20190422_213609.jpeg
 
Si sawa kabisa, hata kama mmeachana hutakiwi kuanika siri na madhaifu yake, sababu alikuamini kiasi kwamba akakueleza siri zake na kama mahusiano yenu yamefika mwisho jaribu kutunza utu wako kubaliana na hali, sio kuanza kumuanika uchi mwenzio kwa wananzengo.
 
Sasa kuna wenzako anaamua kuvujisha mpaka picha za uchi anatoa kasoro zotee ndo najiuliza huwa wanatarajia nini?
Huo muda kuanza kumuongelea ex wangu nautoa wapi.

Katika vitu ambavyo sipendi mtu aniulize ni issue ya ma ex wangu.
 
Mm huwa nashangaa kwa kweli kwanini watu wanafikia hiyo hatua unashangaa kama mwanamke unaanza kuambiwa ooo huyo D ana nini mbona hata hawezi kukata kiuno?

Demu mwenyewe mfupi kama joker?
Sasa nabaki njiapanda wakat ananitongoza hakuona hizo kasoro?
Si sawa kabisa, hata kama mmeachana hutakiwi kuanika siri na madhaifu yake, sababu alikuamini kiasi kwamba akakueleza siri zake na kama mahusiano yenu yamefika mwisho jaribu kutunza utu wako kubaliana na hali, sio kuanza kumuanika uchi mwenzio kwa wananzengo.
 
kuzitoa ni ushamba na ulimbukeni ka mmemwagana ni kimya kimyakimya ka mlivyo chukuana kimya kimya,
 
Sasa kuna wenzako anaamua kuvujisha mpaka picha za uchi anatoa kasoro zotee ndo najiuliza huwa wanatarajia nini?
Sio dhambi kila mmoja anaishi kwa namna anayoona inampendeza uzuri ni kwamba kumuongelea ex sio kuvunja sheria za nchi. Wanaoamua kuwaongelea ma ex wapo na tulioamua ku mute tupo sawa.
 
Mm huwa nashangaa kwa kweli kwanini watu wanafikia hiyo hatua unashangaa kama mwanamke unaanza kuambiwa ooo huyo D ana nini mbona hata hawezi kukata kiuno?
Demu mwenyewe mfupi kama joker?
Sasa nabaki njiapanda wakat ananitongoza hakuona hizo kasoro?
Sikiliza wimbo wa Drake "Doing it bad " utapata majibu
 
Hhahaha sasa hao wanaotoa tuwafanyaje
chakumfanya kidogo inakuwa ngumu kutegemea vile mtu unakabili issue ila mimi namwambia auchune maana yameisha na hakuna haja ya kuyakuza akiendelea nitaangalia njia ya kumthibiti ikiwa ni kuwa kimya ama njia ambayo najua itamfanya awe kimya zaidi
 
Mm huwa nashangaa kwa kweli kwanini watu wanafikia hiyo hatua unashangaa kama mwanamke unaanza kuambiwa ooo huyo D ana nini mbona hata hawezi kukata kiuno?
Demu mwenyewe mfupi kama joker?
Sasa nabaki njiapanda wakat ananitongoza hakuona hizo kasoro?

Nahisi ni kama kisasi/kujiliwaza, mtu anaona sababu hawezi kuwa na wewe tena basi anajaribu kukuanika ili wengine wasiweze kuwa na wewe.
 
Mkiachana salama inakuwa powa shida inakuja pale mnaachana kwa mbwembwe utasikia mpka na vibamia vya kizungu na mabwawa yasio na majina wala kuzalisha umeme
 
Back
Top Bottom