MJADALA: Je, kuna madhara yoyote ya kufanya mapenzi wakati wa hedhi?

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24


Kufanya mapenzi wakati wa hedhi ni kitendo cha kujiusisha na mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana..Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si madhuri kwa afya ya wote wawili.Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajari sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hiloo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa siku hizi...Zifuatazo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati KE yupo katika siku zake{period}..

MADHARA KWA MWANAUME
1.Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.

2.Maambukizi katika tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.

3.Kuziba kwa njia ya mkojo.

4.Utasa au ugumba.

5.Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.

6.Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji,utelezi, au harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu.Pia hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata hufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.

MADHARA KWA MWANAMKE

1.Kupatwa na mambukizi viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID( PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.

2.Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.(Dysmenorrhea).

3.Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.

4.Utasa au Ugumba.

5.Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.

6.Athari mbaya ya kisaikolojia:Mwanamke atahisi kuwa mumewe hamjali wala mpendi bali anajali hisia zake za kingono na kwamba yeye anatumika kingono tu.Pia kuona kuwa mumewe ajali afya yake pamoja na maumivu anayoyapata lakini bado huyu mume anataka KU-DO.
MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU
Ni madhara gani mtu anaweza kupata akifanya mapenzi au tendo la ndoa na mwanamke aliyeko kwenye siku zake?
===
===
===





MICHANGO NA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
===
===
===
===
===
===
 
Kiafya haina tatizo ikiwa mwanamke hana uambukizo wa maradhi kama STD; gono, kisonono, kaswende etc. na mwanaume hana uambukizo na michubuko nk.

Hivyo ni salama kabisa ikiwa hali ya awali imejumishwa katika tathmini. Kikubwa tu ni hofu na fikra kwa kutokujua. I mean we are not well informed.

Angalizo tu ni kwamba it is not hygienic but no health d/effect if contrary is committed yaani hamna madhara kiafya. By not hygienic it means that one can stain the beddings, unpleasant boold smell, etc Kwa msaada zaidi wasiliana nami ili tufanye utafiti wa kina.

You can use condom; both male and female partner for hygiene or any other means one can find reliable.
 
Mimi ni mmoja ambao huwa siku hizi huwa siangalii huwa na DO tu. Sijaona madhara yoyote kuna wakati jamaa aliniambia kuna madhara kama kupata kansa ya kibofu na magonjwa mengie ya kibofu.

Sasa kama unafahamu lolote kuhusu hili zaidi basi mwaga hapa kila ili na wengine ambao wanaDO hii style lakini wanaogopa kusema
 

We mkali! Naona wanaume wengi na wanawake hawana tatizo wanaweka taulo la rangi mbaya chini na kunanino kama kazi Baadhi ya wanawake wanadai enjoyment yake si ya kawaida na wengine wakati huo wanakuwa horny.
 

Wewe mbona hatari utapata mshipa
 
Wewe mbona hatari utapata mshipa

We naima tumeambiwa haina madhara only that couples may become uncomfortable with the environment (hygienecally)!

Mishipa naskia huziba kama mtafanya kinyume na maumbile sasa hii ya siku za hedhi so far is okay!! I hear women get very horny during these time sasa why not explore and see the best time to enjoy sex!!!!

Doctors please come up with datas/info za kutosha.
 
Hakuna madhara yoyote kiafya, kama mwenzio yuko confortable ni ruksa ku-enjoy, hata wakati wa ujauzito ni ruksa kama mama yuko confortable, akianza uchungu anakuwa exempted, akijifungua anapumzika siku 42 tu (PEUPERAL PERIOD) wakati huu genital organs zitakuwa zinarudi to normal pre-pregnant state, then you can resume the activity to full enjoyment.
 

Unafanya hivyo sababu ya tamaa au huna 'control'? Kitu kizuri kukifanya kistaarabu ni bora zaidi kuliko kufanya tu kwa sababu unataka na unaweza kufanya hivyo.

Itakuja kutokea hata kama mwenzako anaumwa 'provided' wewe unataka na unaweza kufanya hivyo utafanya tu. Binafsi naona mambo haya ya kujamiiana yanahitaji ustaarabu na nidhamu - yaani kuyafanya kwa upendo. Muda ambao hali inakuwa hivyo tupumzike na muda ambao hali inaruhusu tunaweza kufanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…