MJADALA: Je, kuna madhara yoyote ya kufanya mapenzi wakati wa hedhi?

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
23
1620215482510.png


Kufanya mapenzi wakati wa hedhi ni kitendo cha kujiusisha na mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana..Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si madhuri kwa afya ya wote wawili.Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajari sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hiloo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa siku hizi...Zifuatazo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati KE yupo katika siku zake{period}..

MADHARA KWA MWANAUME
1.Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.

2.Maambukizi katika tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.

3.Kuziba kwa njia ya mkojo.

4.Utasa au ugumba.

5.Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.

6.Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji,utelezi, au harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu.Pia hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata hufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.

MADHARA KWA MWANAMKE

1.Kupatwa na mambukizi viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID( PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.

2.Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.(Dysmenorrhea).

3.Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.

4.Utasa au Ugumba.

5.Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.

6.Athari mbaya ya kisaikolojia:Mwanamke atahisi kuwa mumewe hamjali wala mpendi bali anajali hisia zake za kingono na kwamba yeye anatumika kingono tu.Pia kuona kuwa mumewe ajali afya yake pamoja na maumivu anayoyapata lakini bado huyu mume anataka KU-DO.
MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU
Ni madhara gani mtu anaweza kupata akifanya mapenzi au tendo la ndoa na mwanamke aliyeko kwenye siku zake?
===
Habari zenu.

Mhhhh. Wenye kutenda mambo hayo ya kuwaingilia wake au wasichana wakati wa hedhi kwenye suala la usafi hapo hawakuzingatia hivyo kweli mtu anaweza kuingiza mwili wake kwenye hali hiyo? sidhani kama inapendeza hatika hali hiyo. sasa najuiliza inakuwa hamu au laana tu maana wengine wetu hapa wanapopenda ngono kuliko kitu chochote wanashindwa hata kuvumilia hizo siku nne mpaka saba za mwanamke.

Mimi natoa ushauri wangu wa bure tu kwa wale wenye kutenda hayo ni bora zaidi kusubiri kwanza unampa muda mzuri wa mwanamke kujitayarisha anapotoka katika siku zake hizo lakini pia wewe mwenyewe unakuwa umefuga hamu yako kuliko kila siku kuparamia miti huchoki?

Uchafu tu

Stone Towner
===
habari wana bodi ya jF.

naomba msaada wenu wataalamu wa afya au we uzoefu na swala la kufanya mapenzi wakati mwanamke akiwa kwenye hedhi.

ni madhara gani mwanamume anayapata kwakushiriki tendo hilo bila kinga mwanamke akiwa hedhini??

muhimu: (sio kama unadhamiria kufanya mapenzi wakati wa hedhi)
imekua ikitokea wakati mtu unafanya mapenzi na mkeo ghafla wakati shughuli inaendelea inapelekea mwanamke kubleed na hedhi kuanzia siku hiyo hiyo au wakati ambapo zile siku zake za hedhi kuisha pengine siku moja baada au mbili mkikutana hujikuta ile damu ya hedhi ikitoka tena kana kwamba ilisahau kutoka na baada ya hapo haiendelei tena.

wataalam na wenye hekima hebu mnijuze tafadhali!!
nawasilisha.
===
Wakuu salaam,

Kama mada inavyojieleza.

Kichupa changu kilikua kimejaa sana ikabidi nimwite demu wangu ghetto siku ya leo akaniambia ana bleed mi nikawa mbishi kutokana na ukame nlionao.

Demu bila hiyana akatimba ghetto hajavaa taulo nkaona ananizingua hana bleed wala nini. Baada ya romance za hapa na pale nikampiga machine a.k.a mkuyati.

Nje Ndani nje ndani ile natoa mashine imeloa chepechepe blood, nkaghairi hapo hapo kuendelea na game mtoto akalalamika nimekua mbishi.

Sasa wakuu nauliza kuna madhara gani kumla demu wakati ana bleed kama ilivyonitokea mimi?1584779491618.png


MICHANGO NA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
nafikiri ni vizuri kujadili hili suala kwa kuwa realistic,wengi wetu tunajua heddhi inakuwa vipi,lakini nashangaa kuona watu wanazungumza kama vile kipindi hiki, wanawake huwa wanavuja damu continuously, halafu wanaosema harufu na uchafu,please lets show respect to our sisters!

hivi ni kweli wanawake huwa wananuka wakati wa hedhi? hatuko nao maofisini,kwenye madaladala nk kila siku? nani anaweza kuniambaia leo amekutana na wanawake wangapi waliokwenye hedhi,akawatambua kwasababu ya harufu mbaya wanayotoa?

Kuhusu kujamiiana wakati wa hedhi; medically hakuna madhara yeyote yaliyothibitishwa kutokea kutokana na mtu/watu kujamiiana wakati wa hedhi, ISIPOKUWA zipo hatari zinazojulikana, nazo ni urahisi wa kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ukiwemao UKIMWI.

Cha msingi,unapotaka kufanya tendo hili wakati wa hedhi, ni vema ukashirikiana na mtu unayefahamu hali yake kiafya, preferably mkeo/mwenza wako muaminifu(aliyepima?), na kabla ya tendo ni vizuri akanawa vizuri hii itapunguza uwezekanao wa ku soil bed sheets na damu (but the good news ni; damu ya hedhi haigandi na haiwezi kuweka permanent stains kwenye shuka, sabuni kidogo, imetoka!)

Pia wataalamu wenaongeza kuwa,wakati wa hedhi wanawake wengi hupata raha zaidi kuliko kipindi kingine, pengine kwa kuwa huwa relaxed, na bila hofu ya kupata mimba

Ni hayo tu!
===
Kitaalam wanasema hakuna madhara ya kitabibu zaidi ya STDs. Wengine wanasema inasaidia ku-relieve cramps.
Ila vitabu vya dini kama biblia inakataza kujamiana wakati wa hedhi.

Lakini na sisi wanaume (wenye ndoa) kwani hatuna kiasi? Think of dirty sheets and mild odor, dont you find disgusting?

Binafsi siamini kwamba its just about the man releasing the load, should that be the case basi wa hivyo wanapatika Ohio ama Ambiance-Afrika Sana.

Sasa kama 4-5 days huwezi kuvumilia akizaa unaanza kumdandia the next day? Na kwa wanaoshauri mdomo una matumizi zaidi ya kula chakula watafanya hivyo during this time?

Lakini kama mmeamua wote wawili kuchakachuana wakati ke yuko hedhi basi mnashauriwa pengine mfanyie bafuni while taking a shower. Sasa kama unakaa nyumba ya kupanga yenye bafu lipo nje tena ni pasipoti size mbinu hii haikufai kwako.

Mkifanyia kitandani basi tumia kondom esp kondom ya kike.
Doing it bare footed it might get itchy kwa mwanaume iwapo damu itakaukia kwenye mtaimbo, so you should both wash up quickly after you finish sio kufuta tu.

Mwisho wa siku: All Ladies out there dont worry too much about men, it is because of these (worries) some(men) take you for granted.

Ukiwa hedhi utafanya sarakasi zote ili a-plug in mdudu wake ili kudauni lodi lakini ujue kama huyo mwanaume ni KUNGURU basi hawa huwa hawafugiki.
===
Je, kuna madhara msichana akifanya mapenzi wakati akiwa katika hedhi (siku zake)?

Kufanya mapenzi wakati msichana yuko katika hedhi hakuna madhara yoyote kiafya kwa mwanaume wala mwanamke kama kati yao hakuna mwenye ugonjwa wa zinaa.

Ila kama mmoja wapo ana ugonjwa wa zinaa, huo ni wakati wa hatari sana kwa maambukizi, kwa sababu utando ndani ya mfuko wa uzazi unabomoka na mlango wa mfuko wa uzazi unakuwa wazi. Hivyo ni rahisi sana vijidudu vya magonjwa mbalimbali kuingia mwilini mwa msichana. Vilevile kama msichana tayari ameambukizwa na magonjwa ya zinaa, katika damu yake viko vijidudu vingi vinavyoweza kumwambukiza mvulana.

Kwa sababu mara nyingi ni vigumu kufahamu kama kati ya wapenzi hakuna mwenye ugonjwa wa zinaa, haishauriwi kujamii ana wakati wa hedhi na kama ndivyo basi kondomu itumike.

Katika jamii nyingi kujamii ana wakati mwanamke yuko wenye hedhi haikubaliki kwa sababu ya mila au dini.

Chanzo: Je, kuna madhara msichana akifanya mapenzi wakati akiwa katika hedhi (siku zake)? - AckySHINE Blog
===
Utafiti wa kisayansi umethibitisha kuwa wakati wa hedhi, mwanamke anakuwa ni kama mgonjwa na kumuingilia kunamuumiza na ni madhara kwa mume na mke mwenyewe, kwani vidudu huenda vikaingia na mwanamke akakosa kuzaa kabisa na pengine mume mwenyewe kupata ugonjwa kwani damu huwa imebeba vidudu vingi.

Kwa wale wenye kuamini dini ya Kiislam wao wanafata aya hii

Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Waambie huo ni uchafu (ugonjwa). Basi jitengeni na mwanamke wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka watwahirike. Wakisha twahirika basi waendeeni Alivyokuamrisheni Allah. hakika Allah Huwapenda wanaotubu na Huwapenda wanaojisafisha
(Qur'an 2: 222).

Aya hii ipo wazi kuwa mwanamke haifai kuingiliwa wakati huo na atakayefanya, amefanya jambo la dhambi na inabidi atubie kwa Allah kwa kutolirudia kosa hilo.

Kwa ufupi, Mtume (saw) amesema unaweza kufanya na mkeo kila kitu katika kuchezeana, Haifahi kumuingilia mpaka amalize ada yake ya hedhi.

Kwa wenye kuamini dini ya kikristo wao wanakatazwa kwa aya hii:

Leviticus 15:20-25

And if a woman have an issue, and her issue in her flesh be blood, she shall be put apart seven days: and whosoever toucheth her shall be unclean until the even.

And every thing that she lieth upon in her separation shall be unclean: every thing also that she sitteth upon shall be unclean.

And whosoever toucheth her bed shall wash his clothes, and bathe himself in water, and be unclean until the even.

And whosoever toucheth any thing that she sat upon shall wash his clothes, and bathe himself in water, and be unclean until the even.

And if it be on her bed, or on any thing whereon she sitteth, when he toucheth it, he shall be unclean until the even.

And if any man lie with her at all, and her flowers be upon him, he shall be unclean seven days; and all the bed whereon he lieth shall be unclean.

And if a woman have an issue of her blood many days out of the time of her separation, or if it run beyond the time of her separation; all the days of the issue of her uncleanness shall be as the days of her separation: she shall be unclean


Ezekiel 18:5-6
But if a man be just, and do that which is lawful and right, and hath not ... come near to a menstruous woman...

There are a few risks to sex during menstruation.

-Many STD organisms thrive in the rich menstrual flow, so any STD contracted is likely to be worse than if contracted while you were not menstruating.

-HIV is more easily passed from an infected woman during her menses.

-Herpes infections often flare up during menstruation, making transmission easier.

-Some scientists believe that sex during menstruation puts a woman at higher risk of pelvic inflammatory disease.

-It should also be noted that, even though this is the time when a woman is least likely to become pregnant, it is not impossible. Don't use menstruation as a contraceptive, because it doesn't work.

A newly published study by Dr. Winnifred Cutler of the Athena Institute for Women's Wellness, Inc. in Chester Springs, PA and her colleagues shows that engaging in coitus during menstruation is associated with heavier bleeding patterns in perimenopausal women

Coitus and Menstruation in Perimenopausal Women
===
Kufanya mapenzi na mwanamke wakati akiwa katika hedhi ni marufuku. na vile vile hata Biblia inasisitiza katika kitabu cha Mambo ya Walawi.

Mwenye nafasi na asome makatazo ya Mungu juu ya kufanya mapenzi na wanyama, ndugu ya mke/mmeo, baba, mama, ndugu, mke wa mwenzio n.k. inasisitiza zaidi kuhusu kumuingilia mwanamke aliye katika hedhi ktk kipengele hiki.

Mambo ya walawi 18:19 (walawi sura ya kumi na nane mstari wa 19) NAWE USIMKARIBIE MWANAMKE KUFUNUA UTUPU WAKE WAKATI WA KUTENGWA KWA AJILI YA UNAJISI WAKE.

Binadamu kadiri siku zinavyokwenda tunahalalisha dhambi na Kuona Mungu anakosea na sisi tupo sawa!
===
Mimi Nakujibu ikiwa Mwanamke yupo kwenye Hedhi na mume anataka tendo la ndoa Yule mwanamke anaweza kumchezea Utupu wa mume wake na huku yule mume akawa ananyonya maziwa ya mke wake basi yule mume atamaliza haja zake zote hapo.

na jibu lako la pili mwanamke akiwa kwenye siku zake wewe Mume haruhusiwi kufanya nae tendo la ndowa ni Haram kabisa kwa Dini zote mbili Dini ya Kiislam na Dini ya Kikristo imekatazwa jambo la kufanya mapenzi wakati mke wako yupo kwenye siku zake za Hedhi ni Uchafu huo Mkuu kufanya tendo la ndoa wakati mke wako yupo kwenye siku zake za Hedhi. kama wewe ni muislam soma aya hii hapa chini

2.SURA AL- BAQARA SURA 2AYA222

222. Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka wat'ahirike. Wakisha t'ahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha.


Tafsiri yake ni hii hapaa (
222. Na wanakuuliza juu ya kuwaingilia wake zenu wakati wanapo kuwa na damu ya mwezi, hedhi. Waambie kuwa hedhi ni uchafu. Basi jizuieni kuwaingilia wakati wake mpaka wat'ahirike (wasafike). Wakit'ahirika basi ingianeni nao katika njia za maumbile.

Na ikiwa mtu amefanya makosa katika haya, basi na atubu, na Mwenyezi Mungu anapenda waja wake wakithiri toba na usafi kutokana na uchafu.
I
limu za kisasa zimethibitisha kuwa wakati wa hedhi yanaweza kuwa madhara kwa kuwa zalio huweza kupata maradhi pindi likiingiliwa na vidudu vya maradhi, ambavyo ni vyepesi kuingia wakati wa kuingiliana na mwanamume. Maradhi hayo huenda yakasababisha mwanamke

asiweze kuzaa. Mwanamume naye huambukia maradhi hayo kutokana na mwanamke kwa kupitia njia za mkojo, na maradhi yakapanda juu mpaka mafigo yakaharibika, na kuathirika

vyombo vya uzazi, na mwanamume naye akawa hawezi kutia mimba. Maradhi haya huleta machungu makubwa. Watu walikuwa hawajui, lakini Mwenyezi Mungu anajua kila kitu. Na mwanamke anapo kuwa na damu anakuwa hana raghba ya kuingiliwa, basi kumuingilia wakati huo huenda kukamletea hali ya nafsi mbaya na chuki kwa jambo hilo.)


Ikiwa wewe Mkuu ni Mkristo hebu soma hapa chini


Mambo ya Walawi, Chapter 12:2-24

12:2 Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto mume, ndipo atakuwa yu najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi, ndivyo atakavyokuwa najisi.


Mambo ya Walawi, Chapter 15:19

15:19 Mwanamke ye yote, kama anatokwa na kitu, na kitu chake alichokuwa nacho mwilini mwake ni damu, ataketi katika kutengwa kwake muda wa siku saba; na mtu ye yote atakayemgusa atakuwa najisi hata jioni.


15:20 Na kitu cho chote akilaliacho katika kutengwa kwake kitakuwa najisi; na kila kitu ambacho akiketia kitakuwa najisi.

15:21 Mtu ye yote atakayekigusa kitanda chake huyo mwanamke atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.

15:22 Mtu ye yote atakayekigusa cho chote ambacho huyo mwanamke amekiketia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.

15:23 Kwamba ni katika kitanda, au cho chote alichokikalia huyo mwanamke, atakapokigusa kitu hicho, atakuwa najisi hata jioni.

15:24 Na mtu ye yote atakayelala na mwanamke na unajisi ukawa juu yake, atakuwa najisi muda wa siku saba; na kila kitanda alichokilalia kitakuwa najisi.Mkuu kwa huu Ushahidi ukifanya Mapenzi na Mwanamke mwenye Damu ya Siku Hedhi wewe ni najisi kwa muda wa siku saba. haya kazi kwako mkuu.
===
MADHARA YA KUFANYA TENDO LA NDOA WAKATI WA HEDHI.

Kufanya mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana (hedhi) ni hatari sana.

Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si madhuri kwa afya ya wote wawili.

Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajali sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hilo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa kizazi hiki.

Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati mwanamke yupo katika siku zake {period}.

MADHARA KWA MWANAUME:

- Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.

- Maambukizi katika tezi dume (Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.

-Kuziba kwa njia ya mkojo.

-Utasa au ugumba.

-Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.

-Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji, utelezi, au harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu.

Pia hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata ufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.

MADHARA KWA MWANAMKE:

- Kupatwa na mambukizi viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID (PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.

- Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.(Dysmenorrhea).

- Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.

- Utasa au Ugumba.

- Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.

- Athari mbaya ya kisaikolojia:Mwanamke atahisi kuwa mumewe/mpenzi wake hamjali wala hampendi bali anajali hisia zake za kingono na kwamba yeye anatumika kingono tu.

Pia kuona kuwa mumewe/mpenzi hajali afya yake pamoja na maumivu anayoyapata lakini bado huyu mume/mpenzi anataka tendo.

Jali afya ya mwenza wako na yako pia, vumilia acha hedhi ipite zuia hisia zako za kingono, tengeneza msisimko wakati wa tendo bila madhara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiafya haina tatizo ikiwa mwanamke hana uambukizo wa maradhi kama STD; gono, kisonono, kaswende etc. na mwanaume hana uambukizo na michubuko nk.

Hivyo ni salama kabisa ikiwa hali ya awali imejumishwa katika tathmini. Kikubwa tu ni hofu na fikra kwa kutokujua. I mean we are not well informed.

Angalizo tu ni kwamba it is not hygienic but no health d/effect if contrary is committed yaani hamna madhara kiafya. By not hygienic it means that one can stain the beddings, unpleasant boold smell, etc Kwa msaada zaidi wasiliana nami ili tufanye utafiti wa kina.

You can use condom; both male and female partner for hygiene or any other means one can find reliable.
 
Kiafya haina tatizo ikiwa mwanamke hana uambukizo wa maradhi kama STD; gono, kisonono, kaswende etc. na mwanaume hana uambukizo na michubuko nk. Hivyo ni salama kabisa ikiwa hali ya awali imejumishwa katika tathmini.

Kikubwa tu ni hofu na fikra kwa kutokujua. I mean we are not well informed. Angalizo tu ni kwamba it is not hygienic but no health d/effect if contrary is committed yaani hamna madhara kiafya. By not hygienic it means that one can stain the beddings, unpleasant boold smell, etc.

You can use condom; both male and female partner for hygiene or any other means one can find reliable.
Mimi ni mmoja ambao huwa siku hizi huwa siangalii huwa na DO tu. Sijaona madhara yoyote kuna wakati jamaa aliniambia kuna madhara kama kupata kansa ya kibofu na magonjwa mengie ya kibofu.

Sasa kama unafahamu lolote kuhusu hili zaidi basi mwaga hapa kila ili na wengine ambao wanaDO hii style lakini wanaogopa kusema
 
Mimi ni mmoja ambao huwa siku hizi huwa siangalii huwa na DO tu. Sijaona madhara yoyote kuna wakati jamaa aliniambia kuna madhara kama kupata kansa ya kibofu na magonjwa mengie ya kibofu.

sasa kama unafahamu lolote kuhusu hili zaidi basi mwaga hapa kila ili na wengine ambao wanaDO hii style lakini wanaogopa kusema

We mkali! Naona wanaume wengi na wanawake hawana tatizo wanaweka taulo la rangi mbaya chini na kunanino kama kazi :) Baadhi ya wanawake wanadai enjoyment yake si ya kawaida na wengine wakati huo wanakuwa horny.
 
Mimi ni mmoja ambao huwa siku hizi huwa siangalii huwa na DO tu. Sijaona madhara yoyote kuna wakati jamaa aliniambia kuna madhara kama kupata kansa ya kibofu na magonjwa mengie ya kibofu.

sasa kama unafahamu lolote kuhusu hili zaidi basi mwaga hapa kila ili na wengine ambao wanaDO hii style lakini wanaogopa kusema

Wewe mbona hatari utapata mshipa
 
Wewe mbona hatari utapata mshipa

We naima tumeambiwa haina madhara only that couples may become uncomfortable with the environment (hygienecally)!

Mishipa naskia huziba kama mtafanya kinyume na maumbile sasa hii ya siku za hedhi so far is okay!! I hear women get very horny during these time sasa why not explore and see the best time to enjoy sex!!!!

Doctors please come up with datas/info za kutosha.
 
Hakuna madhara yoyote kiafya, kama mwenzio yuko confortable ni ruksa ku-enjoy, hata wakati wa ujauzito ni ruksa kama mama yuko confortable, akianza uchungu anakuwa exempted, akijifungua anapumzika siku 42 tu (PEUPERAL PERIOD) wakati huu genital organs zitakuwa zinarudi to normal pre-pregnant state, then you can resume the activity to full enjoyment.
 
Wewe mbona hatari utapata mshipa

Mshipa only ukila mke wa mtu
 
Mimi ni mmoja ambao huwa siku hizi huwa siangalii huwa na DO tu. Sijaona madhara yoyote kuna wakati jamaa aliniambia kuna madhara kama kupata kansa ya kibofu na magonjwa mengie ya kibofu.

sasa kama unafahamu lolote kuhusu hili zaidi basi mwaga hapa kila ili na wengine ambao wanaDO hii style lakini wanaogopa kusema

Unafanya hivyo sababu ya tamaa au huna 'control'? Kitu kizuri kukifanya kistaarabu ni bora zaidi kuliko kufanya tu kwa sababu unataka na unaweza kufanya hivyo.

Itakuja kutokea hata kama mwenzako anaumwa 'provided' wewe unataka na unaweza kufanya hivyo utafanya tu. Binafsi naona mambo haya ya kujamiiana yanahitaji ustaarabu na nidhamu - yaani kuyafanya kwa upendo. Muda ambao hali inakuwa hivyo tupumzike na muda ambao hali inaruhusu tunaweza kufanya hivyo.
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom