Mjadala huru: Je, ni nini imekikumba Chama Cha Mapinduzi?

jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
19,092
35,890
Wakuu Habari ya jioni.

Napenda kuwakaribisha katika mjadala huru,ili kufahamu hasa nini kinachoendelea ndani ya chama kongwe Afrika.

Nimejaribu kujiuliza maswali na wala sipati jibu..
Je ni nini imekikumba cha cha mapinduzi mara baada ya mwenyekiti taifa JPM kuchukua uongozi..

Mana ukitazama haya yanayofanyika sasa ni ya kustaajabisha.

Je ni kukosa sera..?
Je ni chuki binafs dhidi ya wapinzani..?
Je ni kushindwa kuaminiwa na wananchi hivyo kutumia ubabe..?
Je ni nia ya kubadili siasa za nchi kutoka za kidomekrasia kwenda katika mlengo mwingine..?

Ni nini hasa lililo nyumba na aina hizi za siasa.

Je ni kutaka kutawala milele tena kwa mabavu..?
Je ni kuuaminisha wananchi na jumuiya za kimataifa kua inapendwa na hakuna chama cha kisiasa mbadala..?

Kimsingi najaribu kujiuliza nakosa jibu.
Karibuni kwa mjadala huru.

#MaendeleHayanaChama
 
Kuna TTETESI za mpango mkakati wa kuua CHADEMA. Mpango huo kwa sasa upo katika hatua za utekelezaji.

Mpango huu unaratibiwa kwa karibu na ofisi ya msajili baadhi ya watu.

Vyombo mbalimbali vya usalama kuhusishwa.

Mpango upo hivi;

1. Msajili awe na taarifa rasmi za ratiba ya uchaguzi ya CHADEMA ngazi ya taifa.

2. Msajili, na ofisi nyingine waandae pesa ndefu ya kununua baadhi ya wajumbe, kisha waandae safu ya viongozi mamluki.

3. Msajili na ofisi nyingine watamtuma mamluki wao akachukue fomu ya kugombea uenyekiti, na nafasi nyinginezo.

4. Endapo mamluki hao eataenguliwa vyombo vya dola vitumike kuzuia uchaguzi huo, kwa kuelekezwa na msajili.

5. Siku ya uchaguzi ikikaribia viongozi wote wa juu wa CHADEMA watakamatwa na kuwekwa ndani.

6. Kile kikundi cha mamluki kitapelekwa mahali fulani kwa uratibu wa msajili na vyombo vya dola na kutangaza kuwa uchaguzi umefanyika, na viongozi wa kitaifa wamepatikana.

7. Viongozi hao feki wa kitaifa watatambuliwa na msajili.

8. Vyombo vya usalama vitaziteka ofisi zote za CHADEMA ngazi mbalimbali na kuzikabidhi kwa wahaini/mamluki waliochaguliwa.

9. Viongozi walioondolewa watazuiwa hata kuitisha press conference.

10. Mpango mkakati utapimwa kuona namna ulivyofanikiwa kuua rasmi CHADEMA.

CHADEMA kitakuwa moja ya matawi ys CCM.

KAZI KWISHA.
 
Chama Cha Mapinduzi kimeishiwa pumzi.

Kama ilivyokuwa anguko la dola kubwa ya Kirumi ambapo dola hivyo haikuanguka kwa kupigwa vita na dola nyingine iliyoibuka yenye nguvu ya kivita bali uongozi ulioishiwa pumzi na weledi wa kiuongozi ndiyo iliyosababisha dola hiyo yenye nguvu kusambaratika.

Dola ya Kirumi kwa kukosa visheni ilitumia mamluki waliowapachika uongozi wa dola ndiyo waliojitajirisha na kulewa kila aina ya ulevi kuanzia mvinyo na ulevi wa madaraka.

Hali hii ilisababisha wazalendo wa kweli wa dola ya Kirumi kuwaachia na kuwasusia malumki wa kuja waliotetewa na uongozi wa juu waliofanya ukatili wa kila namna na kupora mali za wananchi huku wakitoza kodi kubwa kuimarisha miradi mikubwa ya miundo mbinu ikiwemo kununua merikebu kubwa kubwa na kujenga mabarabara ya mawe kuwezesha askari mamluki kwenda nchi za mbali kujitanua kimipaka na kugawana mali walizopora.

Hivyo anguko la dola la Kirumi likitokana na msuguano wa 'watawala' wenyewe ndani ya dola na siyo kushindwa vita toka uvamizi wa nje.
the Roman Empire fell slowly as a result of challenges from within and without, and changing over the course of hundreds of years until its form was unrecognizable. Because of the long process, different historians have placed an end date at many different points on a continuum. Perhaps the Fall of Rome is best understood as a compilation of various maladies that altered a large swath of human habitation over many hundreds of years. Read more: What Factors Caused the Fall of the Roman Empire?
CCM ya awamu hii imejaa mamluki walioopolewa nje ya mifumo waluozoea CCM asilia. Hii imepelekea wanaCCM asilia kuwa na silika kama ya wazalendo wa dola ya Kirumi kuususia utawala mpya wa awamu ya tano. Kususia kwao hawa wanaCCM asilia kunaanzia kujitoa kuchangia mawazo hata pale wanapoona uongozi wa juu umekosea kisera, manifesto hata vipaumbele gani vianze je ni manunuzi ya ndege na SGR au mengine yenye mguso zaidi kwa wanyonge walio wengi mijini na vijijini wanaohitaji huduma za afya bora, masoko ya mazao na siyo ndege zitakazopandwa na kikundi kidogo cha maCCM mamluki.

CCM hii inayonunua mamluki na kuwapa vyeo haraka haraka ndani ya chama na serikali yake imezua msuguano wa ndani kwa ndani baina hao na hatimaye itakuwa anguko la chama hiki kikongwe kama ilivyotokea kwa dola ya Kirumi.

Mfano hai November 2019 kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji, kelele za kupinga uhuni unaoendelea chini ya serikali ya CCM kupitia TAMISEMI kwa wingi wake zinatokea ndani ya CCM huku zikiungwa mkono kwa wingi wa wale wapinzani.

Haijawahi kutokea CCM kupigiwa kelele kwa umoja wa kitaifa toka pande zote mbili yaani ya wenye serikali na wale wa kambi ya upinzani.

Tunaona waziri wa TAMISEMI na viongozi wa juu wa CCM kaliba ya Humphrey Polepole wakitoa matamko yanayoonesha kuchanganyikiwa na vuguvugu hili jipya lenye kuitishi uwepo wake CCM katika siasa na la kuipinga serikali ya CCM.

Hakika hali hii ya wananchi wote kwa umoja wao kujitokeza kususia chaguzi za kihuni ni mwelekeo wa kuelekea Tanzania Spring inayofanana na Arab Spring ilizozikumba tawala za kidikteta ktk nch za Afrika ya Kaskazikni za Tunisia, Egypt na hivi punde kule Algeria zilizosababisha watawala kukimbia makao yao ya utawala.
 
Chama kimekuwa imara zaidi ya mlima naona tu VYAMA tunaponyoka kila uchao

State agent
 
Yapo mengi sana lakini leo nitakudokeza mambo mawili tu .

1 . Kupora mamlaka ya wanchama na kujimilikisha mtu mmoja tu , angalia uchaguzi wa marudio wa ubunge , hakukuwa na kura za maoni , uamuzi ulikuwa ni wa mungu - mtu mmoja tu , jambo hili liliwafanya wanaccm wajione hawana tena chama wakaamua kumwachia mwenyewe , amewanyang"anya hata malazo ya magari .

2.Jambo la pili lililoua ccm ni kutumia Polisi kutesa wananchi wanaoikosoa badala ya kuwatumia viongozi wake kufafanua , hii ni kwa sababu viongozi wa ccm wa awamu ya 5 akiwemo Polepole hawana uwezo wa kutetea chama chao , wamejikita kwenye kutumia polisi kunyamazisha wakosoaji badala ya kutetea , jambo hili limewafanya wanaccm wenye akili timamu kuona aibu na kuamua kujiondoa kimya kimya ili kuepuka kutekwa na kuuawa.

Kikwete aliwahi kutabiri anguko la ccm ikiwa wataamua kutumia polisi badala ya makada wao , ambapo aliwaambia wanaccm kufafanua maendeleo waliyoleta badala ya kutegemea polisi kudhibiti wakosoaji " Tukitumia polisi tutashindwa , na tutashindwa kweli kweli "
 
Vyama vya upinzani mmesahau yale mavurugu mliokua mkifanya kwenye vituo vya kupigia kura na kuhonga au kutoa rushwa kwa wasimamizi wa uchaguzi.

Je mlishawahi kukemea hayo mambo ya uchafuzi wa uchaguzi?

Sasahivi mnabwekabweka kumbe ni mbwa Koko.

Wabunge mliowachagua wameishia kuwakimbia,maana mlihamasishana kwa uzalendo wa kunywa viroba

Sasa huu ni upinzani au upumbavu
una akili timamu ?
 
Chama kilikuwa kinaishi kwa kutegemea mizizi yake ya muda mrefu ingawa madani yalishaanza kupotea. Jembe kutoka Chato likalima ile mizizi.
 
Wakuu Habari ya jioni.

Napenda kuwakaribisha katika mjadala huru,ili kufahamu hasa nini kinachoendelea ndani ya chama kongwe Afrika.

Nimejaribu kujiuliza maswali na wala sipati jibu..
Je ni nini imekikumba cha cha mapinduzi mara baada ya mwenyekiti taifa JPM kuchukua uongozi..

Mana ukitazama haya yanayofanyika sasa ni ya kustaajabisha.

Je ni kukosa sera..?
Je ni chuki binafs dhidi ya wapinzani..?
Je ni kushindwa kuaminiwa na wananchi hivyo kutumia ubabe..?
Je ni nia ya kubadili siasa za nchi kutoka za kidomekrasia kwenda katika mlengo mwingine..?

Ni nini hasa lililo nyumba na aina hizi za siasa.

Je ni kutaka kutawala milele tena kwa mabavu..?
Je ni kuuaminisha wananchi na jumuiya za kimataifa kua inapendwa na hakuna chama cha kisiasa mbadala..?

Kimsingi najaribu kujiuliza nakosa jibu.
Karibuni kwa mjadala huru.

#MaendeleHayanaChama
 
Wakuu Habari ya jioni.

Napenda kuwakaribisha katika mjadala huru,ili kufahamu hasa nini kinachoendelea ndani ya chama kongwe Afrika.

Nimejaribu kujiuliza maswali na wala sipati jibu..
Je ni nini imekikumba cha cha mapinduzi mara baada ya mwenyekiti taifa JPM kuchukua uongozi..

Mana ukitazama haya yanayofanyika sasa ni ya kustaajabisha.

Je ni kukosa sera..?
Je ni chuki binafs dhidi ya wapinzani..?
Je ni kushindwa kuaminiwa na wananchi hivyo kutumia ubabe..?
Je ni nia ya kubadili siasa za nchi kutoka za kidomekrasia kwenda katika mlengo mwingine..?

Ni nini hasa lililo nyumba na aina hizi za siasa.

Je ni kutaka kutawala milele tena kwa mabavu..?
Je ni kuuaminisha wananchi na jumuiya za kimataifa kua inapendwa na hakuna chama cha kisiasa mbadala..?

Kimsingi najaribu kujiuliza nakosa jibu.
Karibuni kwa mjadala huru.

#MaendeleHayanaChama

Tatizo ni bwana mawe!
 
Umeeleza vyema sana
Chama Cha Mapinduzi kimeishiwa pumzi.

Kama ilivyokuwa anguko la dola kubwa ya Kirumi ambapo dola hivyo haikuanguka kwa kupigwa vita na dola nyingine iliyoibuka yenye nguvu ya kivita bali uongozi ulioishiwa pumzi na weledi wa kiuongozi ndiyo iliyosababisha dola hiyo yenye nguvu kusambaratika.

Dola ya Kirumi kwa kukosa visheni ilitumia mamluki waliowapachika uongozi wa dola ndiyo waliojitajirisha na kulewa kila aina ya ulevi kuanzia mvinyo na ulevi wa madaraka.

Hali hii ilisababisha wazalendo wa kweli wa dola ya Kirumi kuwaachia na kuwasusia malumki wa kuja waliotetewa na uongozi wa juu waliofanya ukatili wa kila namna na kupora mali za wananchi huku wakitoza kodi kubwa kuimarisha miradi mikubwa ya miundo mbinu ikiwemo kununua merikebu kubwa kubwa na kujenga mabarabara ya mawe kuwezesha askari mamluki kwenda nchi za mbali kujitanua kimipaka na kugawana mali walizopora.

Hivyo anguko la dola la Kirumi likitokana na msuguano wa 'watawala' wenyewe ndani ya dola na siyo kushindwa vita toka uvamizi wa nje.

CCM ya awamu hii imejaa mamluki walioopolewa nje ya mifumo waluozoea CCM asilia. Hii imepelekea wanaCCM asilia kuwa na silika kama ya wazalendo wa dola ya Kirumi kuususia utawala mpya wa awamu ya tano. Kususia kwao hawa wanaCCM asilia kunaanzia kujitoa kuchangia mawazo hata pale wanapoona uongozi wa juu umekosea kisera, manifesto hata vipaumbele gani vianze je ni manunuzi ya ndege na SGR au mengine yenye mguso zaidi kwa wanyonge walio wengi mijini na vijijini wanaohitaji huduma za afya bora, masoko ya mazao na siyo ndege zitakazopandwa na kikundi kidogo cha maCCM mamluki.

CCM hii inayonunua mamluki na kuwapa vyeo haraka haraka ndani ya chama na serikali yake imezua msuguano wa ndani kwa ndani baina hao na hatimaye itakuwa anguko la chama hiki kikongwe kama ilivyotokea kwa dola ya Kirumi.

Mfano hai November 2019 kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji, kelele za kupinga uhuni unaoendelea chini ya serikali ya CCM kupitia TAMISEMI kwa wingi wake zinatokea ndani ya CCM huku zikiungwa mkono kwa wingi wa wale wapinzani.

Haijawahi kutokea CCM kupigiwa kelele kwa umoja wa kitaifa toka pande zote mbili yaani ya wenye serikali na wale wa kambi ya upinzani.

Tunaona waziri wa TAMISEMI na viongozi wa juu wa CCM kaliba ya Humphrey Polepole wakitoa matamko yanayoonesha kuchanganyikiwa na vuguvugu hili jipya lenye kuitishi uwepo wake CCM katika siasa na la kuipinga serikali ya CCM.

Hakika hali hii ya wananchi wote kwa umoja wao kujitokeza kususia chaguzi za kihuni ni mwelekeo wa kuelekea Tanzania Spring inayofanana na Arab Spring ilizozikumba tawala za kidikteta ktk nch za Afrika ya Kaskazikni za Tunisia, Egypt na hivi punde kule Algeria zilizosababisha watawala kukimbia makao yao ya utawala.
 
Mkeo akisoma maandishi yako haya atakukimbia
Vyama vya upinzani mmesahau yale mavurugu mliokua mkifanya kwenye vituo vya kupigia kura na kuhonga au kutoa rushwa kwa wasimamizi wa uchaguzi.

Je mlishawahi kukemea hayo mambo ya uchafuzi wa uchaguzi?

Sasahivi mnabwekabweka kumbe ni mbwa Koko.

Wabunge mliowachagua wameishia kuwakimbia,maana mlihamasishana kwa uzalendo wa kunywa viroba

Sasa huu ni upinzani au upumbavu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom