Mjadala alioanzisha Tundu Lissu ni, Je Katiba Mpya italeta nafuu ya Maisha kwa Mtanzania?

Tunachozungumza ni mfumuko wa bei ambao ipo duniani kote na sisi tuna afadhali kuliko nchi zozote, Ufilipino na katiba Yao wameshindwa kuzuia kitunguu kimoja kuuzwa kwa sh.23000/= za Kitanzania jambo ambalo ni ajabu kwa bei wananchi wa Ufilipino.
Kenya wana katiba Bora ila mfumuko wa bei unawatesa mno, South Africa Wana mfumo bora ila bado mfumuko wa bei unawatesa.
Ufilipino bei gani double trip
 
Mleta mada uko na uelewa mdogo sana wa katiba. Usichojua ni kuwa mambo me gi yanayofanywa leo uhalali wake unatajwa kuwa ni kaiba tuliyoandika 1977. Na hata yanayofanywa kinyume na katiba hiyo (kwa sababu ya nyakati mpya) hayana uhalali kwa sababu hayako katika katiba. Kwa hiyo, kuwa na katiba inayokidhi matakwa ya muda ni muhimu!

Unahoji kama katiba itapunguza bei ya vitu. Bei haipunguzwi na katiba! Lakini katiba inaweza kuweka muongozo wa nini kifanyike katika bidhaa muhimu. Bei ni matokeo ya policies za kiuchumi ambazo ni za kisiasa!! Kama JPM aliweza kulazimisha bei zibaki chini, kwanini isiwe hivo kwa SSH???? Mmoja anaamua kutoongeza mishahara kwa miaka mitano mfululizo. Mwingine anakuja anaongeza, hata kama ni kidogo. Mmoja anasema bei ya kuunganisha umeme ni 27,000. Mwingine anasema ni ile itakayoamliwa na TANESCO. Nchi hii inanunua magari ya bei ghali huku vijana hawana ajira, wanafunzi wakikaa chini nk. Kila mtu anafanya yake kwa kutumia mamlaka aliyopewa ambayo hayakuwa na udhibiti nje ya mamlaka yenyewe!!

Katiba sio suluhisho la bei. Katiba ni muongozo unaotoa haki, usawa, na kuweka misingi ya utawala bora ili shughuli za wananchi ziwe ni kwa faida hao. Kama huwezi kuona katika mapana zaidi ya bei - endelea na shughuli zako. Na wala hutaona bei zikipungua hata kwa katiba hii.
 
Mleta mada uko na uelewa mdogo sana wa katiba. Usichojua ni kuwa mambo me gi yanayofanywa leo uhalali wake unatajwa kuwa ni kaiba tuliyoandika 1977. Na hata yanayofanywa kinyume na katiba hiyo (kwa sababu ya nyakati mpya) hayana uhalali kwa sababu hayako katika katiba. Kwa hiyo, kuwa na katiba inayokidhi matakwa ya muda ni muhimu!

Unahoji kama katiba itapunguza bei ya vitu. Bei haipunguzwi na katiba! Lakini katiba inaweza kuweka muongozo wa nini kifanyike katika bidhaa muhimu. Bei ni matokeo ya policies za kiuchumi ambazo ni za kisiasa!! Kama JPM aliweza kulazimisha bei zibaki chini, kwanini isiwe hivo kwa SSH???? Mmoja anaamua kutoongeza mishahara kwa miaka mitano mfululizo. Mwingine anakuja anaongeza, hata kama ni kidogo. Mmoja anasema bei ya kuunganisha umeme ni 27,000. Mwingine anasema ni ile itakayoamliwa na TANESCO. Nchi hii inanunua magari ya bei ghali huku vijana hawana ajira, wanafunzi wakikaa chini nk.

Katiba sio suluhisho la bei. Katiba ni muongozo unaotoa haki, usawa, na kuweka misingi ya utawala bora ili shughuli za wananchi ziwe ni kwa faida hao. Kama huwezi kuona katika ma mapana zaidi ya bei - endelea na shughuli zako. Na wala hutaona bei zikipungua hata kwa katiba hii.
Una hakika Katiba iliandikwa 1977?
 
Ufilipino bei gani double trip
Screenshot_20230125-194021.png
 
Katika yote aliyoongea Tundu Lisu la Msingi ni kupanda mno kwa gharama za maisha ikiwemo Watu baadhi kula mlo mmoja kwa siku

Lisu anaamini Katiba Mpya ndio suluhisho

Je, ni kweli?

Nilitegemea Wachumi wa nchi hii wangekuwa mjadalani tayari lakini wapi!

Mimi najiuliza Uingereza Wana hali ngumu sana ya maisha kwa sasa na wako kwenye migomo endelevu, Je Katiba yao ni Mbaya itawabidi wapate mpya?

Mungu awabariki sana!
Lissu hajasema katiba mpya itashusha bei za vyakula na bidhaa nyingine. Ni mambo mawili tofauti. Tunahitaji katiba mpya, ni suala moja. Kuhusu bei kupanda, (kiasi Cha sehemu kubwa mno ya jamii kushindwa kumudu) ni matokeo ya sera mbovu za serikali na usimamizi mbovu wa watendaji ktk sekta tofauti. Vinginevyo bei za bidhaa ni kawaida Kila mara kupanda. Tatizo liko kwenye kipato. Wengi ktk jamii vipato aidha vimebaki pale pale au vimeporomoka. Inajulikana wazi ndani ya miaka sita iliyopita, Kuna matajiri wengi 'walinyang'anywa' pesa zao, wengine walitorosha mitaji, biashara nyingi zilidorora/zilifungwa kabisa. Tunajua pia wakulima walipatwa na majanga, eg korosho huko kusini, mbaazi huko Arusha na Manyara etc. Yote haya yaliondoa fedha nyingi kwenye mzunguko, na ndiyo imesababisha hali ngumu ya maisha iliyoko mtaani Sasa.
Kwahiyo msipotoshe kwa makusidi alichozungumza Lissu. Tunahitaji KATIBA MPYA Sasa. Pia msiwadanganye watanzania muwaletee Ile katiba iliyopendekezwa na bunge la ccm. Ile walisha ichakachua kwa maslahi yao. Rasimu ya tume ya jaji Warioba ndiyo yenye maoni ya wananchi.
 
Unawaza kula tu……

Katiba mpya/bora ni zaidi ya kuwaza kula.

Hopeless minds.
Hujui njaa wewe.
Kula ni muhimu kuliko hata katiba mpya.
Hufahamu chochote kuhusu uchumi na jinsi ilivyo muhimu katika dunia na umedandia mada.
You quoted me with this content of yours without even thinking.
Sio kila tatizo lihusishwe na Katiba, Katiba haiwezi solve inflation ambayo imesababishwa na world economic factors, kaa ujue hilo.
Nenda Kenya wenye katiba Bora, ulizia bei zao za vyakula, they are sky rocketing .
Wajua kilichomuondosha Truss madarakani? Kushuka kwa paundi na mfumuko mkali wa bei, je Uingereza si wana katiba bora?
 
Una hakika Katiba iliandikwa 1977?
Mkuu umeulizwa swala la msingi kwa maneno ya mzaha. Sio kila Katiba inapofanyiwa marekebisho katika kifungu kimoja basi ile mama inaachwa kuitwa katiba na hiki kifungu kipya kinaifanya katiba nzima kuitwa mpya!! Katiba ilikuwa na nafasi ya kuwa mpya kupitia Bunge la Katiba wakati wa JK. CCM ilifany mchakato kama huo wa mwisho mwaka 1977!! Katiba yenyewe inalipa mamlaka yenye ukomo Bunge kufanya mabadiliko madogo.

Kujibu swali lako, katiba TULIYONAYO ni ile iliyopitishwa 1977 kwa mara ya mwisho.
 
Katika yote aliyoongea Tundu Lisu la Msingi ni kupanda mno kwa gharama za maisha ikiwemo Watu baadhi kula mlo mmoja kwa siku

Lisu anaamini Katiba Mpya ndio suluhisho

Je, ni kweli?

Nilitegemea Wachumi wa nchi hii wangekuwa mjadalani tayari lakini wapi!

Mimi najiuliza Uingereza Wana hali ngumu sana ya maisha kwa sasa na wako kwenye migomo endelevu, Je Katiba yao ni Mbaya itawabidi wapate mpya?

Mungu awabariki sana!
Sio Hilo tuu.
Tangu aguse bei ya vyakula kupanda si umeiona wanavyopishana na maneno ya bei hizi. Mbona hawakuliona tangu awali.
Wameshibisha matumbi yao basi wanakata kimya!
Tuelezeni pesa na plea bargaining ziliko msituyumbushe.
KATIBA mpya ndio muarobaini msijifanye!!
 
Back
Top Bottom