saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 602
- 1,407
Magazeti ya leo yamemnukuu Tundu Lissu akisema ugumu wa maisha hautokani na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan bali ni unatokana na Katiba.
1. Lissu nakuuliza Kwani Katiba ndio imefungua mipaka ya nchi yetu na kuruhusu Wakenya,Wanyarwanda,Wakongomani na Warundi kumiminika hadi mashambani huko vijijini kulangua mazao? hali ilikuwaje miaka ya Magufuli?
2. Katiba ndio imeweka Tozo za miamala ya kibenki na mitandao ya simu? hali ilikuwaje miaka mitano ya Magufuli?
3. Je! Katiba ndio imesababisha wakulima kukosa mbolea na kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa mazao?
4. Katiba ndio imesababisha umeme ukatike mara kwa mara na kusababisha uzalishaji viwandani kushuka na kupandisha bei za bidhaa?
Katiba mpya ni hitaji muhimu lakini kuna matatizo hayasababishwi na Katiba na wewe umekwepa kusema waliotufikisha hapa kwa sababu unazozijua wewe na kusingizia Katiba.
Miaka 5 ya Magufuli tulikuwa tunatumia Katiba gani wakati mchele ukiuzwa 900 hadi 1,200 na sasa tunatumia Katiba gani mchele ukiuzwa 4,000