Mizungu/misemo huelimisha na kuburudisha jamii

Didododi

JF-Expert Member
Jul 21, 2023
321
426
Mizungu ni kauli zinazotumia lugha ya picha na mafumbo ili kuelezea vipengele mbalimbali vya mila na za jamii fulani. Mara nyingi mizungu hutumika kufunza miiko mbalimbali kwa watoto ambao wameingia Katika kundi la watu wazima.

Mfano kabila la Wandengereko hutumia msemo Mtandawala mti pakaya mzuri mno ngaufai jengo, sawa na msemo wa kiswahili Papai limeivia nyumbani siwezi kulila.

Katika muktadha huu vijana wanafundishwa kwamba dada Yako hata akiwa mrembo kiasi gani haifai kumuona.

==========

Tupia mzungu/Msemo wowote na maana yake wadau wa lugha tujikumbushe hata kama ni wa kikabila kikubwa tafsiri iwepo
#Semi yoyote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom