Mizengo Pinda ni Mtu wa Ajabu Sana

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Taarifa za Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kutangaza nia ya kugombea Urais mwaka 2015 iliwashitua wengi sana hasa wakulima ambao hadi hivi sasa hawana mahali pa kuuza mahindi yao huku, Pinda akiwa hana majibu ya matatizo haya ya wakulima. Mizengo Pinda ambaye amekuwa waziri mkuu wa Tanzania kwa miaka ipatayo saba sasa, akiwa ameshindwa kabisa kuongoza nchi anatafuta Urais?

Waziri mkuu Pinda ambaye ndiye mtendaji mkuu wa nchi anatambua wazi kwamba chini ya utawala wake nchi imepitia misukosuko mingi ikiwamo ya migogoro ya kidini, ugaidi, kuongezeka kwa kiwango cha umasikini wa kaya, kuongezeka kwa idadi ya watoto wa mitaani, kuongezeka kwa idadi ya mambumbu, huku hali ya miundombinu ya nchi ikiwa mbaya kupindukia. Nchi hivi sasa inashuhudia ukosefu mkubwa wa maji vijijini na mijini, huku kitendawili cha umeme wa uhakika kikiwa kimekosa mteguaji. Tatizo la foleni za barabarani likionekana kama ni fahari machoni pa watawala hawa waliozoea kupitishwa barabarani kwa ving'ola.

Ni katika utawala huu wa Pinda na Kikwete nchi imejikuta ikiwa kwenye lindi kubwa la madeni ya nje na ndani. Huku deni la nje likikua kwa kasi ya kutisha, deni la ndani sasa linatishia hata mstakabali wa maisha ya watanzania. Kimefikia kiwango cha watanzania kuanza kukosa dawa mahospitalini kutokana na nchi kushindwa kulipa madeni yake. Wakandarasi wanalalamikia kutokulipwa pesa zao baada ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya serikali. wasambazaji wa vyakula mashuleni wapo mbioni kugoma huku baadhi ya vyuo vya elimu ya juu na diploma vikifungwa kutokana na kushindwa kulipa bili za maji na umeme.

Hali ya nchi kiujumla inakatisha tamaa. Huyu Pinda ambaye ameshindwa kutumia nafasi yake kutatua au hata kupunguza ugumu huu wa maisha ya watanzania, akiwawaacha wakulima wakiwa na hali mbaya kiasi cha vijana wengi kutokutamani kukaa vijijini, anaota kuwa Rais? Hii ni ajabu sana, na kwa hakika namuona Pinda kuwa ni mtu wa ajabu sana. Sikutarajia mtu aliyeshindwa kuongoza nchi katika nafasi ya uwaziri mkuu, aweze kufikiria kuongoza nchi katika nafasi ya u-Rais. Ni vizuri Pinda akajiengua katika kinyang'anyilo hiki kuliko kujidhalilisha kutafuta madaraka asiyokuwa na uwezo nayo.
 
mpelekeee mbowe hizo pumba wewe msukule

nadhani hata wewe umemuona #mlevi huyu anavyobwabwaja.

Wana akili fupi watu hawa. Lowasa hawamzungumzii. Wanamsapoti sana kwani wanajua akisimama na Upinzani,itakuwa rahisi sana kuing'oa CCM kwani udhaifu wake (lowasa) uko njenje na ni mchafu.

Pinda anawanyima usingizi watu hawa.

NA BADO!
 
Mimi anachonishangaza ni uwa analalamika tu.Sasa nani wa kuchukua hatua!!

Yeye inafaa awe anachukua hatua si kulalamika lalamika tu
 
Mimi anachonishangaza ni uwa analalamika tu.Sasa nani wa kuchukua hatua!!

Yeye inafaa awe anachukua hatua si kulalamika lalamika tu

Njoo mpanda huku na sumbawanga ndo huseme hayo kama tutawaelewa hatukupata barabara ya rami mpaka tumemweka kijana wetu ,viva pinda kwa uadilifu, kuwa rahisi uimalizie toka mpanda mpaka kigoma na ile ya tabora
 
kwan mtoa mada unamzungumzia pinda yupi? yule mtoto wa mkulima anaetembea na vx? au yule jamaa wa kulialia badala ya kutatua tatizo? au yule jamaa alieamuru watz wapigwe tu? au unamzungumzia yule handsome boy(man)? au yule anaeshindwa kusimamia kodi za watz alafu anaenda kuomba msaada wa madawati kwa mabepari? au yule anaeangalia mikataba mibovu ikisainiwa na mawaziri wake? au yule aliewapiga changa la macho waislamu kuhusu mahakama ya kadhi? au yule anaepita mitaa ya posta na mgari wake huku akishuhudia watoto ombaomba wamekosa elimu huku yeye akimuagiza dereva aongeze "ac" na afunge vioo? daah ni yupi bro? nisaidie!
 
yaani hajitambui, mimi kuna wakati huwa nadhani ana tatizo la msongo wa mawazo maana sioni anacho fanya zaidi ya kusubiri ratiba ya chakula!! NI KOSA KUBWA KUMCHAGUA MTU MASIKINI NA ALITE TOKA FAMILIA MASIKINI YA KIPATO KAMA PINDA AWE RAIS NI KUJITAKIA SHIDA KUU.
 
nadhani hata wewe umemuona #mlevi huyu anavyobwabwaja.

Wana akili fupi watu hawa. Lowasa hawamzungumzii. Wanamsapoti sana kwani wanajua akisimama na Upinzani,itakuwa rahisi sana kuing'oa CCM kwani udhaifu wake (lowasa) uko njenje na ni mchafu.

Pinda anawanyima usingizi watu hawa.

NA BADO!
Pinda ni babako? Kumpigia debe mtu mchovu kiuongozi kama Pinda, ni ulimbukeni na dalili za kuchanganyikiwa.
 
Mizengo Kayanza Peter Pinda-Haiba yake,UADILIFU wake,unawatisha MANYANG'AU na wasaka tonge WENGI
 
Pinda, sawa na Mtanzania mwingine yeyote yule mwenye vigezo; ana haki ya kutangaza nia na kugombea urais! Hata hivyo, labda CCM wawe stupid kupindukia ndipo wanaweza kumpitisha Pinda ambae kwangu mimi, ni the worst PM ever happened in the history!

CCM wakimpitisha Pinda basi wajiandae kugawana mali wanazomiliki coz' itakuwa ndo kitu pekee walichobakiwa nacho!
 
Pinda hana uwezo wa kuongoza nchi yeye aendelee tu kufuga nyuki!!!!! Tunahitaji rais jasiri na siyo mtu anayelilia ovyo kama katoto kalichonyang'anywa pipi!!!!!
 
Njoo mpanda huku na sumbawanga ndo huseme hayo kama tutawaelewa hatukupata barabara ya rami mpaka tumemweka kijana wetu ,viva pinda kwa uadilifu, kuwa rahisi uimalizie toka mpanda mpaka kigoma na ile ya tabora

sawa kabisa atakua rahisi na si Rais
 
Watu wengine sielewi walichaguliwa vipi kushika nyadhifa kubwa namna hii afu haohao wanataka zaidi.Siku moja tutakuja ongozwa na matahira.
 
pinda amewahi kufanya uamuzi gani akiwa waziri mkuu mapaka ameacha uwaziri mkuu? maana sijui kama anaendelea kuwa waziri mkuu mi hata simsikii akifanya jambo lolote la kimaamuzi zaid ya kulalamika na kulia mambo yakimzidia. huyu ni waziri mkuu wa hovyo hovyo sana. hivi ameachana na yule bint aliyemaliza education udsm mwaka 2008 akampeleka dodoma afanye kazi huko awe karibu yake? pinda awe rais? jaman hii nchi mmeichoka kias hiki?
 
Mizengo Kayanza Peter Pinda-Haiba yake,UADILIFU wake,unawatisha MANYANG'AU na wasaka tonge WENGI
Kulingana na sera za CCM zenye lengo la kuiacha nchi ikiwa imechoka, kwa hakika Pinda ni kiongozi bora kuliko wote. Waziri mkuu aliyemshauri Rais akope tuuuuu hadi kufikisha deni la nchi Trioni 40 (bajeti ya miaka miwili ya nchi) huku ilipotumika hiyo hela hapaonekani. Hivi ni kitu gani alichowafanyia watanzania cha kuwezesha japo kuelezea namna ambavyo deni lote hili la nchi limetumika? Ni nani anayeweza kuwaambia watanzania bajeti zinazopitishwa kila mwaka za wizara mbalimbali zinatumikaje hadi huduma zinakosekana?

Katika nchi inayoongozwa na Pinda kama waziri mkuu tunakaa siku tatu bila umeme, halafu huyo huyo anaota ndoto za uRais, na mtu aliyechoka kufikiria kama wewe bado unamuona anafaa kuwa Rais. Kimsingi mimi naweza kusema mtu yeyote ambaye hivi sasa yupo kwenye baraza la mawaziri la Kikwete na ambaye maamuzi ya vikao vya baraza la mawaziri vimepelekea nchi kuwa katika hali mbaya kama ilivyo hivi sasa, hafai hata kwa bure kugombea nafasi ya Urais.

Mtu aliyeshindwa kumshauri vema rais ili afanye maamuzi na kuchukua hatua zenye faida kwa watanzania, anatushawishije leo hii tumwone kwamba atakuwa na uwezo wa kiuongozi akiwa Rais? Uwezo wa mtu unaanzia kwenye ushauri kabla ya yeye mwenyewe kushika nafasi. na kama ukitoa ushauri ukaona unakataliwa, na unaona nchi inaliwa, sharti ujiuzulu ili usiwe sehemu ya matatizo yanayoikabili nchi. Nasema hata akina Membe, Makamba, na ghasia nyingine zote zilizopo madarakani hivi sasa, hazifai kushika nafasi ya Urais.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom