Mizengo Pinda ni Mtu wa Ajabu Sana

Mizengo Pinda ni Mtu wa Ajabu Sana

nadhani hata wewe umemuona #mlevi huyu anavyobwabwaja.

Wana akili fupi watu hawa. Lowasa hawamzungumzii. Wanamsapoti sana kwani wanajua akisimama na Upinzani,itakuwa rahisi sana kuing'oa CCM kwani udhaifu wake (lowasa) uko njenje na ni mchafu.

Pinda anawanyima usingizi watu hawa.

NA BADO!

Yaani huyu ambaye wakati wa utawala wake wa uPM kawaruhusu kuwa wananchi tukiandamana tupigwe ndiyo saa hivi kageuka lulu ya chama cha magamba.

Je, ushafikiria akiwa rais atatoa kauli gani!!!!?

Embu nitajie mambo walau machache yanayoonyesha ufanisi wake katika utendaji wa kila siku wa majukumu yake kama raia wa kawaida au PM!!!!!?
 
Hatufai, tunataka mwenye maamuzi kama Lowasa. Ningesikia Lowasa ndo katangaza nia ningesema afadhali ila all in all MOU imesainiwa CCM hawana chao tena hata aje nani haturudi nyuma. Mambo kama ya NARK Kenya yanakuja.
 
ha ha ha,PM anahamasisha kufuga nyuki tupate asali tujiramberambe
 
Mimi anachonishangaza ni uwa analalamika tu.Sasa nani wa kuchukua hatua!!

Yeye inafaa awe anachukua hatua si kulalamika lalamika tu

ila hata bosi wake analalamika sana nae,maana jana amelalamika kwamba Huko Msoga kuna mkandaras amejenga daraja chini ya kiwango sababu ya rushwa
 
Yaani huyu ambaye wakati wa utawala wake wa uPM kawaruhusu kuwa wananchi tukiandamana tupigwe ndiyo saa hivi kageuka lulu ya chama cha magamba.

Je, ushafikiria akiwa rais atatoa kauli gani!!!!?

Embu nitajie mambo walau machache yanayoonyesha ufanisi wake katika utendaji wa kila siku wa majukumu yake kama raia wa kawaida au PM!!!!!?
Afadhari wewe umeongeza na hili, maana mimi nilikuwa namuangalia kwenye upande wa maisha ya watanzania ya kiuchumi na kijamii. Lakini angalau wewe unasaidia kutukumbusha kwamba hata ule uwezo wa kureason out nini cha kusema kabla hajatamuka ni tatizo. Hawatofautiani sana na bosi wake.
 
Yaani kiongozi kwangu mie ninahisi ni mara 10 tupate rais type ya Pro. JK kuliko kupata rais type ya Pinda maana jamaa anaweza kupelekewa jambo badala ya kutoa maamuzi akaanza kulia pia
 
Ni kwelo ni mtu wa ajabu sana alipoingia madarakani na miwani ya plastic sasa anavaa rimless ya gold kama ya swahiba yake Na keshajua kuvaa pete za gold basi taabu kwisha kabisa! Kauli zimebaki kama lakutokea na litokee na wapigwe tu na kesho mtu anabondwa haswa'! Yale machozi kwa albino hakuna tena! Chezea madaraka wewe?
 
Pinda analalamika wazungu kutunyima pesa eti wamekosea kwa sbb walioiba hela niwachache haikupaswa kuwaadhibu mpaka watu wa vijijini,eti waadhibiwe waliofanya.Binafsi namshangaa kwa sbb mafisadi hawajaanza leo wametamalaki tangu enzi za Mkapa,nayeye mwenyewe niwalewale na haijawahi kutokea serikali hii ikachukua hatua.Sijui tumueleweje? Anadhani wazungu nimazuzu kama Watanzania?,waendelee kutoa huku walengwa haziwafikii?.Mimi nawaunga mkono Wazungu watunyime tu labda tutapata akiri hasa huko vijijini,Dar Tabora na Dodoma alikosema pinda kwa sbb ndio wanaoichagua Ccm
 
mimi nafikiri mleta mada amekurupuka nafikiri hapa alikuwa anamzungumzia Edward Fisadi Lowassa.Watanzania wa leo wanajua mbivu na mbichi kutumika kwenu kumchafua na kumsemea maneno ya uongo Mtoto wa Mkulima Mizengo Pinda hakutafanikiwa ni kiongozi safi mwenye uzoefu mkubwa wa mambo ya kitaifa na kimataifa,muadilifu,mchapakazi hodari anayejali maisha ya watanzania wote,mchukia rushwa,mpenda maendeleoleo tumeshuhudia upatikanaji wa mbolea ya kutosha ya ruzuku kwa wakulima,uzalishaji kwenye kilimo umepanda kwa takribani asilimia 80% haijawahi tokea toka tumepata uhuru 1961,tumeshuhudiakuanzishwa kwa mfumo wa stakabadhi gharani ambapo imewawezesha wakulima kuzalisha na kuuza mazao yao kwa urahisi,tumeshuhudia ujenzi wa barabara na miundombinu iliyo imara kwa kasi kikubwa haijawahi tokea toka tupate uhuru,ujenzi wa mashule ,vyuo na mahospitali kwa kasi kubwa,tumeshuhudia kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato TRA na Bandari kwa asilimia 69.8% toka mwaka 2008 baada ya Mizengo Pinda kuwa waziri mkuu hii imetokana na nidhamu na udhibiti kwa kiasi kikubwa rushwa inayosimamiwa na utawala wake kama mtendaji mkuu wa serikali,tumeshuhudia kutembelewa na viongozi wakuu wa nchi kubwa kiuchumi na ushawishi duniani Marekani na China hii yote ni kwa sababu wanaridhishwa na utawala wa serikali yaawamu ya nne inayoongozwa na Dr J kikwete akisaidiwa na Mizengo PINDA takwimu zinaonyesha wazi mambo mengi mazuri yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika kwenye serikali ya awamu ya nne Mizengo Pinda akiwa waziri mkuu wewe unabeza acha kuleta siasa kwenye mambo ya ukweli yanayoonekana machoni mwa watanzania najua unatumiwa na Mafisadi ili kuminya harakati za kuleta uadilifu kwa watendaji wa serikali na kuleta maendeleo kwa watanzania katika shughuli za kiuchumi na kijamii.Watanzania wanataka kiongozi ajaye awe mca mungu yani awe na hofu ya mungu katika utendaji wake,muadilifu asiyekuwa na harufu ya rushwa,mzoefu kwenye mambo ya serikali ,mwenye uelewa mpana kwenye mambo ya uchumi,kijamii,kiutamaduni na kimichezo ili kuweza kukuza na kuendeleza sekta zote zinazochochea kukua kwa uchumi,kiongozi mwenye hekima na busara katika maamuzi yake kwa maendeleo ya taifa wala si kwa manufaa yake na familia yake.Sifa hizo zote zinazangukia kwa Mizengo Kayanza Peter Pinda ndiyo maana mafisadi na vibaraka wao hawapati usingizi wakisikia Mizengo Pinda.Ewe mtanzania makini mwenye nia njema na tanzania kokote ulipo waelimishe watanzania waliokuzunguka tumpende ,tumtetee na kumsemea ukweli Pinda kwani kuna kundi la watu wachache wenye uchu wa madaraka,mafisadi na wasioitakia mema tanzania na rasirimali zake wanamuhujumu kwa imani kwamba akiwa rais hawatofanikiwa kuinyonya tanzania na ndiyo maana kila kukicha wanamchafua.
 
Mtoto wa mkulima awe huyu? Anajua mateso wanayopata nduguzetu kwa kukosa masoko,pembejeo nakudhurumiwa aridhiyao na wawekezaji mafisadi kwa kisingizio cha utaratibu?
 
Taarifa za Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kutangaza nia ya kugombea Urais mwaka 2015 iliwashitua wengi sana hasa wakulima ambao hadi hivi sasa hawana mahali pa kuuza mahindi yao huku, Pinda akiwa hana majibu ya matatizo haya ya wakulima. Mizengo Pinda ambaye amekuwa waziri mkuu wa Tanzania kwa miaka ipatayo saba sasa, akiwa ameshindwa kabisa kuongoza nchi anatafuta Urais?

Waziri mkuu Pinda ambaye ndiye mtendaji mkuu wa nchi anatambua wazi kwamba chini ya utawala wake nchi imepitia misukosuko mingi ikiwamo ya migogoro ya kidini, ugaidi, kuongezeka kwa kiwango cha umasikini wa kaya, kuongezeka kwa idadi ya watoto wa mitaani, kuongezeka kwa idadi ya mambumbu, huku hali ya miundombinu ya nchi ikiwa mbaya kupindukia. Nchi hivi sasa inashuhudia ukosefu mkubwa wa maji vijijini na mijini, huku kitendawili cha umeme wa uhakika kikiwa kimekosa mteguaji. Tatizo la foleni za barabarani likionekana kama ni fahari machoni pa watawala hawa waliozoea kupitishwa barabarani kwa ving'ola.

Ni katika utawala huu wa Pinda na Kikwete nchi imejikuta ikiwa kwenye lindi kubwa la madeni ya nje na ndani. Huku deni la nje likikua kwa kasi ya kutisha, deni la ndani sasa linatishia hata mstakabali wa maisha ya watanzania. Kimefikia kiwango cha watanzania kuanza kukosa dawa mahospitalini kutokana na nchi kushindwa kulipa madeni yake. Wakandarasi wanalalamikia kutokulipwa pesa zao baada ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya serikali. wasambazaji wa vyakula mashuleni wapo mbioni kugoma huku baadhi ya vyuo vya elimu ya juu na diploma vikifungwa kutokana na kushindwa kulipa bili za maji na umeme.

Hali ya nchi kiujumla inakatisha tamaa. Huyu Pinda ambaye ameshindwa kutumia nafasi yake kutatua au hata kupunguza ugumu huu wa maisha ya watanzania, akiwawaacha wakulima wakiwa na hali mbaya kiasi cha vijana wengi kutokutamani kukaa vijijini, anaota kuwa Rais? Hii ni ajabu sana, na kwa hakika namuona Pinda kuwa ni mtu wa ajabu sana. Sikutarajia mtu aliyeshindwa kuongoza nchi katika nafasi ya uwaziri mkuu, aweze kufikiria kuongoza nchi katika nafasi ya u-Rais. Ni vizuri Pinda akajiengua katika kinyang'anyilo hiki kuliko kujidhalilisha kutafuta madaraka asiyokuwa na uwezo nayo.

Bila shaka wewe ni kibaraka wa Mafisadi unatumiwa kuminya harakati za uadilifu na nidhamu za kiutendaji tanzania mnajua wazi Mizengo Pinda akiwa raisi hamtofanikisha ndoto zenu za kujinufaisha nyinyi wenyewe,familia zenu na marafiki zenu.Watanzania wa leo sio wa jana wanajua chungu na tamu ukitaka chungu chagua Mafisadi wakiongozwa na Edward Lowassa na ukitaka tamu chagua Waadilifu.PINDA ndiyo mpango mzima tumeelimika na kamwe hatudanganyiki katika hilo.
 
Hatufai, tunataka mwenye maamuzi kama Lowasa. Ningesikia Lowasa ndo katangaza nia ningesema afadhali ila all in all MOU imesainiwa CCM hawana chao tena hata aje nani haturudi nyuma. Mambo kama ya NARK Kenya yanakuja.

Hatumtaki Edward Lowassa ni mchafu hawezi kusafishika kwa namna yoyote ametawaliwa na rushwa si muadilifu tukimpa nafasi ya kuongoza JMT atafilisi rasirimali zote na kuliacha taifa likiwa masikini.Tunataka kiongozi mwaminifu ,mwenye nidhamu na uadilifu katika utendaji wake sifa hizo Edward Lowassa hana hivyo hastahili kuongoza JMT.
 
Pinda analalamika wazungu kutunyima pesa eti wamekosea kwa sbb walioiba hela niwachache haikupaswa kuwaadhibu mpaka watu wa vijijini,eti waadhibiwe waliofanya.Binafsi namshangaa kwa sbb mafisadi hawajaanza leo wametamalaki tangu enzi za Mkapa,nayeye mwenyewe niwalewale na haijawahi kutokea serikali hii ikachukua hatua.Sijui tumueleweje? Anadhani wazungu nimazuzu kama Watanzania?,waendelee kutoa huku walengwa haziwafikii?.Mimi nawaunga mkono Wazungu watunyime tu labda tutapata akiri hasa huko vijijini,Dar Tabora na Dodoma alikosema pinda kwa sbb ndio wanaoichagua Ccm

Ni kweli wazungu wana wasiwasi na hii inatokana uzoefu wa uchafu na ufisadi uliofanywa na Edward Lowasa akiwa waziri mkuu kwenye issue ya Richmond,matumizi mabaya ya pesa kwenye halmashauri zetu wakati wa utawala wake na mikataba mingi mibovu iliyoingiwa wakati huyu jamaa akiwa waziri mkuu.hivi karibuni utata huo utaisha baada ya kukamilika kwa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.
 
Mimi anachonishangaza ni uwa analalamika tu.Sasa nani wa kuchukua hatua!!

Yeye inafaa awe anachukua hatua si kulalamika lalamika tu

Unajua kila mamlaka ndani ya serikali ina mipaka yake kiutendaji kwa hilo watu wanaoelewa hawawezi kumlaumu waziri mkuu Mizengo Pinda kwani anafanya kile kilichopo ndani ya mamlaka yake na pale anapoona suala liko nje ya mamlaka yake ushauriana na mamlaka zilizo juu yake kutafutia ufumbuzi.Mnakumbuka suala la Katibu mkuu wizara ya nishati na madini Ndg Jairo lilipatiwa ufumbuzi kwa mtindo huo na huo ndiyo utaratibu mgawanyiko wa madaraka kwa nafasi mbali mbali za kiutawala vinginevyo ni vurugu tupu na itawafanya watendaji kutowajibika kwa kukosa mamlaka kwenye nafasi zao.Hivyo basi kiutendaji Waziri mkuu Mizengo Pinda hana makosa na huwezi kumlaumu kwa hilo yuko makini sana kiutendaji huwa hakurupuki hufanya maamuzi makini yenye hekima kwa wakati sahihi bila kuingilia mamlaka za tawala zilizo juu yake.
 
Hatumtaki Edward Lowassa ni mchafu hawezi kusafishika kwa namna yoyote ametawaliwa na rushwa si muadilifu tukimpa nafasi ya kuongoza JMT atafilisi rasirimali zote na kuliacha taifa likiwa masikini.Tunataka kiongozi mwaminifu ,mwenye nidhamu na uadilifu katika utendaji wake sifa hizo Edward Lowassa hana hivyo hastahili kuongoza JMT.
Noted mkuu mimi nilikuwa na compare na huyo wanayemsema kwenye uzi. Lakini tunahitaji kiongozi mwenye sifa zote ulizozitaja na maamuzi sahihi.
 
Mimi anachonishangaza ni uwa analalamika tu.Sasa nani wa kuchukua hatua!!

Yeye inafaa awe anachukua hatua si kulalamika lalamika tu

Sio kulalamika tu mpaka analia na machozi yanatoka (kama mtu mzima unalia mbele ya mgonjwa au mtu mwenye matatizo si ndio utasababisha kumfanya anyong'onyee)
 
nadhani hata wewe umemuona #mlevi huyu anavyobwabwaja.

Wana akili fupi watu hawa. Lowasa hawamzungumzii. Wanamsapoti sana kwani wanajua akisimama na Upinzani,itakuwa rahisi sana kuing'oa CCM kwani udhaifu wake (lowasa) uko njenje na ni mchafu.

Pinda anawanyima usingizi watu hawa.

NA BADO!

Safi sana mkuu umewaambia ukweli wanamuonea wivu mtoto wa mkulima hawajuhi kama tabia yake na matendo yake imetokana na malezi bora aliyopata kwa wazazi wake,walimu wake shule alizosoma na viongozi waliomlea kikazi akiwa serikalini huyu jamaani muajibikaji na muadilifu by nature yani ndivyo alivyo tofauti na viongozi wengine wanaojionyesha mbele za watu wao ni wasafi kumbe ni mafisadi wa kutupwa wanajulikana hivyo toka enzi za Mwl.Nyerere.Kinachombeba Mizengo Pinda ni hekima,busara,uzoefu mkubwa na uadilifu alionao yani hakuna kama yeye ndiyo maana Mafisadi hawapati usingizi afya zao zinazidi kudhoofika kwa mawazo na presha walizo nazo.
 
Wazazi wa Mizengo nimepata kuwatembelea. Baba yake alikuwa CATEKISTA pale kibaoni(kijijini kwao). alistaafu mwishoni mwa miaka ya 90.

Yaani ni bedui hakuna mfano. na ndio maana hakuna hata mtoto wake hata mmoja amepotea njia. Woote wanaishi ktk maadili safi. hata wale ambao hawakuendelea na elimu zaid,wanaheshima kubwa sana ktk jamii zao.

Kuna mdogo wake pia ni yupo kwenye Jopo la ulinzi la Rais ktk shughuli za ndani na nje.

KIUFUPI; Pinda #amepikwa vilivyo. anatufaa.
 
Back
Top Bottom