Mizengo Pinda: Mawaziri wazembe kufukuzwa kazi

Kama anachokisema kina ukweli basi angeanza na Waziri Kawambwa na waziri Mulugo ili japo tuanze kurudisha imani kwake.
 
Pinda anza wewe kujifukuza kwa sababu kazi umeshindwa upo upo tu wakati wanaotafuna pesa za walipa kodi unawafahamu. Hivi unafikiri kuwa waziri mkuu ni kumtetea mwizi?
 
Mwongo tu huyo, hana lolote. Mtu hawezi hata kumfukuzwa kazi mwalimu wa shule ya msingi, ataweza kumfukuza waziri? Mmeshawafanya watanzania kama misukule, endeleeni na upuuzi wenu but remember there is a day.
Hapo umenena mkuu..
Mtu mwenyewe analia lia ovyo.. atawezaje..!
 
Huna jeuri hiyo mtoto wa mkulima. Katibu mkuu wa wizara ya nishati alikushinda sembeuse waziri! Ni vizuri kukaa kimya kama huna cha kusema. Mliwapeleka hao jamaa kula kodi ya wananchi, with zeo delivery.
mkuu umenena,yeye mwenyewe sio mwajibikaji.sekondari zilijengwa na lowasa zimeishia pale pale hazijaendelezwa mpaka leo
 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema kuanzia sasa mawaziri watakaoshindwa kufikia viwango vya uwajibikaji watafukuzwa kazi. Mbali na hayo amewataka waandishi wa habari kutembelea wizara kila baada ya miezi mitatu kuwauliza mawaziri wamefanya nini katika kipindi hicho.

Alikuwa akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya mfumo madhubuti wa utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya programu na miradi ya maendeleo, Dar es Salaam jana.

Pinda alisema utaratibu huo unalenga kupima uwezo wa utendaji wa kila waziri na watendaji wengine serikalini.

Mafunzo hayo yaliyochukua siku 42 yaliwahusisha watendaji wa wizara mbalimbali, sekta binafsi na wadau wengine kutoka vyuo vikuu, huku wakufunzi wakuu wa mpango huo wakiwa ni wataalamu kutoka Malaysia.

Pinda alisema kwa mujibu wa utaratibu huo, Rais atapata fursa ya kupima uwezo wa kila waziri na kumweleza juu ya utendaji wake na kama ameshindwa kufikia vigezo atamfukuza kazi.

Alisema kupitia mpango huo pia kutakuwa na chombo cha taifa cha kufuatilia mipango ya serikali na kila wizara na halmashauri zitakuwa na kitengo maalumu cha kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mipango hiyo.

“Mfumo huu unalenga kuharakisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kuleta matokeo yanayotarajiwa kwa kujumuisha uchambuzi wa kina wa maabara ,” alisema.

Naye Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa mafunzo hayo, Balozi Ombeni Sefue, alisema katika eneo la nishati, uchambuzi wa kina umelenga katika kuzalisha megawati 2,780 za umeme ifikapo mwaka 2015 kuhakikisha raslimali za mafuta na gesi zinatumika kwa manufaa ya nchi na watu wake.
miaka yote alikuwa wapi?
 
Hivi mtu anahitaji kuwa na elimu fulani kuelewa udhaifu wa hawa watu (mawaziri pamoja na WM)! Ebu tujiulize haya machache:
1. ebu tuseme kama asingekuwepo WM Mizengo tungepoteza nini?
JIBU: Tusingepoteza chochote na badala yake tungeambulia chochote. Jiulize hivi kweli inaingia kichwani WM hata kushindwa kukemea uchafu amabao ni bayana kabisa. Hii umeona wapi!

2. hivi viongozi wa ccm na kama wapo wachache ni kweli na elimu yao pamoja na UZALENDO WAO wanakubali kuziba masikio yao na kukubali kusikia huu udhaifu! Hii tuite ni unafik!!!

3. Nani asiyejua maneno na vitendo vya hayati marehemu Sokoine! Anasema leo na kuagiza na baada ya siku saba au week anakwenda kuangalia UTEKELEZAJI WAKE! hOTUBA ZAKE hardly 30 minutes, Sasa kipimo cha huyu WM pamoja na wenzake kitoke wapi! Sitegemei hata kama kuna haja ya kuweka kumbukumbu ya watu kama hawa kwani historia haiwahitaji kabisa!

Namalizia kwa kusema '' kiongozi yeyote ambaye anakubaliana na performance ya serikali ya CCM basi ni mnafiki!
 
Tanzania haijapata kuwa na waziri Mkuu kichekesho kama siyo soft like snow. Waziri mkuu gani kila mara yeye ni kulalamika na kulia tu.

Tanzania hatukupata kuwa na Waziri Mkuu soft kama huyu Mizengo Pinda. Mtoto gani wa mkulima hata hafahamu kulitumia jembe la madaraka yake.

Tanzania kwa sasa inahitaji Waziri Mkuu mkali na mchapa kazi. Hatuhitaji viongozi wanaofumba macho when the going gets TOUGH. Tunahitaji Waziri Mkuu ambaye when the going gets tough, the tough get going.

Honestly, Huyu jamaa ni bogus.
 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema kuanzia sasa mawaziri watakaoshindwa kufikia viwango vya uwajibikaji watafukuzwa kazi. Mbali na hayo amewataka waandishi wa habari kutembelea wizara kila baada ya miezi mitatu kuwauliza mawaziri wamefanya nini katika kipindi hicho.

Alikuwa akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya mfumo madhubuti wa utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya programu na miradi ya maendeleo, Dar es Salaam jana.

Pinda alisema utaratibu huo unalenga kupima uwezo wa utendaji wa kila waziri na watendaji wengine serikalini.

Mafunzo hayo yaliyochukua siku 42 yaliwahusisha watendaji wa wizara mbalimbali, sekta binafsi na wadau wengine kutoka vyuo vikuu, huku wakufunzi wakuu wa mpango huo wakiwa ni wataalamu kutoka Malaysia.

Pinda alisema kwa mujibu wa utaratibu huo, Rais atapata fursa ya kupima uwezo wa kila waziri na kumweleza juu ya utendaji wake na kama ameshindwa kufikia vigezo atamfukuza kazi.

Alisema kupitia mpango huo pia kutakuwa na chombo cha taifa cha kufuatilia mipango ya serikali na kila wizara na halmashauri zitakuwa na kitengo maalumu cha kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mipango hiyo.

“Mfumo huu unalenga kuharakisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kuleta matokeo yanayotarajiwa kwa kujumuisha uchambuzi wa kina wa maabara ,” alisema.

Naye Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa mafunzo hayo, Balozi Ombeni Sefue, alisema katika eneo la nishati, uchambuzi wa kina umelenga katika kuzalisha megawati 2,780 za umeme ifikapo mwaka 2015 kuhakikisha raslimali za mafuta na gesi zinatumika kwa manufaa ya nchi na watu wake.

Yeye mwenyewe ni mzembe wa wazembe. Hilo ghorofa lililodondoka ilitakiwa yeye ndie awe mhusika mkuu. Ile ripoti ya jengo jingine lililoporomoka aliyokabidhiwa akachukua yale makaratasi na kwendakuanikia ulezi huko kwao angefuata mapendekezo yake hawa watu 36 wasingepoteza maisha!!
 
Je rais na Waziri mkuu wazembe watafanywa nini? Mi naona tufanye kama China wapigwe risasi hadharani.
 
useless ....
IMAGINE ETI WAANDISHI WA HABARI NDIO WA KUWAULIZA MASWALI MAWAZIRI....

... yy ndio wa kwanza KUFUKUZWA.... SI MTENDAJI AT ALL.....
 
Mawaziri wazembe? Uzembe gani huo anaozungumzia? watoto wa form IV wamefeli vibaya, jingo limeanguka na kuua, lakini mawaziri husika bado wanapeta. Kweli "mwacheni mfu amzike wenzie"
 
Wakati mwingine inabidi tu mtu ucheke maana hawa viongozi wetu hawajielewi.
 
...duh kweli nyani hauni kundule, yaani Pinda ndiye wakuwatishia Mawaziri wazembe wakati yeye ni mzembe kuliko wengi wa walio kwenye Baraza la Mawaziri?hiki sasa kichekesho...
Kweli kabisa NYANI HAONI KUNDULE. Mtu mwenyewe Pindaaa!!! Siamini kama kweli ndiye aliyetoa hayo maneno. Kabla ya kuwaangalia wenzie kama wanafaa, ajiangalie yeye kwanza na achukue hatua mara moja ya kubwaga manyanga. In fact, katika historia ya nchi hii hakuna prime minister aliyepinda na kupwaya kama "mtoto wa mkulima".
 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema kuanzia sasa mawaziri watakaoshindwa kufikia viwango vya uwajibikaji watafukuzwa kazi. Mbali na hayo amewataka waandishi wa habari kutembelea wizara kila baada ya miezi mitatu kuwauliza mawaziri wamefanya nini katika kipindi hicho.

Alikuwa akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya mfumo madhubuti wa utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya programu na miradi ya maendeleo, Dar es Salaam jana.

Pinda alisema utaratibu huo unalenga kupima uwezo wa utendaji wa kila waziri na watendaji wengine serikalini.

Mafunzo hayo yaliyochukua siku 42 yaliwahusisha watendaji wa wizara mbalimbali, sekta binafsi na wadau wengine kutoka vyuo vikuu, huku wakufunzi wakuu wa mpango huo wakiwa ni wataalamu kutoka Malaysia.

Pinda alisema kwa mujibu wa utaratibu huo, Rais atapata fursa ya kupima uwezo wa kila waziri na kumweleza juu ya utendaji wake na kama ameshindwa kufikia vigezo atamfukuza kazi.

Alisema kupitia mpango huo pia kutakuwa na chombo cha taifa cha kufuatilia mipango ya serikali na kila wizara na halmashauri zitakuwa na kitengo maalumu cha kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mipango hiyo.

“Mfumo huu unalenga kuharakisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kuleta matokeo yanayotarajiwa kwa kujumuisha uchambuzi wa kina wa maabara ,” alisema.

Naye Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa mafunzo hayo, Balozi Ombeni Sefue, alisema katika eneo la nishati, uchambuzi wa kina umelenga katika kuzalisha megawati 2,780 za umeme ifikapo mwaka 2015 kuhakikisha raslimali za mafuta na gesi zinatumika kwa manufaa ya nchi na watu wake.

Nafikiri alikuwa anaota kwenye harusi ya Mangula. Si huyu huyu alishindwa kumfukuza Jairo na kusema hana mamlaka kwani sio yeye aliye mteua?? Hayo mamlaka kayapewa lini hadi kutujia na ndoto za mchana?

Naamini alikuwa anafurahisha GENGE. Vinginevyo atakuwa anafikiri ni tarehe 1/4 kitu ambacho ilishapita.
 
Back
Top Bottom