Hapo umenena mkuu..Mwongo tu huyo, hana lolote. Mtu hawezi hata kumfukuzwa kazi mwalimu wa shule ya msingi, ataweza kumfukuza waziri? Mmeshawafanya watanzania kama misukule, endeleeni na upuuzi wenu but remember there is a day.
mkuu umenena,yeye mwenyewe sio mwajibikaji.sekondari zilijengwa na lowasa zimeishia pale pale hazijaendelezwa mpaka leoHuna jeuri hiyo mtoto wa mkulima. Katibu mkuu wa wizara ya nishati alikushinda sembeuse waziri! Ni vizuri kukaa kimya kama huna cha kusema. Mliwapeleka hao jamaa kula kodi ya wananchi, with zeo delivery.
miaka yote alikuwa wapi?WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema kuanzia sasa mawaziri watakaoshindwa kufikia viwango vya uwajibikaji watafukuzwa kazi. Mbali na hayo amewataka waandishi wa habari kutembelea wizara kila baada ya miezi mitatu kuwauliza mawaziri wamefanya nini katika kipindi hicho.
Alikuwa akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya mfumo madhubuti wa utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya programu na miradi ya maendeleo, Dar es Salaam jana.
Pinda alisema utaratibu huo unalenga kupima uwezo wa utendaji wa kila waziri na watendaji wengine serikalini.
Mafunzo hayo yaliyochukua siku 42 yaliwahusisha watendaji wa wizara mbalimbali, sekta binafsi na wadau wengine kutoka vyuo vikuu, huku wakufunzi wakuu wa mpango huo wakiwa ni wataalamu kutoka Malaysia.
Pinda alisema kwa mujibu wa utaratibu huo, Rais atapata fursa ya kupima uwezo wa kila waziri na kumweleza juu ya utendaji wake na kama ameshindwa kufikia vigezo atamfukuza kazi.
Alisema kupitia mpango huo pia kutakuwa na chombo cha taifa cha kufuatilia mipango ya serikali na kila wizara na halmashauri zitakuwa na kitengo maalumu cha kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mipango hiyo.
Mfumo huu unalenga kuharakisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kuleta matokeo yanayotarajiwa kwa kujumuisha uchambuzi wa kina wa maabara , alisema.
Naye Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa mafunzo hayo, Balozi Ombeni Sefue, alisema katika eneo la nishati, uchambuzi wa kina umelenga katika kuzalisha megawati 2,780 za umeme ifikapo mwaka 2015 kuhakikisha raslimali za mafuta na gesi zinatumika kwa manufaa ya nchi na watu wake.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema kuanzia sasa mawaziri watakaoshindwa kufikia viwango vya uwajibikaji watafukuzwa kazi. Mbali na hayo amewataka waandishi wa habari kutembelea wizara kila baada ya miezi mitatu kuwauliza mawaziri wamefanya nini katika kipindi hicho.

Kweli kabisa NYANI HAONI KUNDULE. Mtu mwenyewe Pindaaa!!! Siamini kama kweli ndiye aliyetoa hayo maneno. Kabla ya kuwaangalia wenzie kama wanafaa, ajiangalie yeye kwanza na achukue hatua mara moja ya kubwaga manyanga. In fact, katika historia ya nchi hii hakuna prime minister aliyepinda na kupwaya kama "mtoto wa mkulima"....duh kweli nyani hauni kundule, yaani Pinda ndiye wakuwatishia Mawaziri wazembe wakati yeye ni mzembe kuliko wengi wa walio kwenye Baraza la Mawaziri?hiki sasa kichekesho...