Pelekaroho
JF-Expert Member
- Sep 15, 2010
- 1,602
- 378
Hivi kumbe watu bado kabisa hamjui katiba. Kwani mmesahau kuwa waziri lazima atoke miongoni mwa wabunge? Sasa Lipumba ni mbunge wa wapi? Hili haliwezekani msitupotezee muda.
Hivi kumbe watu bado kabisa hamjui katiba. Kwani mmesahau kuwa waziri lazima atoke miongoni mwa wabunge? Sasa Lipumba ni mbunge wa wapi? Hili haliwezekani msitupotezee muda.
Bado anaweza kuteuliwa na Rais kwa sababu katika inamruhusu bwana mkubwa kuteua wabunge kumi na kwa kumbu kumbu yangu bado hazijaisha... Isipokuwa waziri mkuu mbali ya kuwa mbunge lazima awe mbunge wa Jimbo na siyo wa viti maalum au ubunge wa kuteuliwa... Nawasilisha!
ingawa nimelike comment yako ila nilitaka kujua .....je kuna kipengele kinachosema (ktk katiba) kuwa ni lazima awe kutoka jimboni???
Nauliza
Kabla ya kuchagua hao mawaziri Mkuu wafanyiwe vetting kupata watu waadilifu, huyu Mhe Aggrey Mwanry amefunga fensi kubwa hapa A Town lazima naye ajieleze kapata wapi hizo fedha za kununua maeneo makubwa hivyo katikati ya mji wa Arusha???? Mkulu kama anaipenda Tanzania aweke watu waadilifu ingalao kulinda kile kilichopo na kuleta unafuu wa hali ya kiuchumi kwa Watanzania!!!!Magufuli Pombe John,Mzee wa takwimu, Mwanry Aggrey na makelele yake ya kujihami, na yule nanihii, huyu jamaa yetu huyu..kanitoka jina. hawa nilikuwa napima uwezo wao wa ku-crash wasiojiweza bungeni.
Wana-JF Raia Mwema ninalo Mwandishi anajiita MsomajiRaia@yahoo.com na ndiye aliyeandika kila awamu ina rekodi ya kuua.toleo no. 232 la 28/3/2012 na Mhariri Mkuu kukanusha kwa maandishi madogo ukurasa wa mbele toleo no.235 mauaji yake mtoa thread kaacha maneno makusudi yasemayo Natamani hizi ziwe ni tetesi za kweli km zilivtto zingine
Kwa ufupi simsemei Pinda ila nuu uchochezi naq huenda Gazeti nalo llikakanusha tena
... endapo Prof Lipumba atakubali kujiunga na hili li baraza la mawaziri uozo la CCM hakika nitamdharau milele na kutilia wasiwasi utashi wake na kazi ya usomi wake pia!!!!!!!!
Acheni CCM kimalizie uchafu wake wote kama walivyouanza mara baada ya Mwalimu Nyerere kufa ili hukumu ya walalahoi kwa chama hiki hivi karibuni isije ikasambaa hata kwa vyama ambavyo havihusiki na uhandisi wa UFISADI wote wanaolifanyia taifa hili.
Naomba ufafanuzi wa neno UHANDISI