Hii ni sababu moja tosha kati ya nyingine 1000 ya kuwanyima kura...ni lini watajua matatizo ya muhimbili kama wenyewe hawatibiwi hapo au wanafunzi kukaa chini kama watoo wao hawasomi kwenye hizo shule..lakini kwasababu atutumii kura yetu vizuri wacha waendelee kula bataTumesikia kwamba mh. Pinda -Waziri mkuu wa Tz,kaondoka leo kwenda kutibiwa UK kwa wiki moja.
Nadhani ziara ndefu na wingi wa kazi umemchosha sana,kwani hata mwendo miguu inaonekana sio sahihi kabisa,kwani asitibiwe Muhimbili tu.Wanadai kaenda na mkewe tu,kitu ambacho sio rahisi laziza wasaidizi wawepo.Anyway tunamtakia matibabu mazuri waziri mkuu wetu.
Afadhali mtoto wa mkulima kaenda kutibiwa! Mzee wa 'vijisenti' huwa anapeleka suti zake majuu kufuliwa!
....kwa waziri mkuu that is a normal health check up ambayo hufanyika once a year.......
....sijui kwanini viongozi wa kiafrika hawaamini madaktari wa nyumbani....sijui wanagopa siri zao kuvuja..[simnajuwa wakienda ulaya wanaonekana watu wa kawaida na hakuna daktari anayekuwa interested ku share findings na mwenzake].....but pamoja na viapo ukweni nyumbani naona watu wengi hawapendi kufanyiwa vipimo sensitive hospitali za jirani na wanapoishi.....kuna watu wanatoka dar wanaenda hadi kcmc ...na wa moshi wanakuja muhimbili just for the sake of privacy!!!
ulaya na hata afrika nchi kama south africa ,egypt etc marais wanatibiwa Millitary hospital...hapa kwetu wamejitahidi kuboresha Lugalo na e.mzena kwa kiwango kikubwa sana kiasi hata presidaa anaweza kutibiwa maradhi ya kawaida pale lakini ...no body goes!!...bora hizo pesa wangeboresha mikoani huko!...yaani imefikia mahali huduma pekee ambayo viongozi wetu wanaona fahari kuipata kwenye Millitary hospital yetu ni ile Ya Mortuary...ili apigiwe saluti za mwisho mwisho...hata afie wapi ...watampeleka mortuary ya jeshi lugalo....tungependa wahudumiwe pale wakiwa wazima na si wafu!!
Wasu,Nafikiri mkuu si kweli
1.Anapokuja mgonjwa kutoka africa ambaye hana bima ya nchi husika madaktari wanamchangamkia vilivyo, maana hospitali inapata fedha za kutosha kutoka kwa mtu husika.
2.Nafikiri viongozi wanawakimbia madaktari wetu kutokana na hofu ya kwamba wanaweza kuwa manipulated na wabaya wao na kuwa - theorodani, nafikiri hiki ndicho wanakiogopa zaidi.
3. Viongozi wetu wote wana amini ktk ushirikina.
Hawa jamaa nafikiri hawakimbii hospitali zetu kwa sababu hawaamini ma daktari, nafikiri wanachoogopa zaidi ni matatizo ya imani zetu za jadi kama vile kukolimba nk.
Kwa mtizamo wangu kwa kiongozi wa ngazi yake kwenda kutibiwa ughaibuni inaweza kuwa si hoja sana,maana wana stahiki za aina hiyo.Tatizo langu ni kwa nini waende mbali kote huko wakati hata Afrika ya Kusini wana matibabu ya kisasa kama wanayoyafuata huko na gharama zinaweza kuwa nafuu.Hivyo inaelekea gharama kwao si jambo la msingi sana kuzingatia
Huko UK si ajabu akajikuta anatibiwa na daktari mbongo/mtz aliyekimbia maisha magumu tz...hahaha, hapa kwetu hamna hospitali za kuwatibu hawa?, na je, kama wao wanaenda UK sisi tuliowapa kibarua/kura tuende wapi?, iyo ni sawa na baba anachinja jogoo anakula peke yake watoto wanakula mchicha....aibuuuu kwa viogonzi wetu. kwa stail hiyo hawatakuwa hata na mwamko au uchungu kuboresha hospitali zetu au hata kuboresha mishahara ya madaktari wetu ili wasikimbie nchi.