Mizengo Kayanza Peter Pinda

Mizengo Kayanza Peter Pinda

Mnasahau kwamba anapata 80% ya mshahara wa Majaliwa, walinzi na gari la serikali!!!
 
Anawasiwasi gani,Huku kaasali,kule kang'ombe,pole ka zabibu,huko kashamba ka mbiga na vimahindi vya kuchoma kuongeza joto mwilini.Ukweli napenda maisha yake niyakawaida saana,hanatofauti na wengine waishio vijjjni-kasoro yeye alikua kiongozi tu.
Wacha unafiki, usiseme unapenda maisha yake, hata yeye anajuta angejua angechukua chake mapema na kustaafu darisalama unakunywa juice ya ukwaju kwenye kiyoyozi na kaofisi kauongo na kweli katikati ya jiji , we unafikiri watoto wake wanafagilia huu ujinga? Angalia watoto wa Julius walivyo hohe hahe na wakati baba yao alikuwa mtu mkubwa sana. Ukipata nafasi kubwa weka mipango kwaajili ya kesho, mambo ya shamba sawa ila weka wafanyakazi kila mwisho wa wiki unakamata pipa kwenda kijijini kuangalia mashamba na mifugo, wewe angalia jinsi jamaa alivyochakaa huko kijijini kisha unamsifia.
 
kapiga pesa kazitupa mashambani huwez kumyooshea kidole cha wizi akili kichwani.
 
Ukitaka kujua wabongo ni wanafiki wazandiki wakubwa angalia huu uzi akiwa waziri mkuu alikejeriwa mwanzo mwisho leo hii eti mzee ana busara kwa hiyo busara zimekuja baada ya kusitaafu siasa?
 
Huyu mzee pamoja na mapungufu yake namkubli sana,anaishi maisha anayotaka mwenyewe,yani hana madoido kabisa.
Naikubali sana style ya maisha yake.
a725c7264aa304fa0166719d086ca290.jpg

8211e276225415f0ed11de102fbc21c4.jpg
alikuwa na mapungufu yake.. ila mazuri yake yalipita mapungufu. mizani imeegemea kwenye uzuri..
anaishi maisha ya KITANZANIA..namwombea dua njema..
 
Back
Top Bottom