Mizani kerooo kwa abiria wa mabasi makubwa

mwanamapinduko

Senior Member
Jan 24, 2011
178
41
Utafiti niliofanya kwa muda wa mwezi, nimebaini kuwa mabasi yanayosafiri safari ndefu, hayapewi kipaumbele kwenye MIZANI. Hivyo hupoteza muda mwingi, na matokeo yake baada ya hapo huenda mwendo kasi kufidia. Kwa kuwa abiria waliboreka na utaratibu huo mbaya kwenye mizani huwaacha madereva waende kama wanavyotaka bila kuwakemea au kutoa taarifa kwa trafiki kwenye cheki pointi!
 
Hizo barabara za kwenda mikoani ni barabara za kuunganisha vijiji lakini sisi tunazigeuza zinakuwa za mkoa hadi mkoa. DSM - Morogoro bara bara ni nyembamba! kwenye mizani watu wanakaa hadi masaa 3 na mizani mingi unategemea kuna uzalishaji hapo wa kukuza uchumi? Mizaha imejaa sana kila sehemu. Kwenye mizani utakutana na watu aina ya akina Jairo, they are always above the law.Solution hapo ni kupanua barabara, na kuweka mizani zaidi ya 3 kwa kila upande ili kusave muda. Mambo kama hayo ukiyajumlisha kwa mwaka utakuta tunapoteza fedha nyingi kwa kuupoteza muda kwenye inshu zisizo na ulazima wowote.
 
kweli hii mizani ni kero kubwa sana hasa kwa mabasi na adha sana , manufaa yenyewe hatuyaoni, hii ingebaki kwa ajili ya magari makubwa tu hasa maloli
 
lol kwa sisi wa njia ya moshi inatukera saaaaaa eti mkifika kwenye mizani
mwaambiwa msogee mbele ama mchuchumae
na wkt mwingine mnavushwa na taxi gari mwalikuta
mbele labda ni janja kati ya mizanisti
na madereva ila hako katabia
i really hate it
ila kuna baadhi ya mabasi
hasa mangorika
chatco
sijui osaka na mengine meng
kilimanjaro
dar exp
metro
sijaona hii kitu
 
mizani ya mabasi iwepo ubungo na itungwe sheria abiriia akikutwa kasimama alipe faini sawa na ya bus owner
 
Hivi logic ya kuwa na mizani kila mkoa ni nini mi siajaelewa utakuta gari la masafa marefu tuseme kutoka songea to Dar haipakii njiani lakini inaingia kila mzani hiyo ni nini hasa au ndo calibration ya mizani yao hawaiamini eeeh!!!!! mnaojua nipe ufafanuzi wa hilo maana inanikera mnoo hiyo hali.
 
Ndugu yangu hiyo imeshakuwa kero lakini ndo serikali yetu mbovu. Wiki iliyopita nikiwa natokea dar kwenda kanda ya ziwa ndani ya basi la mohamed trans, tulifika mzani mmoja baada ya mji wa singida tukakuta mzani unamatatizo, badala ya kukagua listi za muzani walikopimia kabla ya pale na kuruhusu gari kuwa itapima katika mzani unaofuata kwasababu ipo sehemu nyingine maderva wakaambiwa mzani mbovu alafu bosi wa kituo hayupo inamaana mpaki mumsubiri. Abiria walilahumu na baada ya dk 25 bila kuonekana bosi dereva aliondoa gari. Kitendo hicho kikanionesha kuwa watu wakishaona kiongozi wa juu anafanya vyake hata wao kila mtu anatoa maamuzi, huu ni ushenzi kwa wengine.
 
Back
Top Bottom