Miundombinu ya Dar ikiwa hivi, foleni kwisha habari yake!!

Bill of Quantity

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
1,233
405
Wasalaam jf, hebu cheki hii kitu ya china, natamani tungeiga vitu kama hivi..

Yani Dar ikiwa hivi sidhani kama kutakuwa na foleni wala watu kuwahi kazini saa tisa mpaka kumi usiku..

Wasi wasi wangu itakuwa ni ajali.. hehe

Jionee basi

13015260_1048591365213837_3789239573360350214_n.jpg

NYINGINE HII
13062470_1046431745429799_551274101589508554_n.jpg
 
Nikiwa na miaka 5 baada ya kustaafu, na itakuwa kipindi cha Rais wa awamu ya 10 (kama kila raisi atatawala muhula mmoja). Namaanisha hiyo ni Tz ya 2050....
 
Iwe tu hata hivi.......itatusogeza......
 

Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    214.1 KB · Views: 41
Iwe tu hata hivi.......itatusogeza......
Chini ya hayo madaraja watajaa mama lishe, wauza magazeti na wachoma mahindi, jioni wamachinga kama kawa. Kwenye kingo za madaraja yatajaa matangazo ya kampuni za simu na vinywaji.
 
Kwanza kabla ya kuyatamani maendeleo ya taifa kwa ujumla unapaswa wewe ujiulize unachangiaje maendeleo ya taifa lako.....!!??

Maendeleo si mambo ya kufikirika bali ni zao la juhudi maarifa na utendajo kwa bidii bila ya kusahau uzalendo.....
Uzalendo unaanzia kwa mwananchi mmoja mpaka taifa kwa ujumla.....bila ya kusahau viongozi wetu tuliowapa mamlaka ya kutuongoza......

Tutayapata vipi maendeleo ikiwa wananchi hawapendi na wala hawana utamaduni wa kufanya kazi na wale wanaofanya kazi ni kwa kiwango cha chini sana na wengine mpaka wanakutwa wakifanya ngono sehemu za kazi.......

Tutayapata vpi maendeleo ikiwa wale tuliowapa mamlaka ya kutuongoza hawajui hata maana ya uzalendo......

Tutapata vipi maendeleo ikiwa wananchi wengi kama sio wote wanawaza kuiba na kuwa matajiri pasi na kufanya kazi........
 
Back
Top Bottom