Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,331
- 12,952
Pia, ujenzi wa miundombinu ya Mabasi hayo unaendelea kuanzia Mwenge - Tegeta (DAWASA) yenye urefu wa kilometa 15.63 ambapo ujenzi huo unatekelezwa na Wakandarasi wawili M/s China Geo Engineering na M/s Shandog Group Co. Ltd.
“Tunao Wakandarasi wanaojenga barabara ya Mwendokasi kuanzia Serena Hoteli kuelekea Mwenge na kutoka Mwenge kuelekea Ubungo (Daraja ya Kijazi), Wakandarasi wako kazini na fedha ipo”, amesema Bashungwa.
Bashungwa amemtaka Mkandarasi Sinohydro Corporation anayetekeleza ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Tatu (BRT 3) katika barabara ya Tanganyika Motors – DIT, Uhuru (Buguruni – Msimbazi) Bibi Titi na Shaurimoyo (Karume – Bohari), kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati kulingana na mkataba.
Aidha, Waziri Bashungwa amefafanua kuwa TANROADS wapo katika hatua ya manunuzi ya kumpata Mkandarasi atakayejenga Daraja la Mzinga na kufanya upanuzi wa barabara kuanzia Mbagala Rangi Tatu hadi Vikindu ili kupunguza foleni ya magari na kuondoa adha ya watumiaji wa barabara hiyo kwa wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi kuingia Ubia na Sekta Binafsi kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja ya kulipia tozo kama ilivyokuwa katika Daraja la Nyerere Mkoani Dar es Salaam ili fedha hizo zinazopatikana ziweze kutumika katika ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara na madaraja iliyoharibika.