Mitsubishi Pajero iO inanitesa

Kimeo

Member
May 19, 2009
77
11
Jamani nimenunua Mitsubishi Pajero iO ina kama miezi kumi tu, lakini imeanza kusumbua hasa misi zimekua nyingi na wakati mwingine inanizimikia kwenye foleni hapa mjini.

Nimejaribu mara kadhaa kuipeleka gereji mafundi washanilamba mara kibao lakini tatizo lipo palepale, nimebadilisha kwa maelekezo ya mafundi hadi plug (ambazo zote nne ni kama laki moja) mara mbili lakini bado tatizo lipo palepale.

Nishaurini wazee tatizo ni nini nimechoka sasa​
 
Ooh uza hiyo, sisi tulisahuza zamani japo sijui utamwuzia nani. Pole sana
 
mitsubshi Io watu tumezivamia sababu ya sura tuu, lakini kaka hizo sio gari,nilinunua japan, nikaja nayo tz,ikazima one day gari almost mpya nikachoka the following week nikauza, alienunua sio siri alileta ugomvi the way inavyomtesa,well nahisi kwa gari ndogo hapa tz ni TOYOTA hata mechancs wengi ndo wanazifahamu,so baba, tafuta **** mmoja umshikishe!!
 
Mimi nadhani tatizo lipo kwa mafundi. Check electronics, air supply intake etc..
 
Nilikuwa na mpango wa kununua hiyo gari wife anaipigia sana upatu lkn mimi najua Mitsubishi si nzuri sana huku kwetu km zilivyo Toyota sasa kwa mtindo huu nooma tupu siitaki tena
 
Kuna rafiki yangu pia ilikuwa inamsumbua akapeleka Mitsubish kule Pugu Road, walibadilisha plug, petrol filter na air cleaner. Haijamsumbua tena. Nadhani tatizo lake lipo kwenye hivyo vitu vitatu. Gari yake ilipungua pulling power kutokana na matatizo hayo. Hizi gari mpya mafundi wetu wengi hawajazipatia.
 
kama ulibadilisha plug na bado tatizo lipo badilisha waya za plug,kama litakuwepo badilisha air senser,kama bado tatizo lipo inabidi uipeleke kwa dealer kuna kitu kinaitwa crank sensor,usije ukajaribu kubadilisha mtaani bora kwa dealer wao watapima na computer,maana kwa gari hizo crank sensor ndiy inayoomba mafuta. ikishindikana hapo inataka dua au maombi.
 
Plug nne bei yake laki?,hujaibiwa kweli?,lol!!!
Inategemea na Engine imekaaje, nilikuwa na job mbili, sikuwa na wakati kabisa wa ku-service gari yangu. siku nikaamua kwenda Firestone kwa service & tune up. Jamaa wakanambia kubadirisha plugs itakuwa $295.95+ wakati bei ya plug moja ni $1.00 to $5.00.
 
Mtafute fundi Arnold atakufanyia proper diagnostics kwa specialised equipment.Yupo Namanga nyuma ya Best Bite, 0784871657 au website yake http://www.berksautos.co.tz/. Hakuna longo longo, kama gari imekufa atakwambia badala ya guesswork za mafundi wa kubahatisha.
 
huyo anord mbona naona anashughurika na gari zingine.sioni kama mitsubishi zipo katika line yake
 
Pole sana kwa kuteswa na Pajero io, ambazo waswahili wanaziita GDI. Hizi ni gari nzuri sana na za kisasa, mafundi wengi wamezoea kubabaisha ndiyo maana watu wanadhani zina matatizo. Ningekushauri uipeleke Pugu Rd kwa mafundi wa Mitsubishi (Diamond Motors) au mafundi wa Bosch, wataangalia tatizo ni nini halafu watalitatua. Gari nyingi za kisasa (ikiwemo Pajero io) ziko sensitive sana kwa spark plugs na aina ya petrol, kwahiyo unapokuwa na gari hii uwe makini sana ili upate plug zinazofaa, kwasababu tatizo huanza baada ya kuweka plug zisizofaa, hata manufacturer wenyewe wa Mitsubishi wamekuwekea CAUTION kuhusu genuine plug katika cover ya engine.
Mimi ninayo pajero io, ilinisumbua kidogo nilipobadilisha plugs kwa mara ya kwanza, niliweka plug za kawaida ambazo zilikuwa hazichomi vizuri matokeo yake uchafu ukawa unajazana katika system ya air na vacuum sensor, baada ya kubadili plug na kusafisha system gari limerudi kuwa bomba kama mwanzo. Hata bei ya genuine plugs siyo mbaya, zipo NGK, BOSCH, nk.
 
Kuna rafiki yangu pia ilikuwa inamsumbua akapeleka Mitsubish kule Pugu Road, walibadilisha plug, petrol filter na air cleaner. Haijamsumbua tena. Nadhani tatizo lake lipo kwenye hivyo vitu vitatu. Gari yake ilipungua pulling power kutokana na matatizo hayo. Hizi gari mpya mafundi wetu wengi hawajazipatia.


Ni ukweli kabisa Mkulu,

Na hizi gari hazitaki kabisa kuchanganya mafuta,mara leo lita 5 BP kesho mbili GAPCO..,lazima utaiona sio nzuri.unatakiwa uwe na kawaida ya kuweka mafuta sehemu moja tena mengi yasiishe kabisa kwenye tank.
Na kuhusu Plug,ni kweli,yake mmoja ni alfu 25
 
siku zote huwa nawambia watu MMC sio gari kuanzia RVR,Pajero mpaka zile za wajeda zote ziko wapi pickup ila mkubwa jaribu kuirekebisha hiyo gari alafu uiuze
 
Hizi gari zinawasumbua watu wengi sana, mimi nadhani sababu kubwa ni mafundi wa mitaani, na pia watu wengi wamezoea kuweka mafuta ya vigaroni na hizi gari kwa kweli hazihitaji kabisa mafuta machafu ie yaliyochanganywa na mafuta ya taa, ndugu peleka hilo gari kwa wataalam wa mistubishi baada ya hapo pendelea kuweka mafuta ya BP nanzani hilo gari utalipenda kuliko gari aina yoyote............... mafundi hawajayajulia haya magari hivyo wanaeneza habari ya gari sio nzuri... gari mbovu, or gari hizi zinasumbua.
 
Nishaurini wazee tatizo ni nini nimechoka sasa​

Nenda pale Mlimani city road la kwenda Chuo mkono wa kulia ukipita Steers kuna gereji inaitwa 21st Century ni wataalamu wa magari madogo madogo peleka pale.
 
hongera sana kwa kumiliki gari. japo gari lenyewe bovu! usipeleke kwa fundi wala usiuze ,jipatie expiriensi ya ufundi kupitia gari lako. kina bill geti walianza na mtindo huu.
 
Jamani nimenunua Mitsubishi Pajero iO ina kama miezi kumi tu, lakini imeanza kusumbua hasa misi zimekua nyingi na wakati mwingine inanizimikia kwenye foleni hapa mjini.

Nimejaribu mara kadhaa kuipeleka gereji mafundi washanilamba mara kibao lakini tatizo lipo palepale, nimebadilisha kwa maelekezo ya mafundi hadi plug (ambazo zote nne ni kama laki moja) mara mbili lakini bado tatizo lipo palepale.

Nishaurini wazee tatizo ni nini nimechoka sasa​

ndugu baada ya kupokea ushauri wa wanajamii umetatua tatizo lako?si vibaya ukatuambia wengine tatizo ni nini kwani wengine tuko mbioni kumiliki hizo Mitsubishi!

kwa wale walio na ujuzi,hii Mitsubishi airtrek mnaionaje?kuna anayeitumia hii?ina tatizo lolote Cronic?

natafuta kagari kadogo,nimetazama Rav4,Honda,Escudo,Vitara,landrover freelander..,hii mitsubishi airtrek ndio gari pekee iliyonipendeza kwa bei yake.nategemea kutumia 12M max.
 
Back
Top Bottom