Mitsubishi fuso (tipper) ton 10: For sale! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitsubishi fuso (tipper) ton 10: For sale!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Fusofuso, Sep 13, 2011.

 1. F

  Fusofuso Member

  #1
  Sep 13, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJF


  Mitsubishi Fuso 10 ton (tipper) linauzwa. Lina hali nzuri sana! Ni wiki moja tangu limevalishwa tairi 10 mpya. Ni Fuso ya Dec 1994 na limetembea Km 78,201. Liliagizwa toka Japan na linafanya kazi hapa nchini takribani miezi 18 sasa. Usajiri wake : T......BBR
  P1020060.jpg P1020063.jpg
   
 2. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Weka bei
   
 3. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Bandika bei kaka, na linapatikana wapi kwa kulikagua zaidi...Lilikuwa linatumika kwa kazi ipi? Mchanga, Kokoto au kifusi? Sababu ya kuuza ni nini? NB: Nipo serious na manunuzi kama bei itakuwa ya kizalendo na Kwa muda wa 1.5yr usage hapa tz
   
 4. F

  Fusofuso Member

  #4
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Doltyne, naomba niwie radhi sikuwa hewani tangu juzi.

  Bei ninaanziaTSh 55m (mazungumzo yapo). Linapaki Mbuyuni-Kunduchi along Bagamoyo Road. Linauwezo wa kupepa 25ton ni kwa ajili ya kazi zote nzito nzito kama ulivyozitaja baadhi yake hapo juu. Ninaliuza kwa sababu ninahitaji fedha ya kuongezea maana nimeamua kwenda kufanya PhD-UK na nitajilipia gharama zote. Nimehangaika ninatafuta sponsor...lakini wapi...nikaona ni vema niachie huo mtambo. Ni truck zuri sana....japo huwezi kuamini. Please give a try to link up with me if at you are really serious (E-mail: fuso2015@yahoo.com).
   
 5. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  Mkuu, all the best kutafuta phd UK, samahani kwa kuuliza swali ambalo linaweza lisiwe na mantiki kwako kwa sasa. Unasoma ili iweje? Kama ni investment basi kumbuka 55m return yake ni ya muda mrefu ukizingatia utakuwa masomoni kwa miaka mitatu au minne. Kama huna taarifa UK maisha ni ghali sana, 55m ni pesa ndogo sana, kama £20,000 tu, kule kwa mwaka lazima uwe na £12,000 ili uweze kuishi comfortable kidogo kama mwanafunzi, hiyo ni nje ya ada mkuu. Sasa kujisomesha phd kwa budget hiyo mzee itakula kwako. Binafsi nimetoka UK miezi kadhaa iliyopita, nimesoma vema na naajirika lakini siko tayari kuendelea na kazi za kuajiriwa kwahiyo masomo kama phd na masters nimeshayarule out. Sijui umejipanga vipi, ila mkuu bora tipper liendelee kuleta hesabu itakusaidia maisha ya UK.

  Well back to the business, sina budget ya 55m kununua fuso. Realistically hiyo ni bei ya kununua scania 114, au 124 ya tani 32, yenye double diff mbele na nyuma, hapa bongo wanaita mende.

  Nilinunua volvo UK mwezi wa pili mwaka huu, inapiga mzigo fresh na haikufika hata 30m. Na inakula tani 32 mzee. Ndio maana nilikuambia taja bei inayoendana na soko na umri wa gari.

  Kila la kheri mkuu. Tuko pamoja sana tu.
   
 6. Yakuza

  Yakuza Senior Member

  #6
  Sep 15, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu, ninakushukuru sana kwa ushauri wako. Si mgeni sana na gharama za maisha UK, kwa maana nimesoma huko MSc na nilijisomesha...japo ni kama 3 yrs back. Ni bora nika-invest kwenye elimu kwanza....na kama ni maisha yapo tu.

  Juu ya bei za magari hususani trucks, naomba ubofye kwenye hizo links:
  1. Mitsubishi Fuso / Great - Japanese used cars exports and Japan car import / Truck / Sort by : Update - New to Old / Page. 1 [ tradecarview ]
  2. Scania - Japanese used cars exports and Japan car import / Truck / Dump / Sort by : Update - New to Old / Page. 1 [ tradecarview ]

  Na hizo bei ni F.O.B Japan. Exchange rate ya TSh kwa US $ unaifahamu. Makadirio ya kodi na ushuru kwa TRA n.k unayafahamu pia.

  Kama kweli umeweza kuingiza Scania (Mende) yenye double diff mbele na nyuma kwa less than TSh 30m ambayo ni almost US $ 17,000 basi dunia hii na hususani nchi hii ina double standards! Nisaidie kujua website ya huko ulikochukua hiyo Scania (mende).
   
 7. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  Mkuu nadhani hukunisoma vema. Nilisema nimenunua VOLVO kwa ya tani 32, kwa chini ya 30m hiyo mpaka insurance na kodi zote muhimu. Sikusema scania mende kwa 30m, ukisoma vema hapo juu utaona kuwa ni mil 55 ndio scania mende 114 au 124. Kwahiyo rekebisha uelewa kidogo. Kwa msaada wa pili, ukitaka kununua gari ya japan nunua kutoka japan, mf, mitsubishi fuso ukinunua japan utapa bei nzuri, na ukitaka kununua gari iliyotengenezwa ulaya mf scania au volvo, nunua ulaya ndio utapata unafuu. Kama unataka kununua scania au gari yeyote ya ulaya, ingia hapa www.autotrader.co.uk, wakikuuliza post code andika hii M1 1JR. Endelea na mtandao mpaka utakapoona umeridhika.

  Pia angalia siku todauti tofauti, usifanye haraka kununua au kutuma pesa, chunguza bei na asili ya kampuni inayokuuzia. Unaweza kunicheki hapa au ukanipm nikakupa namba yangu.

  All the best.
   
 8. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Upo sahihi mkuu watu wengi tunafikiri maisha ya UK ni mteremko kumbe sio rahisi kihivyo,hata hivyo hatujui kwa undani mipango yake,Kila raheri mwanafunzi mtarajiwa
   
 9. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Kwa gari ya mwaka 1994 hiyo bei haijakaa sawa
   
 10. F

  Fusofuso Member

  #10
  Sep 16, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Babu, hiyo ni bei ya kuanzia......maongezi yapo kwa yeyote aliye serious.....karibu sana!
   
 11. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hayo mattiper hasa hasa Fuso ton 10, si chini ya 60m kwenye show room za Dar. Bado mtu akiagiza toka Japan haliwezi kuwa chini ya hapo, sababu dola impenda sana na TRA nao wako juu kiajabu. Kodi tu ya hilo fuso si chini ya 15m kwa sasa!

  Watu wasikukatishe tamaa na tipper lako ukaliuza kwa bei ya hasara.....Bora ukaendelea kuwa nalo maana huo ni mtaji tosha! Linaweza kubeba mchanga, mawe, kifusi, tofari, kokoto, cement n.k, Mungu akupe nini? Maana ukitaka kujenga nyumba ni rahisi sana kwako! Du, we acha tu..................
   
Loading...