Miti ya majirani ni kero

Nadhani hiyo ndiyo dawn;
Nadhani hiyo ndiyo dawa hata mimi nilikuwa na tatizo kama hilo ila yeye alikuwa akisogeza mpaka mara kwa mara nikaamua kupandisha ukuta na tatizo likaisha.

Katika picha yako mkuu naona unaukuta nadhani hilo eneo korofi upandishe zaidi naamini tatizo litakwisha
 
Muda mwingne inabidi uwe mnafiki.
Tumia trick ya kwenda kujitia unawasaidia tanesco unawatosha kama "kuna mtu amepanda miti imegusa nyaya na inaweza leta shoti ikamisababishia hasara" watakuja kuikata wakimaliza kajitie unampa jirani pole huku unamsaidia kukusanya matawi kumbe unachukua kuni.
 
Kumbe umekimbilia huku kulalamika, umepata ushauri wa kuumaliza mti wangu na chumvi, sawa,Mimi pia nitashughulikia engine ya baby Walker yako na chumvi , tuone Nani chumvi itamliza
 
Fanya hivi,

Nenda kamtembelee jirani yako. Kapige sana stor ikibd unywe na kahawa. Wakat anakutoa jifanye umeshtuka kuona ule mti kisha mwambie "aisee unautajiri hapa, huu mti mizizi yake ni dawa ya nguvu za kiume na pressure. Then sepa..
 
nilijaribu kumwagia sufuria la chumvi ya unga kwenye mwembe wa jirani eti alikuja kuupanda kwenye mpaka,ulikauka fasta
[emoji115] [emoji115] [emoji115]
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Namimi nitafanya !!!
 
Nimewaza.... kuongeza urefu wa ukuta inaweza kuwa suluhisho ila ikawa hatari kwako na kwake. Kwani hapo ukuta ushakamilika kujengwa hivyo sidhani kama kuongeza tofali walau tano kwenda juu ukuta hauta yumba.
Kama fundi mwaah akisema inawezekana basi ongeza ukuta kupita urefu wa huo mti.

Pili ni kwenda kuongea nae kistaarabu tuu kuwa huu mti majani yake yananikera hasa kufagia kila mara naomba matawi ya huku uwe unayapunguza mara kwa mara. Jitahidi uwe kirafiki zaidi na umshawishi akubaliane na takwa lako.

Mwisho mwambie mfanyakazi wako hilo ni zoezi lako kila asubuhi na jioni lazima afagie. Laah wewe mwenyewe ndo uwe unafagia na ujiambie unafanya hivo kama sehemu ya zoezi badala ya kwenda gym ukimaliza unaagiza kanywaji unakokapenda na kitafunio kinachokukuna masikioni.

Life is too short to hold grieves which don't kill you. Just bypass it.

Kasie.
 
mleta mada ulipokosea ni hizo picha ulizoweka. Kama na yeye yupo jf siatajua unachoenda kukifanya.
ila kuna majirani wengine wanawivu na maendeleo ya watu kwa kweli.
kitu simple tu cha kupunguzia matawi inakuwa shida.
pigilia misumari ile mikubwa na Chunvi.
itakauka. ataotesha mingine. ikikua tena fanya hivyo tena
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ndugu yangu mi nakupenda sana na bado nakupenda usihangaike na hizo mbinu za ajabu ajabu ukaonekana mshirikina we nenda kwa balozi au mwenyekiti uongozi wa mtaa yaan hiyo fence tu inakupa nguvu kubwa ya ushawishi wa kukata huo mti kwasabu ni fence ya umeme .viongozi wa mtaa unawaambia kuwa mi nafence ya umeme na mti unagusa fence na siku mvua ikinyesha ?sio sehem salama tena na nashauri wakati au kupunguza mti kabla hayajatoea madhara

Wasipo kuelewa ripot police
 
Kumbe umekimbilia huku kulalamika, umepata ushauri wa kuumaliza mti wangu na chumvi, sawa,Mimi pia nitashughulikia engine ya baby Walker yako na chumvi , tuone Nani chumvi itamliza
Alafu Mimi ndio mwenyekiti wa mtaa namshauri aumwagie chumvi
 
Naombeni kujuzwa taratibu za kufuata ili kuweka uzio wa umeme waungwana.

Huko ulikomwelekeza akaripoti sidhani kama ni mahali sahihi kwa tatizo hilo mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…