Miti iliyoona mengi. Miti iliyokula chumvi nyingi

Miti iliyoona mengi. Miti iliyokula chumvi nyingi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,453
Reaction score
872,065
Ni miti mikongwe duniani.. Toka kila pembe ya dunia.. Imeshuhudia na kuona mengi.. Inayajua mengi mabaya na mema, ya kizani na ya nuruni

Imeshuhudia maanguko ya falme na himaya katili. Imeshuhudia mauaji ya halaiki na kimbari
Imepona vimbunga na mafuriko

Imesalimika ukame wa kutisha. Imesalimika mabaa yatokanayo na matendo ya binadamu, nyuklia, mioto na kila aina ya uchafuzi wa dunia

Imeshuhudia mambo mema pia, neema nyingi na nyakati za furaha., amani na upendo

Ni miti iliyobeba mengi na ndio maana ukikaa karibu yake hukosi kusikia sauti mbalimbali za vicheko, vilio za kutisha , miziki nknk

Ni miti inayoongea. Ni miti inayoimba

Ni miti inayocheza ala za ajabu

Na kubwa kuliko yote ni miti inayoomboleza kwakuwa inaishi wakati si wao na marafiki wa enzi zao wote hawapo
FB_IMG_1742770138303.jpg
 
Back
Top Bottom