Mitego ya dunia hii siiwez!!

Mitego ya dunia hii siiwez!!

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
18,272
Reaction score
20,714
heshima mbele wakuu!!!!!!!!!

wapendwa ngoja nishee na nyie kisa hiki cha kweli kilichonipata mimi siku ya juzi na jana. ni katika hali ya kujengana tu na sina nia ya kumlaumu mtu manake to me its ok maisha yangu na familia yangu ni yangu.

kisa kilianza hivi: mwez wa 10 last yr nilimwoza binti yangu wa kaazi baada ya kuposwa na kijana mmoja alaiyekuwa shamba boy wangu. to me nilifurah kwamba sasa nao wameanza maisha yao ya kujitegemea. sasa basi baada ya mdada huyu kupata mji wake akaniacha na binti mmoja wa kazi mmdogo sana ambaye pia nilimlea kama mwanangu na mwaka huo wa jana alipata kipaimara hapa kijijini. binti huyu naye haku kawia kwani mwaka huo huo wa jana alipoenda kwao kucheza sikukuu hakurudi tena kwa kisingizio kwamba dada yake kajifungua na hana msaidizi.

sasa ngoma ikaanza juu ya wapi nipate binti. kama ujuavyo ukifikia stage hii lazima akili ikukae sawa wewe mama nikaanza kuulizia kwa kila jamaa na rafiki Mungu bariki nikapata mdada toka rombo.Mdada huyu alikuwa ni mama wa watoto 3. na katika hao mdogo ni wa miezi 9 ananyonya. kwangu mm nikasema poa tu njoo ila uje na mwanao huyo anayenyonya. kwangu mm nililenga njia hii inipunguzue kadhia za leo mwanagu anaumwa nataka niende nikamwone so nilijua akiwa hapa ni rahisi ku monitor mambo yote kisawasawa.

binti alikuja na mwanaye mzuri sana wa kiume, walipendezana na wanangu na maisha yakaasonga mbele. baada ya miez miwili yaani nilipokuwa msibani iringa nilimwacha nyumban mwanae kwan nilijua kwenda nae na kazi za kwenye msiba ni kumtesa dada wa watu. ilinilazimu kusafiri mm na wanangu na nikamuacha na mkaka wa shamba walinde nyumba. nikiwa safarini alinipigia simu kwamba mtoto wake anaumwa basi mm nikamwambaie ampeleke kituo cha afya aapte matibabu. nilishindwa kuish kwa amani so ikanilazimu kuanza safari kurudi huku usiku ili kumuwah binti. nilipofka home nikamkuta mwanae ni mzima wa afya kumuuliza akasema alitapika baada ya kujaribu kumeza kitu kikamkaba. nilichuukia lkn nikasema haina tabu maisha yasonge mbele.

siku tatu baadae simu ya binti ikapigwa dada akaongea kisha akasema mama yupo hapa ongea nae. akaniletea simu mama ongea na baba brayai (baba wa mtoto wake). nikaipokea simu. ile tu nasema halooo!!!!!!!! iliipokelewa na sauti ya ukali san atoka kwa baba mwenye mtt kwamba anamtaka mwanae arudishwe Rombo na mama yake. basi mie kuskia maneno sentensi ya ukali hivyo nikamjibu

''usinieleze upumbavu ongea na mzazi mwenzio""

basi nikairudisha simu binti na yeye binti akakata. kisha nikamuuliza imekuwaje???/ akasema mama baba mtoto anamtaka mwanae na mm nataka nimpeleke kwani katika wababa wote 3 nilio zaa nao huyu ndo ambaye hamalei mwanae na ananifanya mm nateseka sana sasa naona bora nimrudishe tu kwa baba yake nije niendelee na kazi.

kiutu uzima nikamjibu huogopi mtoto mdago kama huyu kumpelekea baba mtoto tena baba yake ni mume wa mtu?? huoni kwamba hata mama wa kambo hatoweza kumkubali mtoto wa kupakatwa na kubebewa mgongoni?? mbona mtoto ni mdogo sana huyu?? akanijibu....................""acha tu mama huyu mtoto amenitesa sana siongei na baba yangu wala mama yangu kisa huyu mtoto""
mie nikamwambia kwani mwanao anakosa gani?? mbona kama makosa ni yako?? akasema """""""""""hapana wazazi wangu hawamapendi mwanangu. """"""""""

baadae akaanza kusema ni lazima wiki hii nimrudishe mwanagu. akiwa anang'ang'ana sana nikapata hofu kulikoni?? nikaamua kuchunguza kuna nini. nikagundua kwamba binti na mkaka wa shamba ni marafiki ok sio vibaya manake wote ni vijana na hawana wenza. ila kijana hataki kuwa na mdada kama bado ataendelea kua na mtoto hapa!!!!!!!!!! kibaya zaid kumbe binti kesha pewa mimba na mkaka wa kazi na ndio maana anataka kumrudisha mtoto ili alee mimba yake.

hapa akili ikanikaa kumkichwa, sasa nafanyeje?? nikamuuliza mama mtoto inakuwaje?? akasema yeye anataka kumrudisha mwanae kijijini. nikamuuliza mkaka akasema

"""binti ana mimba yangu na mm sina uwezo wa kuwahudumia yeye na mwanae hivyo amrudishe mwanae kwa baba yake kisha arudi mie nitamwoa""" .................mmmh! binti kuskia ndoa hakutaka kauskiliza ushauri mwingine so far nikasema niwaache kwanza huku nikipata akili ya kazi.

kweli ikabidi nianze kusaka mdada mwingine ili huyu akiondoka basi niwe na mbadala wake. nikiwa nahangaika tena kwa kupiga simu binti alinisikia hivyo akasema

"""mama kwakua steven yuko hapa bado acha mie nimrudishe mtoto kisha nirudi niendelee na kazi kama kawaida na kwakua hapa ndo nyumban basi mie nitakuwepo"" nikajismea ni wazo zuri sana lakin je kama akipata matataizo haya ya uzazi ya kileo nitaelekea wapi mie?? istoshe mbona kama ni bora akakaa kwa huyo mkaka mie nikawa na binti wangu mwingine na kama pakitokea uhitaj basi nitamtumia kama kibarua??

haya mie nikamwambia kwamba ampeleke mwanae mie aniache kwanza nipate maarifa. kweli majuzi akaondoka kwenda kwao.

PART 11
baada ya binti kuondoka nikawa nawaza nampata wapi binti mwingine?? bahati nzuri nikapata sms tokana kwa shoga yangu kwamba anabinti msukuma amekaa nae miezi miwili ila anaoa mabinti watatu na anaona hawez kuwa nao wote.
hivyo kama kuna mtu anahitaji mmoja nimwambieee!!!!!!!!!!!!

mie nikamjibu mlete kwangu mwali mie mdada wangu kaondoka leo. basi nikamshukuru sana Mungu kwa hilo nikaona maisha sasa yataenda sawa.

kweli mida ya saa tisa mchana shoga yangu anaingia akiwa na binti. Binti huyu ni mzuri sana mashalla Mungu kamuumba. sisemi uongo ni binti wa miaka 21 mnene kiasi ana umbo zuri sana na miguu mashalla. kajaliwa kimo na nywele ndefu. pia ana nidham na ni msaf sana. alikuja amevaa sketi ya kadeti wallah nilisema ama kweli Mungu ahimidiwe kwa uumbaji wake.

basi shoga akanieleza kwann anamtoa kwake kwamba wako wa3 ila pia binti ni mzembe sana wa kazi yaani anafanya taratibu sana sasa waliobaki ni washapu ila huyu anawatia uvivu. Mie nikamjibu kwakuwa siku hizi kangu nimepunguza kazi basi atapaweza kwani wanangu ni wakubwa kikubwa napenda usafi tu.

shoga akaniambia kwa usafi kuanzia kudeki kuosha vyombo ni mzuri sana na hata usafi wa mwili wake yeye na nywele. nikamjibu haya basi nikamkaribisha mdada ndani tuanze maisha. kweli akawa hana wasiwasi na kazi ya kwanza alianza na kuosha vyombo nilimpenda bure. dada wa watu hata mchanga anasugulia sufuria na zinatoka kama zimeoshwa kwa stili wire. nilimshukuruje Mungu sasa??

usiku uliingia tukalala. jana asbh nimelala kwamba siendi kazini ili nimkalizie nimwelekeze kazi zangu hasa kumwagilia ghafla nashangaa mlango wangu unagogwa nikasema ingia. Binti akaingia akiwa analia anasema

""" nimepigiwa simu sasa hivi shagazi yangu kapata ajali alikuwa anakuja dar sasa ninataka niende nyumbani!!""

nkamjibu unayo nauli?? akasema """mpigie shoga yako aniletee nauli niondoke!!......................
mie nikasema sawa. akafunga mlango akaenda chumban kwake. nikanyua wire nikamtwangia shosti. nikamsimulia kila kitu kuhusiana na binti.
shosti akanijibu .........."" mwongo huyo anataka kunichezea akili na sasa simwogopi mwambie sina nauli nimempa mshahara wake wote sasa kama ni vipi autumie huo kuwa nauli"""...............mmmh! nikasema leo ninalo manake binti analia ile mbaya. lakin nikaendelea kujihoji kwann shoga amesema kwa ukali sana?? kuna nini katikati??

nikaona nimtulize binti wa maneno makali ili sasa akisha tulia aamue anataka kaazi ama kweda kwao. ila nitahakikisha kulikoni kati ya binti na bosi wake wa kwanza??

baada ya kuongea nae akanitii na kunyamaza, mchanaa nikaona isiwe tabu nikapika ugali wangu na dagaa tule na wanangu. baada ya kauivisha namwita binti njoo ule binti akagoma mara moja nikagundua binti amesusa kula. nikamwambia ukitaka tukosane wewe nisusie mie msosi utakiona cha mtema kuni. lakin hakuna na mm nikasema kuna jambo ngoja nivute muda nimhoji baadae.

niliendelea ku note kwamba simu ya dada iko bize sana na ikipigwa anongelea chumban ama nje ila sio kwenye uso wangu...................nikajiuliza..............????
baadae nikaaza kupika chakula cha jion nikatoka kwenda jikon. nikamwita tupike. ghafla simu yake ikaita akaenda mwisho wa uwanja kuongea ila sasa hakujua kwamba kwasababu niko nje upepo unapeperusha sauti yake so namsikia kila kitu anachokiongea. nikamsikilza kwa makini kweli nikajua aaah!!! kumbe tatizo liko hapa??

tatizo ni nini??
Binti alitafutwa na mwanaume, na ndiye aliyemtumia nauli ya kuja kazini. istoshe baba hakumshirikisha mama na hata siku binti anaanza safari baba ndiye alikuwa na taarifa. na kwakuwa baba alikuwa kikazi Dodoma alimwambia binti akifika dodoma ashuke stendi kisha watakuja wote dar. basi binti alishuka kweli stendi na akapokelewa na mwenyeji wake wakaenda hotelini wote.

hotelin binti anasema alikaa chumba cha peke yake pamoja na mdada mwingine ila walikaa siku 3 kabla ya kuanza safari ya kuja dar. siku zote walizokaa pale hata kula alikuwa anaambiwa akale meza moja na baba ila alijiogopea hivyo akawa anawaomba wamletee chakula chumbani( haya ni maneno ya binti)

basi baada ya siku 3 wakaanza safari mchana kuja dar, walipofika nyumban mama hakuwepo na so alipigwa simu akaja akawakuta binti akatambulishwa kwa mama mweye nyumba maisha yakaanza.

kama kawaida mtaani maneno hayakosekani basi mtaa ukaanza oooh! huyu binnti ni chakula cha mwenye nyumba mara oooh! mwondoshe huyu kama hujamleta wewe mama nakuambia atakupindua mara sijui lellelelll! manen yakawa meeeeeeeeeeengi mama akaona mmh! asiyeskia la mkuu huvunjika guu................... akaona amtoe amlaete kwangu.

sasa binti alipokata simu tu nikamkaba kwenye kona nzuri ya upendo na umama akanieleza mkanda mzima ulivyokuwa nikasemaa ama kweli kumbeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!

ndipo nikatafaari kama ni shoga yangu na huu ndo ulikuwa wasiwasi wake kwann asingeniambia ukweli juu ya kwann amemwondosha?? sikatai mm kwasababu niko mama tu sina hofu na chochote labda klein wangu lakin najiuliza nitafanyaje kama binti hajatulia asije akaniletea zahama kwa wanangu??

baadae nikawaza nikampa limitation hasa za aina za nguo za kuvaa, na namna ya kukaaa halafu sasa niko pembeni nasubiria movie nione itaendeleaje.
 
Mh!So sad!But kuwa makini sana nae!
'
Ila kwa ushauri wangu tafuta mwingine!
 
gfsonwin dah visa vyako bala a
Ila angalia sana kupinduliwa kwako kuko karibu na wewe
Usilemae na usiridhike sana kuwa umepata maana kama ni tabia yake itakuja kwako pia
 
Last edited by a moderator:
Stori ndefu ya maisha yenye kufundisha uvumilivu. Kwa jinsi ulivyosimulia uzuri wa huyo msichana, lazima anyakuliwe na wanaume! Mwalimu wangu gfsonwin, huna kitu hapo jiandae kumtafuta mwingine Rombo haraka sana.
 
Last edited by a moderator:
Mungu akubariki na akuzidishie moyo wa huruma na msaada kwa wasionacho na baraka zake zitakuwa juu yako na familia yako.
 
pole gfsonwin kuwa mama ni kazi na kupewa jukumu la kulea familia unatunukiwa hekima. Wschana wa kazi ni tatizo kwenye familia nyingi kama ilivyo tatizo la kupunguza vitambi na unene kwa wengi ilhali wanaendelea kutumia mvinyo na nyama choma kwa wingi bila mazoezi na kufuata balanced diet.

Mimi nimeathiriwa sana na waschana wa kazi kiasi kwamba nimeapa mtoto wangu wa mwisho akifika darasa la 5 na more mdada wa kazi ntumbani iwe iweje. Sasa changamoto niliyonayo ni kuanzia sasa hadi mtoto wangu wa mwisho afike darasa la tano nakabiliana nao vp? waschana wamenitenda, wamenikwaza, kunaniliobahatisha wazuri na waaminifu ila hawakukaa kwa sababu moja ama nyingine ila nao ni binadamu na huwa nawaza je ningekuwa mie ndo house girl nimejikuta nimezaliwa kwenye familia inayonibidi nikafanye kazi kwa watu ndo nipate kipato ningebehave vipi kukabiliana na changamoto za kazi ikiwemo kulazimishwa mapenz na baba wenyenyumba, watoto wa wenye nyuma, ndugu wa familia husika, wauza genge na maduka pale mtaani n.k
Nakosa jibu na kumuomba mungu huyu mtoto wangu afike haraka hiyo darasa la 5 ili niingie phase 2 ya kutokuwa na house girl ambapo mie na watoto wangu tukiwa na uzima wa mwenyezi mungu tutagawana majukumu ya nyumba na kushirikiana as a family team.
Nakuombea hekima ya mungu ikutangulie kufanya maamuzi juu ya wafanyakazi wa nyumbani kwako gfsonwin
ila mumeo hayupo? unahisi atakuwa threat kwa huyu mshana mpya? na umekuwa ukiongea na Klein kuhusu kuwa na mahusiano na waschana? either wa mtaani au shuleni au wadada wa kazi-housegirls?
 
Last edited by a moderator:
pole gfsonwin kuwa mama ni kazi na kupewa jukumu la kulea familia unatunukiwa hekima. Wschana wa kazi ni tatizo kwenye familia nyingi kama ilivyo tatizo la kupunguza vitambi na unene kwa wengi ilhali wanaendelea kutumia mvinyo na nyama choma kwa wingi bila mazoezi na kufuata balanced diet.

Mimi nimeathiriwa sana na waschana wa kazi kiasi kwamba nimeapa mtoto wangu wa mwisho akifika darasa la 5 na more mdada wa kazi ntumbani iwe iweje. Sasa changamoto niliyonayo ni kuanzia sasa hadi mtoto wangu wa mwisho afike darasa la tano nakabiliana nao vp? waschana wamenitenda, wamenikwaza, kunaniliobahatisha wazuri na waaminifu ila hawakukaa kwa sababu moja ama nyingine ila nao ni binadamu na huwa nawaza je ningekuwa mie ndo house girl nimejikuta nimezaliwa kwenye familia inayonibidi nikafanye kazi kwa watu ndo nipate kipato ningebehave vipi kukabiliana na changamoto za kazi ikiwemo kulazimishwa mapenz na baba wenyenyumba, watoto wa wenye nyuma, ndugu wa familia husika, wauza genge na maduka pale mtaani n.k
Nakosa jibu na kumuomba mungu huyu mtoto wangu afike haraka hiyo darasa la 5 ili niingie phase 2 ya kutokuwa na house girl ambapo mie na watoto wangu tukiwa na uzima wa mwenyezi mungu tutagawana majukumu ya nyumba na kushirikiana as a family team.
Nakuombea hekima ya mungu ikutangulie kufanya maamuzi juu ya wafanyakazi wa nyumbani kwako gfsonwin
ila mumeo hayupo? unahisi atakuwa threat kwa huyu mshana mpya? na umekuwa ukiongea na Klein kuhusu kuwa na mahusiano na waschana? either wa mtaani au shuleni au wadada wa kazi-housegirls?
sakapal baba Klein hayupo na yeye kama mwanaume siwez kusema hatoanguka dhambini ama la kwani nayeye ni binadamu kama wanaume wengine. na akianguka yeye dhambini kama mtu mzima ataniumiza mm sana sana ila sitokuwa na la kufanya manake yeye kaona hii ndio busara zaid.

kwangu mm sasa hivi nalia na Klein jaman, nimeshaongea nae kwa maneno na hata kwa biblia sasa nimebaki kusali tu. hofu yangu ni kwamba kama akiwa kiruka njia si ndo mwanzo wa kuleta magonjwa kwa watu wa karibu yangu??
 
Last edited by a moderator:
Stori ndefu ya maisha yenye kufundisha uvumilivu. Kwa jinsi ulivyosimulia uzuri wa huyo msichana, lazima anyakuliwe na wanaume! Mwalimu wangu gfsonwin, huna kitu hapo jiandae kumtafuta mwingine Rombo haraka sana.
sawa nitafwata ushauri wako HYGEIA
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin dah visa vyako bala a
Ila angalia sana kupinduliwa kwako kuko karibu na wewe
Usilemae na usiridhike sana kuwa umepata maana kama ni tabia yake itakuja kwako pia

yaani Mr Rocky sijui ni kwann huyu anabeba mimba, huyu nampata kimeo yaani nimepatikana mwaka huu.
 
Last edited by a moderator:
sakapal baba Klein hayupo na yeye kama mwanaume siwez kusema hatoanguka dhambini ama la kwani nayeye ni binadamu kama wanaume wengine. na akianguka yeye dhambini kama mtu mzima ataniumiza mm sana sana ila sitokuwa na la kufanya manake yeye kaona hii ndio busara zaid.

kwangu mm sasa hivi nalia na Klein jaman, nimeshaongea nae kwa maneno na hata kwa biblia sasa nimebaki kusali tu. hofu yangu ni kwamba kama akiwa kiruka njia si ndo mwanzo wa kuleta magonjwa kwa watu wa karibu yangu??

dawa iliyobaki yenye usalama na uhakika rohoni ni maombi tuuu, usiache kusali.
 
kikulacho shoga

umenena lolz!
hapa niko chumban naandika yeye yuko bafuni anafua iyo kanga alovaa ni moja tena fupi bila blauzi.
nimemchungulia ufuaji wake nikasema hapa mguu sawa.
 
mwali una kadi yake ka clinic huyu bidada?
na hao huyo mama bray?
hebu fanya maamuzi magumu!mabwe mbali ujue mpka ufike utakuwa ushalia sana ushindwe hata kunieleza kimetokea nini baada ya hapa!MI STAKI bana!
 
gfsonwin the story is too long, ntamalizia laterz. lakini nimeona part II una mashaka na HG aliyeumbika, naomba umlete kwangu ili kulinda wanao halafu ntakutafutia mwingine ambaye ni "average looks na salama"
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom