Mitazamo chanya katika biashara ya kupangisha vyumba/vyumba

sabuwanka

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
690
751
Ndugu zangu salaam,

Mwaka 2013 kulianzishwa uzi humu ukiwa unazungumzia kuwa mtu anajenga nyumba kwa ajili ya kupangisha hawezi kupata faida, great thinkers Wengi walitoa maoni na mitazamo yao.

Miaka imepita, sera zimebadilika,uwekezaji umeongezeka na idadi ya watu mijini imeongezeka, kipekee napenda tusikie mawazo kutoka kwa waliojenga nyumba za kupangisha jinsi zinavyowalipa na kupunguza umaskini au jinsi zinavyongeza umaskini, mawazo hayo ni msaada kwa wengine walio na nia ya kufanya biashara hiyo.

Mwisho nawapongeza wote tulioshiriki kuingiza Tanzania katika nchi zenye uchumi wa Kati.

Asanteni
 
Nina Nyumba nilijenga 2013 mwaka huu mwezi wa pili imenirushia pesa yangu yote niliyotumia kujengea halafu kodi nimepangisha na hakuna wa kunipangia hivyo sasa nakula faida tu.
Miaka saba pesa inerudi, sio mbaya ukitoa mental picture ya nyumba na unaonaje uwekezaji wa nyumba ni salama? Mambo gani yazingatiwe?
 
Miaka saba pesa inerudi, sio mbaya ukitoa mental picture ya nyumba na unaonaje uwekezaji wa nyumba ni salama? Mambo gani yazingatiwe?
Nyumba gharama ya ujenzi kwa kipindi kile gharama 22M na kidogo Nyumba ni vyumba tatu kimoja master vya kawaida 10 kwa 10 sitting room na dinning ya kishkaji jiko Dogo choo cha ndani tiles gypsum kodi nikianza kwa 250k kama mwaka nikampandishia mpk 300k na sasa nataka nimpandishie ifike 350k kwa mwezi pameshakuwa town sana halafu karelax sana inabidi apate akili na yeye ya kuijenga kwake.

Changamoto kubwa ni wapangaji tu ukipata wapangaji wanaojali na Nyumba faida utaiona, ila kingine ukijenga Nyumba ya kupangisha chumba kimoja kimoja pasua kichwa %kubwa wapangaji wake huwa majanga tupu
 
Nyumba gharama ya ujenzi kwa kipindi kile gharama 22M na kidogo Nyumba ni vyumba tatu kimoja master vya kawaida 10 kwa 10 sitting room na dinning ya kishkaji jiko Dogo choo cha ndani tiles gypsum kodi nikianza kwa 250k kama mwaka nikampandishia mpk 300k na sasa nataka nimpandishie ifike 350k kwa mwezi pameshakuwa town sana halafu karelax sana inabidi apate akili na yeye ya kuijenga kwake,
Changamoto kubwa ni wapangaji tu ukipata wapangaji wanaojali na Nyumba faida utaiona, ila kingine ukijenga Nyumba ya kupangisha chumba kimoja kimoja pasua kichwa %kubwa wapangaji wake huwa majanga tupu
Chumba kimoja kimoja rahisi kupata wateja kwa sababu bei rahisi.
 
At least fanya chumba self na sebule,ule laki laki kwa mwezi
Hapo ndo unakula hasara. chumba kimoja tufanye ni 50, kwahio viwili yani chumba na sebule inabidi iwe laki, sasa hiko choo cha ndani huoni utakua umekigawa bure? chumba self + sebule inabidi iwe 150. kwa laki inabidi upangishe chumba na sebule ila choo cha public.

ila pia inategemea eneo na eneo kwahio siwezi kukubishia sana bei yako.
 
Ukiwa na nyumba 3+ ili uone mafanikio

1. Uwe na mwana sheria, huyu atakuandikia mikataba na kukusaidia katika Maswala ya wapangaji wasiolipa kodi na kuharibu nyumba.

2. Uwe na Timu ya mafundi kuanzia fundi bomba, umeme, carpenter nk. Hawa watashughulika na matengenezo na uwape uhuru wa kufanya kazi nyingine kama huwahitaji.

3. Uwe na rent account wapangaji walipe hela huko.
 
Ng'ombe mmoja mwenye maziwa mazuri sio chini ya 20ltr day.(kisio la chin)
Una ng'ombe 3...kwa siku sio chini la 50lts...uza kwa 1000/-@...una 50,000/-
Kwa mwezi una ngap??....
Mie naona uzuri wa nyumba maybe kuombea mkopo...! Lakini ujenge upangishe laki??? Bora ufuge ng'ombe!
kwa hio unawashauri wale wanaojenga apartments za 450K hadi 600K waamie kwenye ufugaji wa ng'ombe wa maziwa?
 
Back
Top Bottom