Mitandao ya simu: Kuna nini nyuma ya pazia?

Mitandao ya simu: Kuna nini nyuma ya pazia?

Nunueni bundle ya internet separately. tumieni ile ya zantel (200mb - kwa sh.500). piga *149*07#
 
Na hiki ndicho alichokiandika kuhusu hii mitandao ya simu 1423823290784.jpg
 
Vodacom pamoja na Tigo Leo wameshangaza Watanzania, hii ni baada ya kupunguza muda wa maongezi pamoja na MB. Bado hawajaweka bayana nini kinachoendelea chini ya kapeti tumesubiri hata kutumiwa ujumbe ila hakuna kitu.
==================

attachment.php


January Makamba vipi tena mbona unajipinga mwenyewe: 1. unasema TCRA haishughulikii bei, 2. halafu unaagiza TCRA iangalie suala la bei.

Halafu ni aibu kwa waziri mwenye dhamana kutokujua vizuri kazi za TCRA kwani inashughulikia mpaka bei someni kwenye tovuti yake https://www.tcra.go.tz/
 
Huu Ni Wizi Uliotukuka,serikali Ni Wezi Na Viongozi Wake Wote Wezi Sasa Imekua Desturi Watanzania Kuibiwa Kila Kukicha.Ni Viongozi Gani Wasiokuwa Na Hofu Ya Mungu Hawaoni Aibu Ya Wanayoyafanya
 
Je bundle ya internet imekuwaje kwa sasa
Vodacom bado kwenye bundle ya Internet imebaki vilevile
Noana mitandao yote wameamua kutenganisha muda wa maongezi isiwe na bundle za Internet
Airtel bado ni affordable network of all times....
Nikijiunga vifurushi vya data tupu napata 2.5 GB kwa 2500/= kwa wiki unaona unafuu huo?
Kile kifurushi Chao cha uni 255 bado unapata 1gb kwa 1500 kwa wiki....
 
Vodacom bado kwenye bundle ya Internet imebaki vilevile
Noana mitandao yote wameamua kutenganisha muda wa maongezi isiwe na bundle za Internet

Yeah naona wameamua wafanye hivyo wote kwa pamoja
 
Kupitia account yake ya twitter na Instagram

Nimeongea Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Nkoma, kumuagiza azungumze na makampuni ya simu juu ya mabadiliko ya bei za bundles: ukubwa, ughafla na upamoja (mitandao yote). Nimewaagiza pia watoe majibu kwa umma haraka iwezekanavyo. Makampuni ya simu hayapaswi kupanga au kuratibu kwa pamoja bei; tukigundua hilo limetokea ni ukiukwaji wa kanuni za ushindani wa soko. Sheria ya udhibiti wa Mawasiliano haitupi nguvu (Serikali) ya kupanga bei, isipokuwa interconnection fees. Inawezekana gharama za uendeshaji, ikiwemo umeme, zinapanda, lakini hakuna kodi mpya ya Serikali tangu baada ya bajeti. Huko nyuma ushindani ulishusha bei kwasababu hakukuwa na bei elekezi. Bado niko nje ya nchi kwa safari ya Kiserikali, lakini nimekuwa nalifuatilia suala hili kwa karibu. Pia nimeongea na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Rene Meza, kuhusu suala hili leo asubuhi.
 

Attachments

  • 1423827500520.jpg
    1423827500520.jpg
    48.7 KB · Views: 170
Airtel bado ni affordable network of all times....

Nikijiunga vifurushi vya data tupu napata 2.5 GB kwa 2500/= kwa wiki unaona unafuu huo?

Kile kifurushi Chao cha uni 255 bado unapata 1gb kwa 1500 kwa wiki....

Binam kucheka zantel ni aje niwahame voda wamenichoshaaaaa
 
Dah tunaibiwa tena! inanikumbusha enzi za mobitel na tritel hii nchi sio tanzania ila inaitwa KAZANIA bila hivyo huwezi ishi
 
Serikali imezitaka kampuni za Simu inchini kupandisha gharama za kupiga kupokea na bando ya internet ili kuweza kupata pesa za kukamilisha uboreshaji wa daftari la mpiga kura na kura ya maoni kufikia Jana usiku bei zimeanza kupanda Kwa asilimia 79
Sasa ukinunua bando ya internet Tsh 2000 unapata 20 Mb tu.

Mamba 20 yaliyoachwa kwenye rasimu ya katiba - By PolePole


MAMBO 20 MUHIMU YA WANANCHI YALIYOTUPWA NA KATIBA INAYOPENDEKEZWA.

UNATAKA KUUJUA UKWELI BASI SOMA HAPA NA MJULISHE MWENZIO.

Katiba Inayopendekezwa ina mapungufu makubwa na imeyatupilia mbali maoni muhimu ya wananchi kama yalivyotolewa na wananchi wenyewe kama ifuatavyo;-1. Kupunguzwa kwa madaraka ya Rais Wananchi walipendekeza madaraka makubwa ya Rais hasa ya uteuzi yapunguzwe na ziundwe Taasisi za kikatiba za kumshauri Rais kabla hajafanya teuzi. Wananchi walipendekeza pia baada ya Rais kumteua kiongozi basi itabidi mteuliwa huyo Bunge limthibitishe. Katiba Inayopendekezwa imeyafuta haya yote na imemuongezea Rais Madaraka.

2. Kutenganisha Mamlaka ya Mihimili ya Dola Wananchi walipendekeza uhuru zaidi kwa Bunge na Mamlaka zaidi kwa Bunge kuisimamia, kuiwajibisha na kuishauri Serikali. Pendekezo hili linaenda sambamba na kutenganisha serikali na Bunge, hali ambayo iko sasa. Rasimu ya Warioba ililipa Bunge Mamlaka zaidi kuisimamia Serikali na hata pale ambapo Bunge lingekataa bajeti au muswada mbaya wa serikali mara kadhaa, Rais asingeliweza kulivunja Bunge. Wananchi walisema sana Mawaziri wasitokane na wabunge, ili wabunge wafanye kazi ya uwakilishi pekee na mawaziri watumie weledi wao kumsaidia Rais kazi za Serikali.

3. Kumwajibisha Mbunge Rasimu ya Warioba iliwapa wapiga kura uwezo wa kuwawajibisha Wabunge kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani nao wakati wowote (Recall Powers) kama wakienda kinyume na maslahi ya wananchi katika jimbo husika. Wananchi walijiuliza kama mbunge ni mtumishi wao, iweje hayuko katika kituo cha kazi kwa miezi kadhaa na wasiweze kumwajibisha mpaka miaka mitano?

4. Vyanzo vya Mapato vya kuaminika Kuwepo kwa vyanzo vya mapato vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano vitakavyogharimia mambo ya Muungano ambayo yamepunguzwa kutoka 22 hadi 7 lilikuwa pendekezo ambalo hata taasisi za serikali zilipendekeza. Pendekezo la Katiba Inayopendekezwa imerudisha mapato ya Muungano kama Katiba ya Mwaka 1977, na kwa kufanya hivyo tumerudi kwenye mgogoro wa msingi, kuchukua kodi tatu, ushuru wa forodha, ushuru wa bidhaa na mapato kutoka Zanzibar ni kuiua Zanzibar na kuifanya ishindwe kumudu matumizi yake ya ndani kwa mambo yasiyo ya Muungano na vivyo hivyo kwa Tanganyika.

5. Muundo wa Shirikisho lenye Mamlaka Kamili Kwa miaka nenda rudi tumekuwa na kitendawili cha ni muundo gani wa Muungano Jamhuri yetu inao. Kitendawili hiki kimeelezwa na wengi akiwemo Baba wa Taifa Mw. J.K Nyerere. Rasimu ya Warioba iliweka kwa mara ya kwanza Muundo Jamhuri ya Muungano kuwa ni wa Shirikisho lenye Mamlaka Kamili na lenye Serikali 3.

6. Kupunguza ukubwa wa Serikali Wananchi walionesha kutofurahishwa na ukubwa wa serikali unaopelekea matumizi makubwa ya fedha za walipa kodi. Walipendekeza uwepo wa serikali ya muungano iliyo imara, yenye ufanisi na ndogo. Rasimu ya Warioba ilisema idadi ya mawaziri isizidi 15, Katiba Inayopendekezwa inasema Mawaziri wasizidi 40

7. Tume ya Uhusiano na Uratibu Rasimu ya Warioba ililenga kuhakikisha kunakuwepo uhusiano mzuri, mawasiliano na uratibu wa serikali zote tatu chini ya Mamlaka ya Serikali ya Muungano na kupitia Tume ya Uhusiano na Uratibu. Bunge Maalum lilishindwa kuelewa mantiki ya pendekezo hili na Katiba Inayopendekezwa imelivuruga kabisa, kutoka pendekezo la Warioba la “Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali” hadi “Tume ya Uratibu wa Mambo ya Muungano” katika Katiba Inayopendekezwa.

8. Kupunguza ukubwa wa Bunge Wananchi walizungumzia pia ukubwa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na gharama zinazoambatana nalo, na wakapendeza bunge dogo na lenye ufanisi mkubwa. Warioba alisema idadi ya wabunge isizidi 75, Bunge Maalum likasema Wabunge 390.

9. Ukomo wa vipindi vya ubunge Wananchi walizungumzia nafasi za ubunge kuhodhiwa na watu fulani kwa miaka nenda rudi na wakapendekeza ifike mahali kuwe na ukomo ili kuleta uwakilishi mpana na mabadiliko. Rasimu ya Warioba iliweka ukomo wa vipindi vya ubunge kuwa vitatu na kuwa na ukomo wa miaka 15 kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Bunge Maalum na Katiba Inayopendekezwa wamefuta pendekezo hili.

10. Kuwepo kwa Tunu za Taifa (Core Values) Wananchi walipendekeza uwepo wa tunu za Taifa (core values) katika katiba, tunu hizi ni pamoja na utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya Taifa. Raia wa Tanzania walikuwa na wajibu wa kuheshimu tunu hizi lakini Katiba Inayopendekezwa imezifuta tunu hizi.

11. Maadili na Miiko ya Viongozi Wananchi walizungumza kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya jamii, watumishi na viongozi wa umma, wengi wakisema Katiba iainishe Maadili na miiko ya viongozi wa umma ambayo kwayo tutawawajibisha. Katiba Inayopendekezwa imesema Maadili na Miiko kwa viongozi (mathalani kutenganisha biashara na uongozi ili kuepusha mgongano wa maslahi), isiwemo kwenye Katiba bali ikawekwe kwenye Sheria.

12. Masharti yasiyoweza kubadilishwa na Bunge Rasimu ya Warioba iliweka masharti ya kuzuia Bunge kubadili baadhi ya masharti mahususi ya Katiba (entrenched provision) ibara ya 119 isipokuwa kwa ridhaa ya wananchi kupitia kura ya maoni (mathalan Malengo Makuu ya Taifa, Haki za Binadamu n.k. Na bahati mbaya tulisahau kuweka na Sura ya 3 juu ya Maadili). Masharti yote ya Ibara hii yamefutwa isipokuwa Muundo wa Muungano na Uwepo wa Jamhuri ya Muungano.

13. Kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi Wananchi walizungumza umuhimu wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia chaguzi za Jamhuri ya Muungano. Ilisisitizwa juu ya umuhimu wa Tume kugawa majimbo ya uchaguzi na kwamba Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake wathibitishwe na Bunge ili kuwapa uhalali wa kitaifa, pendekezo hili limefutwa na Katiba Inayopendekezwa.

14. Usawa wa 50:50 kati ya wanawake na wanaume Kuwepo uwiano wa uwalikishi wa 50:50 kati ya wanawake na wanaume ni lazima kwa mazingira ya sasa. Uwiano kati ya wanawake na wanaume katika vyombo mbalimbali vya dola hasa vile vya kutung sheria limeendelea kuwa tatizo nchini na lililokaa kwa muda mrefu. Wananchi na hasa wanawake na baadhi ya wanaume walipendekeza uwiano ulio sawa katika kufikia fursa hasa ukizingatia wanawake ndio wazalishaji wakubwa. Katiba Inayopendekezwa imefutilia mbali pendekezo hili muhimu.

15. Kuanzishwa kwa Mgombea Huru Haki ya wananchi kushiriki shughuli za umma imekuwa ikizuiwa siku nyingi na kwamba ushiriki katika shughuli za umma kama kiongozi wa kuchaguliwa inapaswa kuwa haki ya msingi ya mwananchi yeyote yule. Rasimu ilitoa haki ya mgombea huru bila vikwazo, Katiba Inayopendekezwa imeweka masharti magumu ambayo hakuna mtu anayeweza kuyatimiza kirahisi, kitendo hiki sio sawa.

16. Msaada wa Kisheria kwa Wananchi Wananchi walieleza kutokuridhishwa kwao na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wenye uhitaji huo na wakapenda huduma ya msaada wa kisheria liwe suala la kikatiba kwa mwananchi yeyote yule na serikali iwajibike kutoa huduma hiyo. Katiba Inayopendekezwa imesema wananchi hawatakuwa na haki ya kudai huduma hii kokote nchini, hata mahakama hazitaweza kusikiliza mashauri ama Serikali imetoa haki hii au haikutoa haki hii rejea Ibara ya 21.

17. Uhuru wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Rasimu ya Warioba ilipendekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi atekeleze kazi zake kwa uhuru, bila woga, upendeleo wala chuki na kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria za nchi. Masharti haya yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa

18. Tume ya Utumishi wa Jeshi la Wananchi Tume ya Warioba ilipendekeza kuwepo kwa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania itakayokuwa na jukumu la kusimamia masuala yote ya utumishi katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti haya licha ya wapiganaji kupendekeza utaratibu wa kusimamia maslahi yao Kikatiba.

19. Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi itakayokuwa na jukumu la kusimamia utumishi wa Jeshi la Polisi. Katika
 
Back
Top Bottom