Mitandao ya simu: Kuna nini nyuma ya pazia?

Mitandao ya simu: Kuna nini nyuma ya pazia?

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
26,634
Reaction score
38,245
Vodacom pamoja na Tigo Leo wameshangaza Watanzania, hii ni baada ya kupunguza muda wa maongezi pamoja na MB. Bado hawajaweka bayana nini kinachoendelea chini ya kapeti tumesubiri hata kutumiwa ujumbe ila hakuna kitu.
==================

attachment.php


Tunakoelekea sasa ni zaidi ya ubeberu! Mtandao wa Airtel niliokuwa nautegemea sasa na wao wameamua kupunguza vifurushi vyao.

Awali, kifurushi;

- Tshs 399 dk 5+ 50sms na mb 15
- Tsh 499 unapata dk 10 sms 300 na mb 75
- Tsh 599 dk 15+ 350sms mb 100
- Tsh 649 dk 17+ 450sms na mb 125
- Tsh 999 dk 25 +1000sms na mb 150

Sasa hivi;

- Kifurushi cha 399 hakipo,
- Tsh 499 unapata dk 9 sms 300 mb 10
- Tsh 699 dk 24 +1000sms na mb 10
- Tsh 999 dk 24+1000sms na mb 10

Tunakoelekea hii nchi sio sasa!

Hii ndo habari vodacom wametoa;

WATANZANIA WAENDELEA KUNUFAIKA NA MAWASILIANO YA GHARAMA NAFUU

-Watanzania waendelea kunufaika na gharama nafuu za mawasiliano
-Nchi nyingine kama Kenya,Afrika Kusini,Ghana,Nigeria na India viwango viko juu.
10985047_941000649257651_7693680316028543952_n.jpg

Watanzania wanaotumia huduma za mawasiliano bado wanaendelea kupata huduma hizo kwa gharama nafuu kwa kupiga simu na matumizi ya interneti ukilinganisha na huduma zinazotozwa kupata mawasiliano katika nchi nyingine za Afrika ikiwemo Afrika ya Kusini,Kenya,Nigeria na hata nchi ya india.


Haya yaemebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza,katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo alitoa mfano kuwa licha ya ongezeko la bei katika vifurushi vya kupata huduma mawasiliano bado katika kifurushi cha gharama ya chini ambayo ni shilingi 500 mteja anaweza kupata MB za kutosha kutumia internet ikiwemo kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS).

Alitoa mfano kuwa mteja akinunua kifurushi cha shilingi 500,kati ya hizo fedha shilingi 138 inakwenda serikalini kwa ajili ya kodi na kampuni kubakia na shilingi 362/- ambapo fedha hizo zinamuwezesha kupata muda wa dakika 15 za maongezi ikiwa kila dakika inatozwa shilingi 24/-,MB za kuperuzi internet 8 kila MB ikiwa inatozwa shilingi 5 na kutuma ujumbe wa maneno (SMS) 250 ambapo kila ujumbe natozwa shilingi 0.12

"Viwango vya malipo kwa Vodacom ni vya gharama nafuu na vimepangwa kulingana na mahitaji ya wateja wetu licha ya mabadiliko madogo katika bei yaliyofanywa hivi karibuni.Hivi sasa tunatoza shilingi 4.9/-kwa kila MB katika kifurushi cha GB5 ambapo bei ya awali kilikuwa kinatozwa shilingi 3.9/-.

Bado malipo ya sasa ni madogo ukilinganisha na mallipo yanayotozwa kwenye kifurushi cha GB5 kwenye soko la huduma za mawasiliano kwa fedha za kitanzania kwa mfano Nigeria inatoza shilingi 17/-/Afrika ya Kusini Shilingi 13/-,Kenya shilingi 12/-,Ghana shilingi 7/-na India shilingi 5/-


Meza pia alielezea mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na kampuni ya Vodacom katika kipindi cha mwaka 2014 amabpo aliwashukuru wateja wote kuwa wamechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mafanikio hayo ikiwemo zaidi ya wateja 1.7 kujiunga na familia ya Vodacom.

Pia alisema kuna ongezeko la wateja wanaoendelea kufaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa na Vodacom ikiwemo huduma ya internet ya gharama nafuu na huduma nyinginezo kama vile M-Pesa ambayo imekuwa na mafanikio kwa kuwa na mtandao wa mawakala 85,000 na kufanya mihamala inayofikia Trioni 1.2 kwa mwaka pia huduma ya M-Pawa imekuwa kwa kasi na inawawezesha wateja wengi kuweka pesa na kukopa.Pia aliongeza kuwa kampuni imeongoza kwa kuwa ya pili kulipa na kukusanya kodi za serikali na kuwa ya kwanza katika sekta ya mawasiliano.

Alisema kwa mwaka jana kampuni iliweza kuwekeza shilingi bilioni 180/- na mwaka huu itawekeza shilingi bilioni 140/- katika kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya internet na kusambaza huduma bora kwa wateja nchini kote.

Alimalizia kwa kusema kuwa moja ya dhamira ya kampuni ni kuunga mkono juhudi za kusambaza huduma nchini kote hususani sehemu za vijijini ambapo katika kuunga mkono jitihada hizi kampuni imekuwa ikichangia fedha kwenye mfuko wa kusambaza huduma za mawasiliano vijijini ujulikanao kama UCAF.
 

Attachments

  • Makamba.png
    Makamba.png
    25.1 KB · Views: 17,892
majambawazi hao halafu january makamba anautaka urais wakati kashindwa kudhibiti ushenzi huo wa mitandao nchini
 
Baada ya kuona hatukomi kwa kutuibia kwa kipindi kirefu, leo voda wameimarisha wizi wao baada ya kuondoa kifurushi cha 250 na 400 ambacho kilikuwa nafuu sana kwa sisi walal hoi!

Sasa itabidi tujikamue zaidi kwa kununua kifurushi cha 500 dk 15 sms 250 na 8mb, badala ya dk 19 sms 250 na 50mb.

Kilio kwa wengi kitakuwa hapo kwenye MB maana hamna kifurushi chenye MB zaidi ya 8.

Mb 8 ni chache sana jaman wenye smart phones itabidi muongeze bajeti. Huu ni wizi mwingine kama ule wa escrow!!


Mnan'ang'ania vodacom wanini wakati airtel wana super internet speed na viwango nafuu Sana vya data?

Mfano ukinunua vocha ya 500 yakujiunga moja kwa moja unapata 15 minutes kwenda mitandao yote SMS 300 na 125 Mb.....


Cha buku unapata 30 minutes to all networks 1000sms na. 300 mb

kuna vifurushi unajiunga kwa kupiga *149*81# ni very cheap mnahangaika na hao makabaila wanini?

Nimehamia airtel siku nyingi nainjoi maisha achana na wahuni hao.....
 
Kama n hivyo ngoja nkanunue airtel tu hawa watu hawana huruma na sisi kabsaaaaaaaaaa
 
AIRTEL BABA LAO,cha wiki sh 2000 utatumia mpaka uchoke
 
Mnalalamika Nini kwani mmefungwa Vichwa ,si kuna mitandao mingi tu yrnyr huduma mnazozitaka ni nn kinawanyima kuhama .

1. Tigo

2. Airtell

3. Zantel

4. Smart .

mingi tuu ..hakuna haja ya kuita watu wezi ,hayo ni mazungumzo na makubalianonya kampuni
 
Ww maamuzi yako unataka yawe maamuzi ya watu wanaomiliki kampuni ,acheni kufanya harakati mpaka kwnye makampu ya wetu ,kama walichokifanya ninkibaya basi ndio kasoro yao na ndicho kinawapa makampuninmengine fursa ya Kufanya vizuri .
 
Ni majanga..mleta mada tunashukuru sana kwa kututarifu. cheka time ya wiki iliyokua ni dak 105 sasa hvi niv dak 85.
 
Mnan'ang'ania vodacom wanini wakati airtel wana super internet speed na viwango nafuu Sana vya data?

Mfano ukinunua vocha ya 500 yakujiunga moja kwa moja unapata 15 minutes kwenda mitandao yote SMS 300 na 125 Mb.....


Cha buku unapata 30 minutes to all networks 1000sms na. 300 mb

kuna vifurushi unajiunga kwa kupiga *149*81# ni very cheap mnahangaika na hao makabaila wanini?

Nimehamia airtel siku nyingi nainjoi maisha achana na wahuni hao.....

Mpea umeongea points nna miezi sita nimehamia airtel na sijutii yani wako vizuri mno Voda ni kwa m pesa tu na kwa kua airtel kwenye money transaction wanazingua ila natafuta simu niweke tigo niwahame voda siwezi kuitupa maana ndo inatambulika ila VIFURUSHI VYA VODA NI MAJANGAA.
 
baada ya kuona hatukomi kwa kutuibia kwa kipindi kirefu, leo voda wameimarisha wizi wao baada ya kuondoa kifurushi cha 250 na 400 ambacho kilikuwa nafuu sana kwa sisi walal hoi!

Sasa itabidi tujikamue zaidi kwa kununua kifurushi cha 500 dk 15 sms 250 na 8mb, badala ya dk 19 sms 250 na 50mb.

Kilio kwa wengi kitakuwa hapo kwenye mb maana hamna kifurushi chenye mb zaidi ya 8.

Mb 8 ni chache sana jaman wenye smart phones itabidi muongeze bajeti. Huu ni wizi mwingine kama ule wa escrow!!

hamia tigo
 
Back
Top Bottom