Mitandao jamii ni salama kweli ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitandao jamii ni salama kweli ?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Aug 2, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 2, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kama wewe ni mtembeleaji wa Tovuti kama Facebook pamoja na Hi5 utakuwa umeona baadhi ya vijimambo vinavyoendelea katika tovuti hivyo , mfano unapojiunga na tovuti hizo inakuwa na sehemu maalumu ambayo inakuwezesha wewe kujiunga na account yako ya yahoo au google ili uweze kualika marafiki zako wengine waliokuwa katika contacts zako za hiyo yahoo mail au google unapojiunga pale na kweli rafiki zako hao wote watapata hiyo mialiko yako na wengi watakuja kujiunga na wewe kama ni facebook au hi5 au tanged huu ndio ulimwengu wa sasa ambapo kumtafuta mtu wakati mwingine ni rahisi zaidi kuliko anavyofikiria ukiingia katika tovuti hizo za kijamii unaweza kumtafuta mtu huyo kama ameweka taarifa zake sahihi .

  Wakati ambapo mashirika mengi ya kijasusi duniani yakitumia mitandao hii ya kijamii kwa ajili ya taarifa zao za kila siku , kama kujua Fulani anayetumia jina Fulani yuko wapi na anafanya nini au anawasiliana na nani ameweka tarifa gani katika account yake ya facebook au hi5 na ndio magenge mengi ya kihalifu pia yanatafuta watu wa kushirikiana nao katika uhalifu wao katika nchi kadhaa duniani , wengi wanatumika bila wao kujua au kwa kujua ingawa takwimu zinaonyesha wengi wanaingizwa bila wao kujua kama wanatumika katika uhalifu wa aina Fulani .

  Unapopata barua pepe kutoka facebook ambayo inatakiwa kuja kwako moja kwa moja inaingia katika sanduku la barua pepe yako kama ni yahoo au hotmail , unapotaka kuangalia ujumbe huo inakufungulia katika window nyingine au tab nyingine inategemea wewe unavyotaka lakini mara nyingi huwa zinafungua moja kwa moja pamoja na password yako , hii ina maanisha kama ulikuwa sehemu ambayo mtandao unaenda taratibu ukaamua kuondoka zako ukaacha kazi zako hapo mwingine anaweza kuja kukaa katika computer hiyo na kufungua kile ulichotaka kufungua wewe na kufanya kazi zake au na kufanya uharibifu hata kwenye profile yako kama alikuwa na nia hiyo mbaya .


  Katika makala yangu mmoja kuhusu usalama wa mitandao ya mawasiliano haya niliwahi kusema vyombo vyetu vya usalama viwe na watu maalumu ambao wanawaweka katika mitandao hii kwa ajili ya kufanya kazi maalumu nayo ni kujiunga katika vikundi mbali mbali katika mitandao hii kwa ajili ya kupata taarifa na kujua watu wengi zaidi katika dira mbali mbali za kujenga au za kubomoa jamii mbalimbali

  Kuna jambo ambalo niliwahi kuhisi huko nyuma kwamba inawezekana kabisa huu wizi katika ATM inawezekana mawasiliano kati ya wahalifu hawa yanafanyika kwa njia ya mitandao hii jamii na sio kwa njia ya barua pepe za kawaida ambazo watu wamezoea , mimi sio mtaalamu sana katika mawasiliano ya Barua pepe lakini unapotumia barua pepe ni rahisi zaidi mtu kuweza kukubamba kuliko unavyofanya mawasiliano kwa njia ya mitandao jamii kama facebook au hi5 .

  Mwaka jana katika moja ya Somo langu niliwahi kufanya utafiti kuhusu watu na tabia zao wanapotumia mitandao hii , imeonyesha kwamba unapojiingiza katika mitandao jamii hii ni rahisi sana kuweza kujua tabia za watu haswa zilizojificha na hata kujua vitu anavyopenda yeye haswa kama unatumia jinsia bandia haswa za kike wahalifu wengi wa naigeria wanatumia jinsia za kike ingawa wao ni midume na kwa njia hiyo wamefanikiwa kulaghai wengi sana haswa wanaopenda mijimama ya kizungu au wale wanaopenda safari za ulaya ua njia rahisi za kujipatia kipato

  Ukiacha facebook na hi5 kwa sasa kuna mwingine umekuja kwa kasi sana nao ni twiter , mitandao hii haswa twiter inaonyesha inaweza kufunika kabisa shuguli za blogu na forums zingine huko mbeleni kama forum hizi na blogu hizi hazijajiimarisha zaidi kibiashara na kuwa na vitu vya kibunifu zaidi kuliko ilivyo sasa hivi , nafikiri kinachoweza kufanyika zaidi ni kwa kampuni kubwa katika google kununua zinazochipukia kama twitter , au tanged pamoja na tovuti zingine zinazotoa huduma za mawasiliano na vikundi vya kijamii .

  Leo jioni nilikuwa naangalia uwezo mbali mbali wa Browser mbali mbali katika masuala ya usalama wa mtumiaji , nikawa natumia browser ya chrome ambayo ni mali ya google , nilipomaliza kazi zangu nikaifunga kabisa na kuzima computer nilipoiwasha tena nikafungua chrome yangu ikanifungulia links za tovuti ambazo nilikuwa naangalia mara ya mwisho hii ina maanisha kwamba kama inatumika kwenye internet café mfano ni rahisi sana kwa mhalifu kuweka target ya kufanya uhalifu Fulani kuweze kujua Fulani ametembelea tovuti zipi mwishoni , kama mtu hujui cha kufanya basi unaweza kuliwa .

  Kuna tatizo lingine pia nimeliona nalo ni kwa antivirus kutokutambua pale ambapo nilipofungua chrome tena , nafikiri ilitakiwa kuniuliza kama zile ni kazi zangu au la , kama kweli ni zangu basi niendele na nilichokuwa nafanya , najua katika Norton Internet Security inasehemu ya kuweka password kuweza kulock tovuti zote unazotembelea kwahiyo pindi mtu mwingine akija basi hawezi kuangalia ulichokuwa unafanya wewe kama uliweka password hiyo kwa bidhaa zingine huwezi kufanya hivyo tatizo la hii pia ni mpaka uwe na hiyo Norton halafu sasa uiambie ifanye hivyo .

  Ni hilo tu kwa leo , kwahiyo ndugu unapotumia hizi browser za mitandao haswa katika internet café uwe makini sana uangalie kama unaacha chochote kama reference katika browser catch za computer hizo , uhalifu mwingi sana katika mitandao siku hizi unafanyika kwa watu kuacha reference hizo ambazo wengine wanaweza kuzitumia kushambulia sehemu zingine au hata kuweza kukushambulia wewe binafsi

  Kwahiyo huko makazini mwetu tunapofanya kazi pia hakikisha huachi reference ukiacha mashambulizi hayo , hata documents nyingi nyeti zinaibiwa kwa njia hii au ambazo zinahusiana na hizi , kama unavyoona hapo uhusiano wa mtu anapotumia mitandao hiyo jamii halafu mwisho inavyokuja kujihifadhi katika catch ya browser yake ya chrome hapo anakuwa amepatikana kwa kiasi kikubwa

  Naamini kwa kiasi kikubwa watengenezaji wa browser sasa wanafanya jitihada za dhati kuimarisha usalama wa mitandao hii haswa kwa watu ambao wanatumia mitandao hii kwa ajili ya shuguli zao nyeti , ingawa jitihada zao haziwezi kuzaa matunda kama hawashirikiani na watengenezaji wa antivirus pamoja na watumiaji wengine ambao wanaandika kwa njia ya maandishi kama sisi .

  Kuna mengi ya kuandika ila kwa leo nitaishia hapa ,

  USIKU MWEMA
   
 2. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mkuu Shy, heshima mbele.

  Mitandao jamii inazidi kukua kila kukicha na itaendelea kushamiri siku zinavyosogea mbele.

  Mitandao hii inajumuisha watu wa rika mbalimbali na ndipo tunaona hata mitandao mingine inakuwa maarufu kuliko mingine.

  Mitandao kama Facebook, MySpace au Hi5 imekuwa maarufu kutokana na kuwa na wanachama wenye rika tangu watoto hadi watu wazima.

  Hata Ughaibuni mashirika ya kijasusi kam M15 na M16 ya Uingereza, FBI na CIA ya Marekani na mengine, yametumia mwanya wa uwazi wa kimawazo wa wamitandao jamii kuchagua wanafunzi wazuri kwa kuangalia na kusoma "profiles" za wanachama.

  Kisheria mitandao jamii au SNS(Social Networking Sites) ina wajibu wa kulinda siri za watumiaji hasa wanachama hata kama wenye mitandao hio wapo nje ya bara la Ulaya kwa mfano. Mkazo wa kauli hii unatiliwa zaidi kwa kuzingatia kwamba watumiaji wa mitandao hii hawawezi kukwepa sheria kwa sababu tu watumiaji wanatengeneza "content" na ku-post mtandaoni kwa sababu wao ni "data controllers".

  Wale wenye mitandao jamii wana-process data za watumiaji na kusaidia shughuli zote za registration na deletion za accounts za watumiaji.

  Pia hawa SNS providers wanaangalia matumizi ya mtumiaji kwa minajili ya kufanya matangazo na shughuli za masoko wakiwemo third parties.

  Lakini pia tusisahau kwamba watumiaji wa mitandao jamii wana wajibu wa kuwa na "duty of care". Mfano unaweza kuwa kwa kuangalia sheria au kanuni ambazo zimewekwa na jamii forums hapa.

  Pia wewe kama mtumiaji makini utaona kwamba unawajibu wa kuhakikisha kwamba unazitumia vizuri "settings" ambazo mwenye mtandao jamii anakuwa amekupa kuzifanya ili kuwa "protected". Mfano unaweza kusema kwamba hupendi "contacts" zako ziwe wazi kwa public bali kwa wale walio katika network yako tu.

  Kwa hio mawazo yako kuhusu "doubts" ulizo nazo kuhusu mitandao jamii zinaweza kuwa sawa kulingana na uelewa wako kuhusu uendeshaji wa mitandao jamii hii.

  Lakini tuendelee tu kuelimishana.
   
  Last edited: Aug 5, 2009
Loading...