Mitandao isitumike kumchafua Rais

ukiona watu wenye akili na taaluma zao wanatumia mda wao kujadili maisha binafsi ya viongozi ujue wanatakiwa kulazwa I.C.U MIREMBE
 
Hapa mhariri naye anajipendekeza tu kwa JK! Mbona kuna mambo mengi yanajadiliwa humu kuhusu utendaje mbovu wa Kikwete na hasemi? Suala la madaktari mpaka leo hajasema lolote hadi leo na watu wamelijadili humu mbona huyo mhariri hasemi? Kuchafuliwa kwa Kikwete ni kutokana na utendaje wake mbovu na wala si vinginevyo? Kama JK angekuwa kiongozi imara, mwenye kufanya maamuzi sahihi na ya haraka kwenye mambo muhiimu ya nchi tusingeshuhudia yeye kuhusishwa na matokeo mabaya ya mtoto wake Mwanaasha!! All in all inakera sana wahariri kama huyu wa Tanzania daima kujipendekeza kwa JK!
 
kama kweli wote tulipitia posts baada ya tukio matokeo ya mwanaasha tunakubaliana kwamba mjadala ulihama kutoka kwa mtoto kwenda kwa baba.

Baba anapimwa kwa mafanikio ya familia yake. haya sasa Riz 1 kashakuwa fisadi, Mwanaasha kalamba IV. tuna baba kweli hapa?? Je ataweza kulea watoto wa wenzie kweli (akina Kayumba)???
 
Kwa nguvu aliyokuwa nayo KIKWETE kama familia yake ingemzuia kugombea Urais mwaka 2005, asilimia 99 ya watanzania wangeandamana kuishinikiza!
 
kikwete ni kiongozi anaeishi maisha ya wananchi wake.yeye mwnyw amesoma shule za humu humu,kazi ameanzia vijijini tena singida watoto wake ndio hao wanasoma ktk shule hizi hizi za yebo yebo.hawa wenye gubu wanaoropoka humu hawana uzalendo.
 
FEZA Academy shule ya yebo yebo? Kamuzu Academy shule ya yebo yebo?
 
Uchafu ni uchafu ili uwe msafi lazima uuchukie . Tumsipomchafua ataogaje
 
Baba anapimwa kwa mafanikio ya familia yake. haya sasa Riz 1 kashakuwa fisadi, Mwanaasha kalamba IV. tuna baba kweli hapa?? Je ataweza kulea watoto wa wenzie kweli (akina Kayumba)???

huna hoja..watoto wa nyerere akina makongoro walikuwa walevi wa gongo arusha lakini nyerere alibaki na msimamo na uzalendo wake adi leo tunamkumbuka kwa mazuri yake,hatuangalii watoto.
 
Mtoto akifanya vizuri kwenye jambo lolote mzazi huwa anasifiwa pia mtoto akiwa mchafu mzazi ndo wa kwanza kulaumiwa kwa kushindwa kumtunza vizuri
 
FEZA Academy shule ya yebo yebo? Kamuzu Academy shule ya yebo yebo?

By Rais wa migomo

kikwete ni kiongozi anaeishi maisha ya wananchi wake.yeye mwnyw amesoma shule za humu humu,kazi ameanzia vijijini tena singida watoto wake ndio hao wanasoma ktk shule hizi hizi za yebo yebo.hawa wenye gubu wanaoropoka humu hawana uzalendo.

Rais wa migomo kila nikitafakari post zako nashindwa kukuelewa. huyo Mwanaasha wala hayupo tena TZ. Alipomaliza hiyo form four alipelekwa ughaibuni. sasa uzalendo upi unaouzungumzia wewe? Hiyo FEZA ni shule ya kata??????
 
huna hoja..watoto wa nyerere akina makongoro walikuwa walevi wa gongo arusha lakini nyerere alibaki na msimamo na uzalendo wake adi leo tunamkumbuka kwa mazuri yake,hatuangalii watoto.

Hapo kwenye red kuna walakini. Huwezi kumbuka mtu kwa mazuri yake tu. Hata Adam na Eva walikuwa na mabaya yao na ndo mwishowe tunaenda motoni kwa ajili yao (kwa imani). Nyerere alikuwa na mabaya yake pia. Fikiria kwa kutumia medula oblangata mkuu
 
Mkuu, nakubaliana kwa kiasi kikubwa na hoja ulizotoa. Ila baraza/wizara waangalie na upande wa pili wa trauma these children are going through (nina maana watoto waliofeli). Kuna wengine wanafikiria hata kujitundika, etc.
 
FEZA Academy shule ya yebo yebo? Kamuzu Academy shule ya yebo yebo?

unazifananisha hizo na zile za nje ya nchi ambazo baba yako amesoma akakusomesha na ww?be critical mama ww usiropoke
 
ukiona watu wenye akili na taaluma zao wanatumia mda wao kujadili maisha binafsi ya viongozi ujue wanatakiwa kulazwa I.C.U MIREMBE

Ukishakuwa Raisi wa Nchi, huna maisha binafsi na ndio maana popote anapokuwa lazima TISS wawepo. si tungekuwa tunakutana naye baa na disco kama zamani. Lolote afanyalo now linakuwa la kitaifa maana ndo mkuu wa taifa. Angalia hata kwa wenzetu, hata kama ulikuwa na kimada miaka 20 iliyopita, inaweza kuku cost usiukwae uraisi. Mh kwani ya Clinton umeisahau mkuu?? Au hujui siasa nini?
 
Sidhani kama ni kumchafua, maana kama ni usafi mtoto wake angesoma Lugoba Secondary School au shule nyingine ya kata kama kweli ni uzalendo. Lakini mtoto anayefeli akisoma kwa WATURUKI wanoonekana kuendesha shule vizuri, ujinga ni pale mzazi anaposhindwa kuangalia mwenendo wa masomo wa mtoto wake na kuchukua hatua. Wenye matokeo yake ya kidato cha pili watusaidie. Lakini pili wasingemfukuza wakati asipotimiza wastani na sera ya JK ni kutokuwa na wastani katika darasa lolote hadi chuo kikuu. Kukamatwa kumefutwa na hakuna haja ya kudesa pia!!

Pili hivi ni mtoto wa Salma Kikwete au...? Simchafui naulizia!
 
Naona unataka kuleta mambo ya SOPA na PIPA hapa nchini wakati dunia nzima inapinga system hizo. Na we hebu jiulize 'ni kwanini anajadiliwa?'
 
ukiona watu wenye akili na taaluma zao wanatumia mda wao kujadili maisha binafsi ya viongozi ujue wanatakiwa kulazwa I.C.U MIREMBE

At least umejua tuna akili na taaluma zetu, kwa hiyo ujinga wako si tatizo sana. Lipo jambo moja tu ndio hulijui; mpk hapo na wewe unatujadili sisi badala ya mada
 
Mkuu, nakubaliana kwa kiasi kikubwa na hoja ulizotoa. Ila baraza/wizara waangalie na upande wa pili wa trauma these children are going through (nina maana watoto waliofeli). Kuna wengine wanafikiria hata kujitundika, etc.

Mimi huwa nafikiria kujitundika naposikia Lowasa na Chenge wakishirikiana na Karamagi wamechukua majipesa ya nchi na kuweka kwenye akaunti zao za nje. Naomba ukataze na hilo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…