nyabhingi
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 15,515
- 20,005
Kama kweli nyie wazalendo basi mjue kuna zaidi ya Dowans inanitia shaka nadhani kuna kitu kwenye hii Dowans ndio maana ikitajwa wote mnaruka uwiiiii, jamani tumevamiwa na longo longo jingiiiii hamjengi haja za msingi kwanini Dowans isiwasheshwe. Pengine hamfahamu kuwa IPTL yenye mkataba wa miaka 20 ndio ni kampuni ya kufua umeme ghali maradufu ya Dowans mbona yenyewe mmeinyamazia? au yenyewe haikuingia mkataba na tenesco kwa kutumia hila? Sisi wananchi lazima tuwe na upeo wa kujiuliza mambo tusikurupushwe na wanasiasa kisha tukawa tunaitikia viitikio vyao.
Umeme wa Dowans lazima uwashwe ili kuwapunguzia makali wananchi! utasaidia kuongeza production viwandani! sioni tatizo la kuwashwa mitambo ya Dowans ikiwa maslahi ya taifa yataangaliwa upya katika huo mkataba mpya. Sitapenda kulalama na kuropoka mpaka pale nitakapojua IPTL, AGGREKO na SONGAS WASAFI kiasi gani.......
My take.
Tuache ushabiki wa kishamba tuchambue hoja ili kujenga hoja...............
IPTL iliingia wakati kikwete ni waziri wa nishati,DOWANS akiwa rais alafu mmiliki wake ni rafiki yake wa karibu na shemeji yake..connect the dots,.kama ulikuwa unajaribu kumdefend kikwete..umeshindwa,..kwani hatuwezi kukodisha mitambo mingine zaidi ya hii yenye utata,..hivi wewe hunusi ufisadi hapa??