Mitambo ya Dowans sasa kuwashwa - Waziri Mkuu Pinda

Mimi nashangaa hii serikali ya SISIEMU inamwogopa nani. Huo ni uozo kuingia mkataba na kampuni feki. Uhalali wa Dowans sasa hivi unatoka wapi? Serikali inatakiwa kuitafisha ile mitambo kisha iwashwe. Hata kama Dowans wataenda mahakamani wananchi watakuwa wameshapata nafuu.
Kama serikali iliwahi ku-deal na kesi za uhujumu nchini before, kinawashinda nini kutaifisha hii mitambo ya kitapeli?
Kuingia mkataba mwingine na dowans ni kuwahalalisha from Fake to legitimate company. Na kamwe dowans haiwezi kuwa kampuni HALALI.
 
Tena hao wanaoishi majuu ndio hovyo kabisa mie siwaelewi eti tatizo lao ni nani mmiliki wa Dowans kwanini hawataki kujua wamilikiwa wa IPTL, Songas, Aggreko na Tanpower? Ukiwauliza kwanini Dowans wanatutoza capacity charge mil 152 na IPTL mil 300 halafu tunataka kumjua mwenye 5owans hatutaki kumfahamu IPTL mwenye mkataba wa miaka 20 wataikwepa hiyo hoja! Agrrrrr nimechoka kama u great thinker wenyewe ndio uko hivi!


Zamani katika baadhi ya makibila ya kiafrika mtemi akifa huwa alikuwa anazikwa na vijana wawili walio hai kuipakata maiti yake, na vijana hawa walikuwa wanajitolea kama mashujaa, ni bahati mbaya sana sijasikia wala kusoma majina ya waliodhani kufanya hivyo ni ushujaa kwenye historia tunasikiatu, Mtemi Isike, Mirambo n.k.hakika ulikuwa ni ujinga si ushujaa. Sasa wewe nakuona kama mmoja wa hao vijana ambaye anaishi enzi hizi. Hivi nikuulize kwanini usione Dowans ni kama starting point ya kuelekea kuuliza hayo mengine. Maana ya dowans yako wazi hata juha anaona hapa kuna walakini.
 
kama ni kweli nampongeza sana waziri mkuu maana hasara ambayo tumepata kwa sababu za kipuuzi ni kubwa.mitambo iwashe na madai yaendelee maana hakuna kinachomtegema mwenzake.
 
[QUOTE= mfanyabiashara mwingine mkubwa anunue mitambo ya Dowans na aingie kwenye mkataba wa muda mrefu na TANESCO wa kuzalisha umeme Bila shaka huyo atakuwa RA
 
We`re negotiating on switching on the Dowans power generation plant``

Dowawnsmitambo.jpg

Dowans power plant


Top management of Tanzania Electric Supply Company Limited (Tanesco) said yesterday it has received no letter from Dowans on the latter's intention to forgive the compensation award.
"Talks on the 94bn/- compensation offer are yet to start because we have not received any letter from Dowans on the subject," said Tanesco Managing Director William Mhando in an exclusive interview with The Guardian yesterday.

The latest statement by Tanesco's top official runs contra to the call by the Parliamentary Energy and Mineral watchdog on the power firm to respond to the Dowans offer.
Dowans said in a statement recently that it has already written to Tanesco expressing its intention to forgive the 94bn/- compensation.

In its verdict in November last year, the International Chamber of Commerce (ICC) ruled that Tanesco should pay Dowans the hefty amount for breach of contract between the two.
The decision has since then provoked a series of heated debates in both public and private circles, with many Tanzanians saying the penalty was unjustified.

Speaking to journalists recently during a tour by the Parliamentary Energy and Minerals Committee of the International Power Tanzania Limited (IPTL), Dowans finance director Stanley Munai said: "We have written to Tanesco regarding our intention to forgive the 94bn/- compensation, but the latter seems reluctant to accept the offer… they have yet to reply to our letter."
However, Tanesco managing director said the state-run firm is yet to receive the said letter from Dowans.

"It's good that you got Dowans version of the (compensation) story and contacted us for confirmation…let me insist that we have not received an official letter from them that they are forgiving the debt. There are no talks going on regarding the matter," Mhando said.

"So, what you heard or saw in the media is totally untrue…how could we dare refuse an offer?" Tanesco chief wondered without giving details.
Mhando, however said the two parties have started negotiations on switching on the power generation plant owned by Dowans.

This is seen as a strategic move by power stakeholders, industrialists, investors and ordinary people to mitigate the negative impact of the country's power crisis.
The question whether or not the Dowans power generation plant should be switched on would be determined by the outcome of the ongoing talks and the subsequent signing of the agreement.
"We may or may not sign a contract with Dowans to switch on the plant…but all this including the payment modalities would be decided by the talks. The public would be informed on the outcome today or tomorrow," he said.

In his statement last week, Dowans finance director said the private power firm reached the decision to forgive the 94bn/-, following outcries by Tanzanians, but wants Tanesco to only pay USD24m being services-related debts.
When reached for comment, The Parliamentary Energy and Minerals Committee chairman, January Makamba said the fact that Dowans had communicated, in writing with Tanesco on the 94bn/- offer was "public knowledge."

"But if Tanesco managing director says he has not received the letter, then that is something else…I have no comment on that. However, I am still of the view that the offer is a good opportunity," he said, adding: "We agreed that Tanesco should be the main speaker on this controversy."



SOURCE: THE GUARDIAN
 
Tena hao wanaoishi majuu ndio hovyo kabisa mie siwaelewi eti tatizo lao ni nani mmiliki wa Dowans kwanini hawataki kujua wamilikiwa wa IPTL, Songas, Aggreko na Tanpower? Ukiwauliza kwanini Dowans wanatutoza capacity charge mil 152 na IPTL mil 300 halafu tunataka kumjua mwenye 5owans hatutaki kumfahamu IPTL mwenye mkataba wa miaka 20 wataikwepa hiyo hoja! Agrrrrr nimechoka kama u great thinker wenyewe ndio uko hivi!

Shossi, Kitu ninachokupendea ni kuwa huwa unasimamia hoja zako kwa kile unachokiamini.Kudos! Ninaiona hoja yako tena kwa mantiki. La muhimu ujibu hoja za wenzako kwa mantiki pia. Comrade, punguza jazba! mara nyingi inaficha hoja zako nzito (ushauri). Mathalani unaposema hao wanaoishi majuu ni Hovyo! mhh, sijui sehemu anayoishi mtu inahusiana vipi na hoja. Kwahiyo wale wanaoishi uwanja wa fisi, au mimi ninayeishi Dongobeshi na shopping yangu ni Loliondo utasikiliza hoja zetu kweli!
 
Kama kweli nyie wazalendo basi mjue kuna zaidi ya Dowans inanitia shaka nadhani kuna kitu kwenye hii Dowans ndio maana ikitajwa wote mnaruka uwiiiii, jamani tumevamiwa na longo longo jingiiiii hamjengi haja za msingi kwanini Dowans isiwasheshwe. Pengine hamfahamu kuwa IPTL yenye mkataba wa miaka 20 ndio ni kampuni ya kufua umeme ghali maradufu ya Dowans mbona yenyewe mmeinyamazia? au yenyewe haikuingia mkataba na tenesco kwa kutumia hila? Sisi wananchi lazima tuwe na upeo wa kujiuliza mambo tusikurupushwe na wanasiasa kisha tukawa tunaitikia viitikio vyao.

Umeme wa Dowans lazima uwashwe ili kuwapunguzia makali wananchi! utasaidia kuongeza production viwandani! sioni tatizo la kuwashwa mitambo ya Dowans ikiwa maslahi ya taifa yataangaliwa upya katika huo mkataba mpya. Sitapenda kulalama na kuropoka mpaka pale nitakapojua IPTL, AGGREKO na SONGAS WASAFI kiasi gani.......

My take.

Tuache ushabiki wa kishamba tuchambue hoja ili kujenga hoja...............

hawana hoja tatizo KANZU maagizo ya hekaluni tumewastukia
 
Kama kweli nyie wazalendo basi mjue kuna zaidi ya Dowans inanitia shaka nadhani kuna kitu kwenye hii Dowans ndio maana ikitajwa wote mnaruka uwiiiii, jamani tumevamiwa na longo longo jingiiiii hamjengi haja za msingi kwanini Dowans isiwasheshwe. Pengine hamfahamu kuwa IPTL yenye mkataba wa miaka 20 ndio ni kampuni ya kufua umeme ghali maradufu ya Dowans mbona yenyewe mmeinyamazia? au yenyewe haikuingia mkataba na tenesco kwa kutumia hila? Sisi wananchi lazima tuwe na upeo wa kujiuliza mambo tusikurupushwe na wanasiasa kisha tukawa tunaitikia viitikio vyao.

Umeme wa Dowans lazima uwashwe ili kuwapunguzia makali wananchi! utasaidia kuongeza production viwandani! sioni tatizo la kuwashwa mitambo ya Dowans ikiwa maslahi ya taifa yataangaliwa upya katika huo mkataba mpya. Sitapenda kulalama na kuropoka mpaka pale nitakapojua IPTL, AGGREKO na SONGAS WASAFI kiasi gani.......

My take.

Tuache ushabiki wa kishamba tuchambue hoja ili kujenga hoja...............

hawana hoja tatizo KANZU maagizo ya hekaluni tumewastukia
 
Hawajui wananchi wa
kishachukua nchi hizo pesa za ufisadi zitakuwa frozen baada ya revolution?Hata assets zao zitakuwa frozen kwasababu ni jasho la wananchi,hawa watu hawajui dunia imebadilika...Yani very out of touch,they dont connect with the people for they dont live the same world!

Wanadhani wananchi bado ni wajinga,nani alisema mitambo ya Dowans haiwashiki?We both knew that mitambo ya Dowans ni mizima na kuna watu miongoni mwao baadhi ya wanasiasa wetu ambao wanataka mitambi hiyo iwashwe,si kwasababu wanauchungu na shida ya watanzania bali ether wametumwa na wenye mitambo hiyo ama wana maslahi na uwashwaji wa mitambo hiyo,tatizo si mitambo,bali tatizo ni uwazi wa mikataba ya mitambo hiyo ambayo iliwahi kumilikiwa na kampuni hewa!

watawala watumie akili kwasababu wananchi wanataka uwajibishwaji wa viongozi wote ambao wamelisababishia Taifa hasara kutokana na mikataba hiyo,wananchi wanajua mitambo hiyo iko ila kabla haijawashwa,wanataka kujua itawacost kiasi gani,na pia kama wanatakiwa waendelee kulipa fidia za mitambo hiyo kuwa chini na wakati viongozi waliofanya hayo madudu bado wako madarakani na wengine ndio wenye kampuni,sasa ni kama wanatoa pesa mfuko wa kushoto na kuhamishia wa kulia.
Viongozi ambao ni wezi watakuwa wamejifunza yaliyotokea Tunisia,Egypt na sasa hivi Libya.Hawawezi kuweka pesa zao Europe or USA, sasa hivi watazipeleka Uarabuni au nchi kama Malaysia ambapo serikali zao hazijali.
 
Viongozi ambao ni wezi watakuwa wamejifunza yaliyotokea Tunisia,Egypt na sasa hivi Libya.Hawawezi kuweka pesa zao Europe or USA, sasa hivi watazipeleka Uarabuni au nchi kama Malaysia ambapo serikali zao hazijali.

Naona Bwana we unaelewa mambo yanavyo endeshwa na nyumba kwa mfano hizi za msoga zinazo ota kama uyoga kwenye kichuguu watazifanyaje? Au watazihamisha maana dunia ya sasa imeendelea bwana labda kumegunduliwa technologia ya kuibeaba nyumba na kuipeleka malaysia. Maana huwezi kunishawishi kuwa hizo si mali za kuwa frozen
 
Kama kweli nyie wazalendo basi mjue kuna zaidi ya Dowans inanitia shaka nadhani kuna kitu kwenye hii Dowans ndio maana ikitajwa wote mnaruka uwiiiii, jamani tumevamiwa na longo longo jingiiiii hamjengi haja za msingi kwanini Dowans isiwasheshwe. Pengine hamfahamu kuwa IPTL yenye mkataba wa miaka 20 ndio ni kampuni ya kufua umeme ghali maradufu ya Dowans mbona yenyewe mmeinyamazia? au yenyewe haikuingia mkataba na tenesco kwa kutumia hila? Sisi wananchi lazima tuwe na upeo wa
 
hawana hoja tatizo KANZU maagizo ya hekaluni tumewastukia

No! no! no Sir! This is not right. Shosshi has a point which need be examined. He says why dowans should be an issue if IPTL and SONGAS which we don't know the owners are siphoning the money! Whether he is right or wrong, we need to answer the core issue. I always say, people must refrain from injecting trivial matter to avert or dilute the meaning of the discussion. I asked Shosshi not to use ''majuu hovyo'' because it adulterates his point. Again, you should not use Kanzu or gauni to divert from the core issue. If you say Kanzu, what about wearing Lubega. Does lubega make me superior or inferior!!! What does Lubega has to do with current power crisis?
Ladies and Gentlemen,
It takes more to be a great thinker, not simple because one can cause Pandemonium, is ranting lot, or making tantrum with libel.
 
Tena hao wanaoishi majuu ndio hovyo kabisa mie siwaelewi eti tatizo lao ni nani mmiliki wa Dowans kwanini hawataki kujua wamilikiwa wa IPTL, Songas, Aggreko na Tanpower? Ukiwauliza kwanini Dowans wanatutoza capacity charge mil 152 na IPTL mil 300 halafu tunataka kumjua mwenye 5owans hatutaki kumfahamu IPTL mwenye mkataba wa miaka 20 wataikwepa hiyo hoja! Agrrrrr nimechoka kama u great thinker wenyewe ndio uko hivi!


Mkuu vipi tenaaaa!? Watanzania wanaoishi nje ndiyo HOVYO KABISA! Hawa ndiyo wanatuletea matatizo yote! kampuni iingie mkataba na Serikali kwa kuudanganya umma wa Watanzania kwamba ni kampuni toka Marekani na HQ iko Houston Texas. Wana uzoefu mkubwa wa kuzalisha umeme hivyo wanataka kuisaidia Tanzania ili iondokane na giza lililotanda nchi nzima.

Pamoja na wataalam wa TANESCO kuishauri Serikali kwamba kampuni hii haina utaalamu wowote wa kufua umeme na Watanzani walio Marekani kugundua kwamba hii kampuni iliudanganya umma wa Watanzania kuwa na HQ yake Marekani wakapewa mkataba walioshindwa kuzalisha hata tone la umeme.

Mkataba ulipovunjwa na TANESCO baada ya Richmond/Dowans kushindwa kutimiza makubaliano ya mkataba ule ukafanyika ufisadi wa kurithisha mkataba ule kwa Dowans (ndiyo wale wale Richmond lilibadilishwa jina tu ili kutuzuga Watanzania) katika mazingira yasiyoeleweka leo hii "mmiliki" wa Dowans anataka kuja kuwapora Watanzania walipa kodi $94 million, Watanzania walo nje wanyamaze tu wasitie neno lolote!

Nani alikwambia IPTL haikujadiliwa kwa kina na marefu hapa jukwaani na Watanzania mbali mbali katika kila kona ya dunia? Tafuta humu Mkuu utayaona majadiliano ya hali ya juu kuhusu utata wa mkataba mzima wa IPTL. Kwani wanaohoji kuhusu utata wa mmiliki wa Dowans ni Watanzania walio nje tu? Mbona hata walio ndani ya nchi nao wanafanya hivyo kwa idadi kubwa tu akiwemo Waziri Sitta?

Je unataka kuwaambia Watanzania walio nje wasishiriki katika mijadala yoyote inayohusu nchi yao kwa kuwa tu wako nje ya nchi? na pia siyo magreat thinker kama unavyodhani wewe? Tatizo hapa si Watanzania waishio nje bali ni mikataba haramu iliyofanywa kuanzia Richmond na sasa Dowans ambao unawafanya Watanzania wa ndani na nje ya nchi waliokwishachoshwa na ufisadi wa hali ya juu EPA $133 million, Meremeta $155 million, Uuzwaji wa nyumba za Serikali $200m and counting, ununuzi wa Rada $40 million, Ununuzi wa magari ya jeshi na helicopters huu kiasi chake mpaka leo hii kinafichwa, Ununuzi wa ndege ya Rais hatujui kiasi halisi, Mkataba wa ATCL haijulikani utatugharimu kiasi gani maana bado haujaisha, huu wa Dowans nao haujulikani nao mpaka utakapokwisha tutakuwa tumeporwa kiasi gani. Wale RITES nao kutoka India waliingia bila hata senti tano wakafanya wizi wa hali ya juu katika bank acccunts za TRC na wakagoma kukaguliwa na sasa wanakinga mkono kutaka kulipwa $87 million. Naomba tusielekeze malalamiko yetu kule kusikohusika i.e. Kwa Watanzania walio nje.

Watanzania waishio nje ya nchi hawakuhusika kwa namna moja au nyingine katika madudu yote hayo niliyoyataja hapo juu yaliyofanywa na Serikali za awamu ya tatu na ya nne na pia wana haki ya kujadili na kutoa maoni yao kuhusu chochote kile kinachojiri ndani ya nchi yao kama wale ambao wapo ndani ya nchi bila mawazo yao kuonekana kama ni HOVYO KABISA.

Siku na kazi njema

Cheers



 
Hivi watanzania wanashindwa kuchoma moto hii mitambo ili tusahau ili janga...tumechoka kusikia haya maswala TZ.
 
Shossi, Kitu ninachokupendea ni kuwa huwa unasimamia hoja zako kwa kile unachokiamini.Kudos! Ninaiona hoja yako tena kwa mantiki. La muhimu ujibu hoja za wenzako kwa mantiki pia. Comrade, punguza jazba! mara nyingi inaficha hoja zako nzito (ushauri). Mathalani unaposema hao wanaoishi majuu ni Hovyo! mhh, sijui sehemu anayoishi mtu inahusiana vipi na hoja. Kwahiyo wale wanaoishi uwanja wa fisi, au mimi ninayeishi Dongobeshi na shopping yangu ni Loliondo utasikiliza hoja zetu kweli!

Mkuu Nguruvi,

Watu wa majuu uhovyo wao ni kuwa hawajui machungu na athari za mgao wa umeme, mimi nafahamu adha na makali ya mgao ninasikitishwa na jinsi wanavyochangia hoja ya Dowans! wakumbuke hii Dowans ni kitu cha juzi kuna madudu ya miaka nenda rudi lakini hatuyazungumzii wala kuyaundia kamati teule za bunge! Wartsila, IPTL, Songas na Aggreko haya ni majuinamizi/mamumiani kwa Tanesco na sisi zaidi ya hiyo Dowans! Nastaajabishwa na kwanini watanazania tumetekwa sana hii hoja na hatutaki imalizike? Kama sisi wazalendo na hao watu wa majuu ni wazalendo kwanini wasiwaonyeshee vidole wale wenye kuiumiza Tanesco zaidi? huo uzaleondo wao wa maboksi?

Tumesikia kuwa mitambo ya Dowans inabidi iwashwe kupunguza makali ya mgao wenzetu wa majuu wanakuja juu isiwashwe sababu nini hasa? eti sabbabu ni mmiliki! inahusu nini? hapo ndio utakapochoka hoja hazijibiwi kwa hoja wanajibu kwa hisia. Kama Dowans wanaidai Tanesco hili suala jingine sie tunahitaji umeme!!!! nyie mliopo majuu kama mnataka mitambo ya Dowans isiwashwe na nyie mrudi muonje adha ya mgao!
 
Mkuu vipi tenaaaa!? Watanzania wanaoishi nje ndiyo HOVYO KABISA!

Siku na kazi njema

Cheers




Mkuu soma between the lines nauliza kwanini Dowans???????????????? kwanini sio IPTL yenye mkataba wa miaka 20 inayotutoza capacity charges mil 300 au Songas inayotulima capacity charges mil 265! au mikataba ya hayo makampuni ni fair na iliwekwa wazi tukaikubali??????

Kama huu ndio u great thinker then nadhani mie sina uwezo wa kufikiri...............

Siku njema na wewe mitambo ya Dowans na isiwashwe tule adha ya mgao au vipi?
 
Mkuu soma between the lines nauliza kwanini Dowans???????????????? kwanini sio IPTL yenye mkataba wa miaka 20 inayotutoza capacity charges mil 300 au Songas inayotulima capacity charges mil 265! au mikataba ya hayo makampuni ni fair na iliwekwa wazi tukaikubali??????

Naona kuna tatizo la kimatiki katika hoja yako. Kumbuka haya yalianzia kwenye Richmond ambapo matokeo ya uchunguzi rasmi wa kamati ya bunge yayalipelekea kumwangusha PM na baraza zima la mawaziri. hivyo nadhani kuna tofauti kubwa sana ya namna Dowans ilivyoingia kwenye hili sakata ukilinganisha na hayo makampuni mengine. Hao wengine hatuna 'uhakika' juu ya wizi wao (angalau katika level ya uchunguzi wa kibunge) lakini hili la Dowans lipo wazi zaidi na ndio maana watu wanapiga kelele. Naweza kusema hivi , hao wengine wanatuibia usiku tu lakini kwenye dowans tunaibiwa 'mchana kweupe'!).
 
Kwa kweli mimi sio muumini wa miujiza.... I can see everything openly! Kwamba mabwawa yanaelekea kukauka... hilo nalo uongo? kwamba Songas ilipata hitilafu ya mitambo yake.... amkeni Watanzania... angalieni vitu kwa mapana zaidi.

Nadhani wewe una haja ya kufanya hivyo haraka zaidi kuliko hata hao watanzania unaosema. Kwamba mabwawa yanaelekea kukauka hilo Sio Uongo lakini tujiulize, Hii ndio mara ya kwanza kuwa na tishio la kukauka mabwawa kiasi cha kutufanya kuanza kutafuta njia za dharura na zimamoto ili kulikabili tatizo la giza linalotukabili???
Mgawo mkubwa wa kwanza ulianza mwanzoni mwa miaka ya 90 kutokana na tishio hili hili lisiloisha la 'Mabwawa Kukauka'.
Kama Viongozi wetu na Chama chao wangekuwa na Vision mwaka huu tusingekuwa tunafikishwa tena mahali pa kulazimishwa tukubali mitambo ya kitapeli iwashwe ili ati kutuokoa na giza! Miaka kumi na tano na zaidi ya kuwa na mgawo wa umeme kila mwaka ingetufanya tuwe tayari na nia mbadala za kukabiliana na mabwawa yanayokauka kila mwanzo wa mwaka kwa faida ya baadhi ya watu!!
Kukubali kirahisi kwamba ati mitambo ya Dowans iwashwe ili tujiepushe na giza ni kukubali kuingizwa kwenye Upumbavu wa viongozi wetu.

Ingebidi tufike mahali tukubali kukaa hata mwaka mzima na mgawo wetu ilimradi tunapata njia za uhakika na za kudumu kukabiliana na giza na utapeli wa matapeli wa kimataifa kama dowanz na wapambe wao nchini.

Huko nyuma tuliishawahi kuwa na mgawo wa umeme kwa miezi Nane, rudia NANE na bado tuliendelea ku-survive. Kwa nini leo hii tushindwe kufanya hivyo ili mradi tu katika kufanya hivyo tunaepukana na utapeli tunaofanyiwa na Viongozi wetu na sisi kufikia hatua ya kuona ni halali mitambo ya Duwanzi kuwashwa ili tuokoke na Giza???
Mpaka lini hii dharura isiyokwisha??

Umenena vyema, Watanzania tunapaswa kuamka na kuangalia vitu kwa mapana zaidi! na tufanye hivyo basi na kuchukua hatua zinazostahili.
 
Back
Top Bottom