Mitambo ya Dowans sasa kuwashwa - Waziri Mkuu Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitambo ya Dowans sasa kuwashwa - Waziri Mkuu Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Mar 1, 2011.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda leo ametamka rasmi kuwa TANESCO itaingia mkataba mpya na Dowans wa kuzalisha umeme.

  Amesema mitambo ya Dowans itawashwa muda wowote kuanzia sasa licha ya kesi iliyopo mahakamani kuhusu tozo ya ICC.

  Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhutubia mkutano ulioandaliwa na The Economist kwenye hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam, Pinda alisema kuwa ni vyema SONGAS au kampuni nyingine binafsi inakununua mitambo ya Dowans siku zijazo ili iendelee kuzalisha umeme nchini.

  Alisema hivi sasa kuna upungufu wa 160MW kwenye gridi, hivyo 100MW ya Dowans ingesaidia kupunguza makali ya mgao.

  Pinda alisema serikali kununua mitambo ya Dowans imeleta maneno mengi kuwa haiwezekani serikali ikanunua mitambo iliyotumika, hivyo ameona suluhisho ni kwa SONGAS au mfanyabiashara mwingine mkubwa anunue mitambo ya Dowans na aingie kwenye mkataba wa muda mrefu na TANESCO wa kuzalisha umeme.

  Tayari Baraza la Mawaziri limetoa kibali kwa TANESCO kuingia mikataba ya kukodi umeme kama ya Richmond/Dowans ili kupata 260MW.

  Sasa hivi inasubiriwa bodi ya wakurugenzi ya TANESCO itoe tamko rasmi kuwa serikali itaingia mkataba mpya na DOwans.

  Hivi hawa mafisadi wa DOWANS wataendelea kupora pesa za wavuja jasho wa Tanzania mpaka lini?
   
 2. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Kuiwasha sawa lakini kwa gharama ya nani na madeni ya nyuma atalipa nani.
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  And the story goes on......
   
 4. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  uuuuuuuuuuuuuuwwwwwwwwwwwwwwwwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii uwi uwi
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,234
  Trophy Points: 280
  Nilisema kule nyuma, na ninasema tena, sio tuu tumeingia mkataba mpya, hata deni tutalipa!.
   
 6. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Sinema inaelndelea. Hivi kazi ya Ngeleja ni ipi pale wizarani maana haya ni matokeo ya Kamati ya January Makamba. Tutaona mengi mwaka huu. N sasa tunaelekea kuwalipa hata hilo deni piga ua
   
 7. Glue

  Glue Senior Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hili ni changa la macho.........
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Daaaaa kweli tufwile! , tosue mweeee!
   
 9. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 482
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  kuhusu ule mzigo ndo wamesamehe au?du kama bado wanatudai kweli sisi shamba la bibi kwani ule mzigo c watosha kuagiza kamtambo kapya/WADAU HEBU NI JUZENI
   
 10. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #10
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Wawashe tu tupate umeme...
   
 11. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  yale yale! walijua mwisho wa siku tutafika hapo, sasa leo wanamjua mmiliki wa Dowans
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Safi sana Pinda!

  Kila binadamu mwenye akili timamu lazima apende kuwa na "mchango kwenye jamii & heshima ya kutambulika pia" - "meaning & contribution" - LEGACY!

  Kwa hili Pinda you will be remembered, my brother!
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  wahenga walisema:

  baniani mbaya kiatu chake dawa
   
 14. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  January alishaonyesha njia, na ujio wa mwarabu ndiyo hivyo tena. Mkataba huo utakuwa siri ili wachache waneemeke! Kufa kufaana wakuu,
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ukiwa na roho nyepesi unaweza ukajitoa roho kwa vitukp vya nchi hii.
   
 16. 911

  911 Platinum Member

  #16
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  New brand day,same old bulsh!T.
   
 17. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Au Ali Hadaiwi alitembeza bahasha nini?

  Au January alikula tayari kutoka kwa RA na EL nini?
   
 18. f

  fat faza Member

  #18
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duu mitambo kuwashwa???hivi hawa viongozi wetu wameletwa na nani???JAMANI NISIDIENI JE HUU SI UTAWALA WA SHETANI??????
   
 19. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #19
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wafanye wanavyotaka ila nguvu ya uma itafanya kazi yake. Naona wameanza kumpaka matope Pinda wa watu na uchafu wao wa ufisadi.

  peoples power,
   
 20. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #20
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kama kweli nyie wazalendo basi mjue kuna zaidi ya Dowans inanitia shaka nadhani kuna kitu kwenye hii Dowans ndio maana ikitajwa wote mnaruka uwiiiii, jamani tumevamiwa na longo longo jingiiiii hamjengi haja za msingi kwanini Dowans isiwasheshwe. Pengine hamfahamu kuwa IPTL yenye mkataba wa miaka 20 ndio ni kampuni ya kufua umeme ghali maradufu ya Dowans mbona yenyewe mmeinyamazia? au yenyewe haikuingia mkataba na tenesco kwa kutumia hila? Sisi wananchi lazima tuwe na upeo wa kujiuliza mambo tusikurupushwe na wanasiasa kisha tukawa tunaitikia viitikio vyao.

  Umeme wa Dowans lazima uwashwe ili kuwapunguzia makali wananchi! utasaidia kuongeza production viwandani! sioni tatizo la kuwashwa mitambo ya Dowans ikiwa maslahi ya taifa yataangaliwa upya katika huo mkataba mpya. Sitapenda kulalama na kuropoka mpaka pale nitakapojua IPTL, AGGREKO na SONGAS WASAFI kiasi gani.......

  My take.

  Tuache ushabiki wa kishamba tuchambue hoja ili kujenga hoja...............
   
Loading...