Mitambo ya Dowans sasa kuwashwa - Waziri Mkuu Pinda

Wakuu,

Mimi nadhani kuwashwa kwa mitambo si tatizo, tatizo ni mchakato mzima toka wameanza kwa Richmond hadi Dowans!!! Wakuu wetu wa nchi wamekaa kutowatambua wamiliki, ilhali hayo yakitokea na saga lote kwenda mbele na nyuma, tunaishia kuambiwa prime minister anasema mitambo inawashwa, sasa does this mean uozo wote umekwisha? Utapeli wote umekwisha, haya makampuni yamekuwa safi? Maana ikumbukwe Richmond ilitamkwa bungeni kuwa kampuni hewa, Dowans pia....

Ina maana serikali leo imemjua mmiliki? IPTL haina tabu maana mmiliki anajulikana, shida ni umbumbumbu wa viongozi wetu waliosign mkataba wa kijinga, we are continually paying the price...
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda leo ametamka rasmi kuwa TANESCO itaingia mkataba mpya na Dowans wa kuzalisha umeme.

Amesema mitambo ya Dowans itawashwa muda wowote kuanzia sasa licha ya kesi iliyopo mahakamani kuhusu tozo ya ICC.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhutubia mkutano ulioandaliwa na The Economist kwenye hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam, Pinda alisema kuwa ni vyema SONGAS au kampuni nyingine binafsi inakununua mitambo ya Dowans siku zijazo ili iendelee kuzalisha umeme nchini.

Alisema hivi sasa kuna upungufu wa 160MW kwenye gridi, hivyo 100MW ya Dowans ingesaidia kupunguza makali ya mgao.

Pinda alisema serikali kununua mitambo ya Dowans imeleta maneno mengi kuwa haiwezekani serikali ikanunua mitambo iliyotumika, hivyo ameona suluhisho ni kwa SONGAS au mfanyabiashara mwingine mkubwa anunue mitambo ya Dowans na aingie kwenye mkataba wa muda mrefu na TANESCO wa kuzalisha umeme.

Tayari Baraza la Mawaziri limetoa kibali kwa TANESCO kuingia mikataba ya kukodi umeme kama ya Richmond/Dowans ili kupata 260MW.

Sasa hivi inasubiriwa bodi ya wakurugenzi ya TANESCO itoe tamko rasmi kuwa serikali itaingia mkataba mpya na DOwans.

Kweli mafisadi wa Dowans wataendelea kupora pesa za wavuja jasho wa Tanzania!

Hapa kuna uongo na kweli na kuna upotoshwaji wa kusudi: Hebu someni alichosema JK na kuona kilichoamuliwa na Baraza la Mawaziri ni Dowans ama ni mitambo mingine ya kukodi?

"Ndugu wananchi,
Jambo la nne ni hali ya umeme. Kama mnavyofahamu, hali ya upatikanaji wa umeme nchini ni mbaya. Chanzo cha matatizo ni kupungua sana kwa maji katika Bwawa kubwa la Mtera. Hadi jana kina cha Bwawa hilo kimeshuka hadi kufikia mita 691.25 ambacho ni pungufu kwa mita 7. Kwa sasa zimebaki mita 1.25 tu juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme.

Tarehe 15 Februari, 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa TANESCO wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme. Baraza limeitaka Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha kuwa mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi. Aidha, imesisitizwa kuwa pamoja na udharura uliokuwepo sheria na taratibu za manunuzi ya umma vizingatiwe. Pia, wahakikishe kuwa mkataba wataoingia uwe ni wenye maslahi kwa taifa. Vile vile, watoa huduma wawe ni makampuni yanayofahamika na yenye sifa stahiki na kuaminika.

Natambua kuwa Bodi na Mejemienti ya Shirika la Umeme, wanaendelea na mchakato wa kupata umeme huo wa dharura kati ya sasa na Julai, 2011.

Ndugu Wananchi;

Tulipopata tatizo kama hili mwaka 2006/2007 tuliamua kuwa tuanze safari ya kupunguza kutegemea mno umeme wa nguvu ya maji kwa kuongeza matumizi ya vyanzo vingine vya nishati. Mpango umetengenezwa na utekelezaji wake unaendelea. Tayari umeme wa MW 145 wa kutokana na gesi asilia umeongezwa kwa kugharamiwa na Serikali. Aidha, mwisho wa mwaka huu MW 160 zitaongezeka yaani MW 100 Dar es Salaam na MW 60 Mwanza kwa gharama za Serikali.

Bahati mbaya kutokana na matatizo ya fedha ya kimataifa, wawekezaji wa sekta binafsi wa kuzalisha MW 300 za umeme wa gesi asilia pale Mtwara walijiondoa. Umeme huo ungekuwa tayari umeshaingizwa katika gridi ya taifa hivi sasa na kuondoa tatizo la sasa. Wawekezaji wengine wamepatikana na mazungumzo yanaendelea vizuri. Mradi wa Kiwira umecheleweshwa na mchakato wa kubadili milki na kupata mkopo wa dola za Marekani 400 milioni za kuwezesha ujenzi wa kituo cha kuzalisha MW 200. Suala la kubadili milki limefikia ukingoni na mchakato wa kupata mkopo unaendelea kwa matumaini.

Ndugu Wananchi;

Waswahili wana msemo usemao "jitihada za mwanadamu hazishindi kudra ya Mwenyezi Mungu". Bahati mbaya sana tatizo la ukame limetukuta tena wakati mipango hiyo haijakamilika. Miaka miwili ijayo hali itakuwa tofauti sana kwani miradi hii na mingine kadhaa itakuwa imekamilika na kulihakikishia taifa uhakika wa umeme.
Naomba ndugu zangu muelewe kuwa miradi hii huchukua muda kukamilika. Mitambo huchukua muda kutengenezwa na ujenzi wa kituo nao pia. Ingekuwa ni mitambo ya kununua tu dukani tungefanya hivyo na kulimaliza mara moja tatizo hili. Tena lingeisha zamani na wala sisi tusingelikuta. Subira yavuta heri."

Kwa maelezo hayo hapo juu, suala la Dowans inayozalisha MW100 liko wapi?
 
Wakuu,

Mimi nadhani kuwashwa kwa mitambo si tatizo, tatizo ni mchakato mzima toka wameanza kwa Richmond hadi Dowans!!! Wakuu wetu wa nchi wamekaa kutowatambua wamiliki, ilhali hayo yakitokea na saga lote kwenda mbele na nyuma, tunaishia kuambiwa prime minister anasema mitambo inawashwa, sasa does this mean uozo wote umekwisha? Utapeli wote umekwisha, haya makampuni yamekuwa safi? Maana ikumbukwe Richmond ilitamkwa bungeni kuwa kampuni hewa, Dowans pia....

Ina maana serikali leo imemjua mmiliki? IPTL haina tabu maana mmiliki anajulikana, shida ni umbumbumbu wa viongozi wetu waliosign mkataba wa kijinga, we are continually paying the price...

kwa wao maana yake kila kitu ni shwari kwa sasa
je ni kwa nini wasiingize mitambo mipya mingine?/
hivi kuna utata gani?/kama tatizo ni pesa na hiyo mitambo wanatumia bure?? hapana..
 
Du! Kweli sisi mbumbu wa mambo ya uchumi... yaani hilo nalo tatizo na wanasiasa wakombozi kama CHADEMA hawaoni ni vyema kupata 100MW kunusuru uchumi kuliko kupiga makelele yasiokuwa na maana kweli taifa limetekwa.

CDM hawakusema mitambo isiwashwe ila wamesema wasilipwe na mitambo itaifishwe. Kwa kufanya hivyo hatutapta hasara yeyote. Ila anavyofanya Pinda na Mkwere tuna mashaka nayo.
 
Kwa hiyo hawa jamaa wanaendelea kutudanganya??
Raisi anaongea togauti na PM naye anakuja kivyake..duh hii ni kali
Hapa kuna uongo na kweli na kuna upotoshwaji wa kusudi: Hebu someni alichosema JK na kuona kilichoamuliwa na Baraza la Mawaziri ni Dowans ama ni mitambo mingine ya kukodi?

"Ndugu wananchi,
Jambo la nne ni hali ya umeme. Kama mnavyofahamu, hali ya upatikanaji wa umeme nchini ni mbaya. Chanzo cha matatizo ni kupungua sana kwa maji katika Bwawa kubwa la Mtera. Hadi jana kina cha Bwawa hilo kimeshuka hadi kufikia mita 691.25 ambacho ni pungufu kwa mita 7. Kwa sasa zimebaki mita 1.25 tu juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme.

Tarehe 15 Februari, 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa TANESCO wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme. Baraza limeitaka Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha kuwa mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi. Aidha, imesisitizwa kuwa pamoja na udharura uliokuwepo sheria na taratibu za manunuzi ya umma vizingatiwe. Pia, wahakikishe kuwa mkataba wataoingia uwe ni wenye maslahi kwa taifa. Vile vile, watoa huduma wawe ni makampuni yanayofahamika na yenye sifa stahiki na kuaminika.

Natambua kuwa Bodi na Mejemienti ya Shirika la Umeme, wanaendelea na mchakato wa kupata umeme huo wa dharura kati ya sasa na Julai, 2011.

Ndugu Wananchi;

Tulipopata tatizo kama hili mwaka 2006/2007 tuliamua kuwa tuanze safari ya kupunguza kutegemea mno umeme wa nguvu ya maji kwa kuongeza matumizi ya vyanzo vingine vya nishati. Mpango umetengenezwa na utekelezaji wake unaendelea. Tayari umeme wa MW 145 wa kutokana na gesi asilia umeongezwa kwa kugharamiwa na Serikali. Aidha, mwisho wa mwaka huu MW 160 zitaongezeka yaani MW 100 Dar es Salaam na MW 60 Mwanza kwa gharama za Serikali.

Bahati mbaya kutokana na matatizo ya fedha ya kimataifa, wawekezaji wa sekta binafsi wa kuzalisha MW 300 za umeme wa gesi asilia pale Mtwara walijiondoa. Umeme huo ungekuwa tayari umeshaingizwa katika gridi ya taifa hivi sasa na kuondoa tatizo la sasa. Wawekezaji wengine wamepatikana na mazungumzo yanaendelea vizuri. Mradi wa Kiwira umecheleweshwa na mchakato wa kubadili milki na kupata mkopo wa dola za Marekani 400 milioni za kuwezesha ujenzi wa kituo cha kuzalisha MW 200. Suala la kubadili milki limefikia ukingoni na mchakato wa kupata mkopo unaendelea kwa matumaini.

Ndugu Wananchi;

Waswahili wana msemo usemao "jitihada za mwanadamu hazishindi kudra ya Mwenyezi Mungu". Bahati mbaya sana tatizo la ukame limetukuta tena wakati mipango hiyo haijakamilika. Miaka miwili ijayo hali itakuwa tofauti sana kwani miradi hii na mingine kadhaa itakuwa imekamilika na kulihakikishia taifa uhakika wa umeme.
Naomba ndugu zangu muelewe kuwa miradi hii huchukua muda kukamilika. Mitambo huchukua muda kutengenezwa na ujenzi wa kituo nao pia. Ingekuwa ni mitambo ya kununua tu dukani tungefanya hivyo na kulimaliza mara moja tatizo hili. Tena lingeisha zamani na wala sisi tusingelikuta. Subira yavuta heri."

Kwa maelezo hayo hapo juu, suala la Dowans inayozalisha MW100 liko wapi?
 
Wakuu,

Mimi nadhani kuwashwa kwa mitambo si tatizo, tatizo ni mchakato mzima toka wameanza kwa Richmond hadi Dowans!!! Wakuu wetu wa nchi wamekaa kutowatambua wamiliki, ilhali hayo yakitokea na saga lote kwenda mbele na nyuma, tunaishia kuambiwa prime minister anasema mitambo inawashwa, sasa does this mean uozo wote umekwisha? Utapeli wote umekwisha, haya makampuni yamekuwa safi? Maana ikumbukwe Richmond ilitamkwa bungeni kuwa kampuni hewa, Dowans pia....

Ina maana serikali leo imemjua mmiliki? IPTL haina tabu maana mmiliki anajulikana, shida ni umbumbumbu wa viongozi wetu waliosign mkataba wa kijinga, we are continually paying the price...

Zanzibar wali-deal na historia hivyo hivyo mpaka baada wakajua huwa historia hailipi!!! sasa tatizo lilikuwa Richmond (history) then mkatapa ukasainiwa halali kabisa na DOWANS... yet leo watu wazima wanaongelea DOWANS ambao haina issue yoyote... yaani... our brains are......
 
CDM hawakusema mitambo isiwashwe ila wamesema wasilipwe na mitambo itaifishwe. Kwa kufanya hivyo hatutapta hasara yeyote. Ila anavyofanya Pinda na Mkwere tuna mashaka nayo.
Ndio matatizo tuliyonayo sisi.

Kwa nini usilipe? Na kwa nini utaifishe? please provide concreate and legal stands on this!!! Acha siasa za Kipuuzi!!! DOWANS is not RICHMOND you need to be clear on this? DOWANS ina mkataba halali na TANESCO na ili-deliver per contract.
 
Kasheshe said:
Kwa kweli mimi sio muumini wa miujiza.... I can see everything openly! Kwamba mabwawa yanaelekea kukauka... hilo nalo uongo? kwamba Songas ilipata hitilafu ya mitambo yake.... amkeni Watanzania... angalieni vitu kwa mapana zaidi.

Kasheshe,

..ninasema tatizo ni la kutengeneza kwasababu wahusika waliamua kwa makusudi kutoiruhusu Tanesco kununua mitambo mipya. labda ningesema haya matatizo ni ya kujitakia ningeeleweka vizuri zaidi.

..kwa maneno mengine wahusika wanasubiri mpaka matatizo yawe makubwa, na wananchi waanze kutaabika, halafu wanatumia upenyo huo kusaini mikataba inayoliumiza taifa na kuneemesha mifuko yao.
 
Wanaofahamu kama Mh. Sitta na Mwakyembe wameridhia haya maamuzi watujuze. Au maamuzi yataishia kwenye Bodi ya Tanesco ili kuwakwepa hawa wapambanaji kwenye Baraza la Mawaziri?
Jana hukuisoma speech ya JK ? mbona alielezea kila kitu kuwa wamekaa baraza la mawaziri na kukubaliana kuingia huo mkataba.
Au una maanisha hao akina 6 na mwakembe hawakuwepo kwenye kikao?
 
Mh,haya wabongo na kukulupuka dowans,dowans kelele nyingi hivi kweli na kelele zote hizo viongozi wako tayari kuwasha ujue watu walilishwa longolongo wakalipokea zimazima YATAWARUDI MWAKO HUU.Tunataka prove ya kwamba adawi ni fake.mianasiasa mingine bana kwani ukiwa rais hufi
 
Bora wewe kaka. Kubali yaishe, ila usije ukawa unatetea udini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Ndugu yangu umeshindwa kuona uozo huu, eti kuna maslai ya Taifa. Iweje wanadai na huku kukiwa na wasiwasi wa kulipwa tena wakubali kuingia mkataba mwingine.

Baba Pinda, Mhe. kuna haja gani ya kununua mitambo hii wakati mmiliki wake ni mwenzetu. Au ameseme hataki kuingia mkataba tena. Tatizo lenu ni kuficha mwenye mitamba wakati hanajulikana!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Akili yako imejengeka kidinidini, hivi nikuulize waliosaini makubaliano kwa upande wa dowans na tanesco wote wa dini moja? acheni kubwabwaja leteni hoja msiingize mambo ya dini na siasa kwenye suala la umeme. Watafuteni waliiingiza Tanzania hapa! Mimi natofautiana na wewe pamoja na wengine kupiga kelele kuhusu Dowans na kunyamaza kuhusu IPTL yenye mkataba wa miaka 20. Dowans wanachaji capacity charges mil 152, IPTL wanatuchaji mil 300 Songas wanatulima 265 najiuluza hao wengine waliingia mkataba na tanesco kihalali na ni makampuni "malaika" basi kwanini wanatutoza zaidi ya "shetani" dowans? au kuna jambo jamani? au mie sina akili labda nawaza tofauti na wenzangu?

Naona huku kunanishinda ngoja niende zangu kwenye jukwaa la mapenzi na mahusiano niwaacheni nyie majiniasi wenye kuona 300 mil ni ndogo ila 152 mil ni nyingi!
 
Hatari kubwa inatunyemelea. walijua tu ndio maana hawakuchukua hatua madhubuti mapema ili waje waiwashe baadaye. Hii si bahati mbaya bali ilipangwa. Kina cha maji kilianza kuleta taabu miaka 6 iliyopita. Mitambo sasa ina miaka minne nchini. January alikuwa anayajua yote yote ndiyo maana aliipigia debe . But the truth will be the next when Chadema takes over
 
Kuwasha mitambo ya Downs ni sawasawa na Mkeo kufile kesi ya divorce mahakamani halafu anaendelea kulala na mumewe kabla kesi haijawa finalised

Mtalaka hatongozwi!!

Lisilo budi hutendwa, kichungu huonjwa
Japo chungu vumilia pia ni dawa
Baniani mbaya kiatu chake dawa
Likikosekana la mama lafaa lambwa
 
Akili yako imejengeka kidinidini, hivi nikuulize waliosaini makubaliano kwa upande wa dowans na tanesco wote wa dini moja? acheni kubwabwaja leteni hoja msiingize mambo ya dini na siasa kwenye suala la umeme. Watafuteni waliiingiza Tanzania hapa! Mimi natofautiana na wewe pamoja na wengine kupiga kelele kuhusu Dowans na kunyamaza kuhusu IPTL yenye mkataba wa miaka 20. Dowans wanachaji capacity charges mil 152, IPTL wanatuchaji mil 300 Songas wanatulima 265 najiuluza hao wengine waliingia mkataba na tanesco kihalali na ni makampuni "malaika" basi kwanini wanatutoza zaidi ya "shetani" dowans? au kuna jambo jamani? au mie sina akili labda nawaza tofauti na wenzangu?

Naona huku kunanishinda ngoja niende zangu kwenye jukwaa la mapenzi na mahusiano niwaacheni nyie majiniasi wenye kuona 300 mil ni ndogo ila 152 mil ni nyingi!

duh,nimekukubali kaka hii sikujua unajua humu kuna magreat thinker lakni sio.mi mgeni humu ila nishajua kuna jamaa humu wana lao jambo tu na sivingine na wengi wako majuu yani oovyo hasa
 
Kama kweli nyie wazalendo basi mjue kuna zaidi ya Dowans inanitia shaka nadhani kuna kitu kwenye hii Dowans ndio maana ikitajwa wote mnaruka uwiiiii, jamani tumevamiwa na longo longo jingiiiii hamjengi haja za msingi kwanini Dowans isiwasheshwe. Pengine hamfahamu kuwa IPTL yenye mkataba wa miaka 20 ndio ni kampuni ya kufua umeme ghali maradufu ya Dowans mbona yenyewe mmeinyamazia? au yenyewe haikuingia mkataba na tenesco kwa kutumia hila? Sisi wananchi lazima tuwe na upeo wa kujiuliza mambo tusikurupushwe na wanasiasa kisha tukawa tunaitikia viitikio vyao.

Umeme wa Dowans lazima uwashwe ili kuwapunguzia makali wananchi! utasaidia kuongeza production viwandani! sioni tatizo la kuwashwa mitambo ya Dowans ikiwa maslahi ya taifa yataangaliwa upya katika huo mkataba mpya. Sitapenda kulalama na kuropoka mpaka pale nitakapojua IPTL, AGGREKO na SONGAS WASAFI kiasi gani.......

My take.

Tuache ushabiki wa kishamba tuchambue hoja ili kujenga hoja...............

Tulia kaka, tatizo sio ushamba wala ushabiki, pia sisi sote tunaumia na mgao wa umeme kwa namna moja au nyingine. Tatizo ni je DOWANS ni nani, tumeingia mkataba na nani. Kumbuka rais wako alisema kuwa hawajui DOWANS na leo hii nchi yake inaingia mkataba na mtu ambaye hajulikani hata kwa rais.

Pia matatizo yasiwe chanzo cha utumwa, kumbuka kuwa kwa sasa DOWANS ni adui wa watanzania maana ana mpango wa kutupora bilion 94. Sasa adui anapotumia matatizo yako kukufilisi lazima ushituke. Kinachoonekana hapa ni kwamba watanzania tunaichukia DOWANS ila watawala wetu wapo karibu nae sana huyu mdudu.

Anyway tunahitaji umeme, ila shida zetu zisituongezee shida zingine, ni bora kutafuta another altenative kwa umakini zaidi kuliko kukurupuka kihivyo.

I love my country but I hate her people
 
Pinda ameamua kuingia kundi la mafisadi,si yule mtaratibu tena! Wameshamchakachua hawa jamaa...eeh Mungu ipe nguvu chadema maana ndio kimbilio letu lililobaki.

Kweli huyu mzanzibari mkimbizi aka starring wa movie ya dowans amemwaga heelaa! Hizi watakula now,ila watazitapika kesho..they should be careful.

Kwangu mimi ni bora nilale gizani,kuliko kutumia umeme wa dowans..wakiwasha naweka solar kwangu,I swear
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom