Mitambo ya Dkt. Bashiru yazoa upinzani jiji la Tanga

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Messages
859
Points
1,000

Egnecious

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2015
859 1,000
Siku ya tatu ya ziara ya Dkt. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Tanga, imezoea upinzani ambapo madiwani Nane wa CUF wamekihama Chama hiko na kujivua nafasi zao zote na kujiunga na CCM.

Uamauzi huo wameufanya katika mkutano wa ndani wa Katibu Mkuu wa CCM alipokuwa akizungumza na viongozi wa Mashina, Matawi na Kata wilaya ya Tanga mjini katika uwanja wa Mkwakwani jioni ya leo tarehe 15 Januari, 2020.

Viongozi hao wameongozwa na Mwenyekiti wa CUF Mkoa wa Tanga Ndg. Bashiru Azizi na Naibu Meya wa jiji la Tanga Ndg. Haniu Ally kata ya Tangasisi, madiwani wengine ni Mswahili Njama Kata ya Chongoleani, Ndg. Said Alei Diwani Kata ya Masiwani na Habibu Mpa Diwani Kata ya Ngamiani Kati.

Wengine ni Ndg. Nassoro Salimu Diwani Kata ya Tongoni, Akida O. Akida Diwani Kata ya Ngamiani Kaskazini, Mwanaisha Abdala Diwani Viti Maalum Tarafa ya Chumbageni, Thurekha Mahadhi Diwani Viti Maalum Tarafa ya Ngamiani na Mke wa Mbunge wa CUF Tanga Mjini.

Licha ya viongoz hao, Makada wengine waliokihama Chama hiko wameongozwa na Bi. Hidaya Ahmed aliyekuwa Kampeni Meneja wa Jimbo la CUF.

Madiwani hao waliojiunga na CCM wameeleza sababu mbalimbali za kukihama Chama hiko, ikiwa ni pamoja na vyama vyao kukosa dira ya uongozi na kuelekea kupoteza uhalali wa kuomba ridhaa ya kuwaongoza Watanzania, hivyo wamerudi CCM kutoa mchango katika maendeleo makubwa yanayoendelea kufanyika chini ya umadhubuti wa CCM inayoongozwa na Mwenyekiti na Rais wa Tanzania Ndg. John pombe Joseph Magufuli.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
IMG-20200116-WA0055.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,390,782
Members 528,265
Posts 34,061,719
Top