Hapo nyuma barabara ya kuelekea Bwiru kutokea Kona ya Bwiru karibu na Kanisa la Baptist napo palikuwa hatari sana. Vijana wa hapo waliwahi kumkaba mwanajeshi, wakamjeruhi. Kilichofuatia hapo baada ya wiki mbili toka mwanajeshi akabwe, ni fundishontoka kwa vibaka. Siku hizi hata upite saa nane, hutasikia hata mjusi akikimbia. Wanajeshi walitoa fundisho.