Miswada mitatu(3) ya kujadili masuala ya madini na maliasili yafikishwa Bungeni kwa hati ya dharura

12. National Assembly MAY.....

Hii MAY hii ndo kikwazo Chenyewe! Kwanza inalipunguzia bunge nguvu yake, kwa sababu Serikali isipotaka mikataba ipitiwe, haitoipeleka miswada hiyo bungeni na serikali itakuwa sahihi kisheria!. Neno May liondoke liwekwe neno SHALL, ili mikataba yote ya rasilimali ipitiwe na bungw pia
Muhimu.Serikali hii inaweza kuwa na dhamira Nzuri.Ya kesho jee?yaweza kukitumia vizuri kiufisadi kipengele hicho.
 
Ninaunga mkono 100 kwa 100... hii miswada kwanza ni mifupi na inaeleweka kabisa. Kwa mzalendo yeyote yule hawezi kupinga hichi kilicholetwa. Kudos Mhe Rais... tupo nyuma yako.
Kwani ilivyoletwa mara ya kwanza si ilikuwa inaeleweka kama hivi na ikapita kwa haraka sababu ya kueleweka kwake?
 
Hakuna mswada mpya hata mmoja hapo. Hawa jamaa wanapenda kupiga kelele bila kuwa na substance. Serikali imepeleka amendments kurekebisha baadhi ya vifungu katika sheria mahsusi ili ku-backup (harmonise laws with financial appropriation Act 2017/18) ikiwa ni jitihada za sasa za serikali kukusanya 1% ya gross value (budget 2017/18) ya madini yanayosafirishwa kupitia minerals clearing centres (airports/bandarini/mipakani). Ni kuhakikisha kuwa nchi inanufaika zaidi na rasiimali za madini.
Mi ninachokiona,tatizo si muswada mpya au wazamani,tatizo hiyo hiyo ya zamani ilipitishwa kwa style ya haraka kama hii na ikawa na makosa kama yanayooneka.Sasa kama ndo hivyo kwanini isipewe muda wa kutosha ijadiliwe kwa umakini ili yale makosa yasijirudie,haraka ya nini kama ni kwa manufaa ya Taifa?
 
Tatizo kuna watu always are pessimistic...hata ufanye lipi jema wataona unatwanga maji kwenye kinu....nikweli huko nyuma watu walitumia vibaya fursa ya uwepo wa kupeleka miswada ya dharura wakafanya yao....but currently the government is doing its activities in a good faith....tumuunge mkono Mh. Rais wetu.
How sure you are?
 
Inajulikana tunataka kufaidi rasilimali zetu hivyo lazima tuwe wabia (wanahitaji kuweka kiwango labda 40%-50%), Tax holiday badala ya kuwa milele kama sasa wanaweka kipengele tu kwamba ni mwaka wa kwanza tu baada ya hapo wanalipa, ajira za mgodini labda 70% wawe waswahili, hakuna kuchnjua madini nje ya nchi, kila madini yanaposafirishwa lazima yarekodiwe na yapatiwe vibali kutoka benki kuu, etc!Tunahitaji kuunguza hela zetu za kodi kwa kubadilisha hivi vipengele??
Kama muda hautoshi tuwaongeze,ila wakae bila posho si wanalipwa mishahara??
Aa!hapana,posho wapewe na kazi ya maana wafanye .
Kama ndiyo hayo uliyosema yatajadiliwa kweli.
 
View attachment 532865
View attachment 532866

Kwa hali ya kawaida huwezi kulazimisha Mikataba kupitiwa na Bunge kwa kutumia Ibara moja tu ya maneno 23 (Iliyo ndani ya Sheria nyingine)ambayo inaweza kufutwa na Waziri kwa kumwekea Ibara moja yenye sehemu ndogo yenye maneno 16 kupitia Kanuni.
Pia Ibara hizo mbili zinafuatana ili kuwa rahisi utekelezaji( 12 &13).:):)
Hivyo kwa Ushauri, utengenezwe Muswada wa nne utakaohusika na Upelekaji wa Mikataba ya Rasilmali za Asili Bungeni kuidhinishwa ikiainisha Aina ya Mikataba na Utaratibu wa kupelekwa Bungeni.
Pia uainishe kuwa kama Mkataba ukikataliwa na Bunge basi unakuwa batili moja kwa moja (‘Null and Void’).

Unaweza kuitwa:
The Natural Wealth and Resources (Types of Agreements/Contracts Subject to Ratification) Act, 2017.
Hii itasaidia angalau kulihusisha Bunge kwa kutumia Sheria inayosimama peke yake..

May be reviewed by National Assembly ------Kisheria maana yake inatoa ruhusa kwa Bunge kupitia hiyo mikataba, lakini hailazimishi kwamba Bunge ni lazima iipitie hiyo mikataba. Nneno sahihi la kisheria pale lilipaswa kuwa "shall". Ingawa sio mbaya kwa kuanzia maana bunge linaweza kutoa azimio la kuiomba na kuipitia kwa kuwa wamepewa ruhusa na katiba.
 
Jamaa wanapenda posho hawa....!Hivi kweli kuna ambacho hatukijui kwenye kurekebisha sheria za madini, gesi, na mafuta??Sio kwamba inaletwa miswada mipya hapana, ni ile ya zamani ifanyiwe marekebisho ambayo tayari tumeshayapigia makelele sana!Mnataka kuendelea kutafuna kodi zetu mpk lini???Rekebisheni miswada acheni kulalama, kwanza Heche sijui kama atatoa hata mchango!
kwa hiyo lisu kasikilizwa
 
Siku ile namwona ****** katika makabidhianao ya ripoti ya wachumi na wanasheria kuhusu mchanga wa madini nikajua kuna jambo la dharura.

Hatujakaa sawa akapewa MIC na anena kwamba ipo haja ya kurekebisha sheria. Akili yangu ikasema hapa kuna something fishy around.

Kwa hati ya dharura (business as usual) dili lingine laenda kutengenezwa watz tuendelee kupigwa kwa maamuzi ya siku moja.

Hata wiki moja haitoshi katika hili ila sio mbaya, nyaya nyekundu zimeunganishwa kwenye taa ya kijani. Tunapigwa tena knock out, bila maandalizi.

HATARI SANA!
 
Kwa hii Mwekezaji atakubali kuwekeza matrilioni Tanzania?
Screenshot_20170701-103306.png
 
Sijaona chochote
Sec. 11. Kwenye permanent sovereign inasema hakuna mashauri yanayohusiana na Mali asili yatasikilizwa nje ya Tanzania. Swali ni je mahakama za tanzania ziko na independence hii ya kumuaminisha mwekezaji? Kwa sababu hiyo Tanzania inajitenga na jumuiya ya kimataifa katika biashara

Sec.7 ya hiyo attachment ya pili inamlazimisha mwekezaji kukubaliana na renegotiation ya serikali kwa lazima.
 
Sec. 11. Kwenye permanent sovereign inasema hakuna mashauri yanayohusiana na Mali asili yatasikilizwa nje ya Tanzania. Swali ni je mahakama za tanzania ziko na independence hii ya kumuaminisha mwekezaji? Kwa sababu hiyo Tanzania inajitenga na jumuiya ya kimataifa katika biashara

Sec.7 ya hiyo attachment ya pili inamlazimisha mwekezaji kukubaliana na renegotiation ya serikali kwa lazima.
Tuache hivyo hivyo ukitaka visa huwa unaweza kunegotiate?!
 
Ufanisi wa Mahakama zetu na Ukamilishaji wa Uchunguzi /Uendeshaji Mashitaka tunaujua. Ole wao kesi zitakazofunguliwa hapa nchini kwani chapu chapu matokeo yataonekana!
 
Ufanisi wa Mahakama zetu na Ukamilishaji wa Uchunguzi /Uendeshaji Mashitaka tunaujua. Ole wao kesi zitakazofunguliwa hapa nchini kwani chapu chapu matokeo yataonekana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom