Miswada mitatu(3) ya kujadili masuala ya madini na maliasili yafikishwa Bungeni kwa hati ya dharura

Mbona unapotosha kwani wabunge wanamwakilisha nani bungeni
 
Kweli wameamua japo si nguli wa sheria miswada 3 ya maliasili za nchi kwa hati ya Dharura kweli?
 
Hebu wekeni inputs acheni blah blah bana....leteni hoja za kizalendo kwenye miswada hiyo...Pingeni miswaada kwa hoja na sio kwa sababu imeletwa kwa dharura.

Maoni ya wananchi kuhusu nishati madini na maliasili yapo wazi toka enzi na enzi.
 
Kwani bunge linaandaa miswada ya sheria?!!! Muswada kwenda bungeni ni kama utaratibu tu kwa maana mswada huandaliwa na Mwanasheria Mkuu wa serikali na ukipitishwa na bunge hauwi sheria hadi Rais aukubali na kutia saini. Hivyo siku moja inatosha kabisa kwa bunge zima kupitisha hata miswada kumi.
 
Mambo ya kitoto,ghala wabunge hao hao wa chama kile kile waliopitisha sheria na kukosea kwa asilimia 99 wanaaminikaje?Bora wajadili kwa muda angalau week mmoja kila mswaada.
Kwa sababu they are not clever enough to discuss 3 issues simultaneously in one day!
 
Tuaiombea imalizike ikiwa upande wa maslahi ya mtanzania
Mbona ishu nzito kama hii itapelekwa tu kwanza tayari imeandaliwa tayri ikingia bungeni itakuwa ni kuliza tu kuwa wangapivwanaafi na wangapi wasio afiki basi.ili wake wazee waendelee kunusa na kukohoa kishibe.
 
Niko tayari kusahihishwa....Nadhani Tundu Lissu aliwahi kusema ili tuwabanevizuri wezi wa dhahabu zetu hatuna budi kubadilisha sheria zetu za madini kwanza....kama ndiyo hivyo basi tuzipitishe haraka hata hayo makontena yatakapo ondoka tupate fedha saafi na pia apongezwe.
 

Aahaaa!! Kwani wabunge si ndo wawakilishi wa wananchi. Wewe ulitakaje? Yaani watanzania milioni 20 watoe maoni yao? Aisee, haya bana.
 
KAMA ZINA UDHARULA ILI ZITUSAIDIE KWENYE SUALA LA MAKANIKIA YALIYOPO BANDARINI AM AFRAID TUMEPOTEA NJIA NA KAMA SI HIVYO HAKUNA HAJA YA KUWA NA DHARULA HIYO. WABUNGE WAPEWE WAJE NAYO KWETU WANANCHI, PIA IPITE KWA WADAU WOTE, WATAKAPORUDI BUNGENI NEXT TIME WAJADILI NA KUFIKIA MUAFAKA
 
Heche analeta mzaha kwenye mambo mazito kama wabunge wengi wa upinzani wanavyofanya.
 
Kama maandishi yamepelekwa kwa lugha ya malkia ndio kabisaaaa imekula kwa wengine hapo,akili zao zote wanasubiriatu kugonga meza na sauti za ndiooooooooo zikirindima

Siku hizo tano ni muda wa vijembe,matusi,kero,pongezi na hatimaye adhabu kwa wale ambao hawatii kiti

Jaji Mkuchika nae anawasubiri,nami bando lipo napata habari za ndani ya bunge
 
Mkuu kufanya kitu kwa nia nzuri ni jambo muhimu sana lakini kitu hicho kinaweza kufanyika vibaya na kuathiri malengo. Hata amendments lazima zisababishe mswaada na sheria yote kusomwa upya ili kujua hayo mabadiliko yana maana gani. Huko nyuma tunajua haraka imesha tumika kuficha vitu lakini pia haraka inaweza ikaruhusu vitu ambavyo havija kaa sawa kupitishwa. Baada ya kelele zote zilizopigwa itakua jambo la ajabu kupitisha amendments bila majadiliano ya kutosha. I hope bunge litakubaliana ni muda gani unatosha kwa kazi hiyo kufanyika kwa weledi unatakiwa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…