Mistari ya wimbo wa Fid Q sumu

blooms

Member
Dec 20, 2016
52
41
Alieniumba alinipa mdomo hovyo nina haki ya kuongea/ ni bahati nimeotea..safi… Kamwe siachi kuishea/ hamtaki niwe fair…? Trust me.. Me huwa happy niki-care/ na ninaowatouch husema” mshkaji upo smart upstairs / usiache kuongea/ usiache wewe ni incharge huna spear/ kipaji ka ngwear/kwa mpaji ni ka zawadi aliwagea/flag pepea/alihitaji zaidi ya Maji na mmea…? Ilikuaje wamuache hadi mshkaji ulaji wa drags ukamzoea ..?

Tunamoka ili kusafiri kihisia au kufoka pia…ikotoka ukaisikia..huwezi ichoka au kuotosa ikikuingia../ kinachoichosha hii nia…ni kulosa ulichokiota kupatia..kiwachota kihisia…tunasota je inatosha hii fidia..?

Shibe ya mdau hainilazi njaa, sababu mganga yupo juu../ furaha ya baadhi ya wadau ni kuona star anawalamba miguu.

Asie nihitaji simuhitaji, kamwe simuachi anijazie INZI../ bandidu kama TSOTSI sipigi goti kama PNC../ hakuna ambae hakosi labda ZIZI kwa DEE ANDY../ yangu self esteem haitoki ka riport za TMZ

Na hainizuii nisile mkate kwa kuhofia..kiungulia…/na uemcee hauniachi huniangalia ka fidelia../ka bruce lee hizi karate mtatupigia.. Mtaishia…/na sintosita kusema asante kwa kunisaidia au kuwasifia .. Kwa kunisaidia…

Washkaji baadhi hawana haki ya kuipresha hii medula…/wao wako radhi kukupa pombe na si pesa ya kula….

Nawaona vyura tu kama snura hii sura ya muhuni haina gere…/ mastar wanaovaa masut mtaani nyumbani kunguni tele…

Kwa magonjwa yanayotibika tunapoteza maisha.. Huruma../watachanga kwenye msiba ukifa.. Hawajali ukiumwa..

Au wanaweza wakahisi umekufa kwa kukutwa umezirai…/ usipo stuka Africa unaweza kuzikwa ukiwa hai…

Haumuui chura kwa kumtupa ndani ya maji../ ukinizuga kwa ulaji takupa fact kwa lugha ya kiushkaji…

Mnataka vitu rahis..? Me nawapa vitu halis…/ watata mnamtaka ibilisi../na sio huyu big kaka ka idris…

Mrnice jua lanutosi na mtaa unakiu ile mbaya…/ hawamsaport isipokuwa wanawapromoti aliowainspaya…
Wakati ney sio kama moxie STOSHI hakupaswa kumgwaya../ lakini uzee bila noti ni zaidi ya nyoshi akiwa vibaya….

I didn’t come this far just to come this far…/ siwezi sanda kama bikra hata nikiishi kistar

Maisha hayakupi unachotaka ila yanakupa unacho tafta…/ pesa ya sadaka wazushi wanaivuta kwa chafu tatu….

Binadam wako wapi hadimnanitoa mie nisiwemo.. / leo nawapa offer ya mswaki halafu kesho mnaning’oa meno..?

Time is money, nafasi haijali kukuzuga../ Wema anataka saa ya almasi ZARI anaujali muda..

Washa sana nyasi, raster yupo kwa fasi vuta../ wanashindwa kujinafas kwa unafki nafsi zinawasuta…

Wabongo wa majuu hamna upendo mnajigawa../ Uongo hauna miguu lakini skendo zinamabawa…

Aliemtia umaskini Africa leo analia kwa yanayomsibu…/ na humtangaza akimpa msaada kiasi cha kumtia aibu…

Dunia sio chafu.. Ni chafu.. Uchafu tukiutazama../ kuna sumu ndani ya watu na hapo hapo tunapokwama…

Hawaamini kwenye kuunda Diamond au KIBA wawili../ wanachoamini ni kumshusha mmoja ili mmoja awe dili…

Cha kupewa hakishibishi.. Ukipewa lazima ukumbushwe…/ Dunia mwendo wa ngisi kung’aa sio lazima star ashushwe..

Ukiacha hisia zikuendeshe Kwa ujeuri utaishia kufeli../ neno la kweli sio zuri na zuri halina ukweli…

Nitasahau vyote.. Lakini milele tamkumbuka alie niumba../ na daily takaa mkao wa push-up tu kama Umbwa







www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez







Post Views: 2,141


Share this on WhatsApp
 
huyu jamaa ni mwanaFALSAFA msela... yani kichwa chake unaweza safiri toka Mafiga Morogoro hadi Igoma Mwanza ukakutana watu wawili tu wa aina yake... yaani ni NOMA zaidi ya hizi herufi nne..
 
Neno la kweli sio zuri na zuri halina ukweli, chakupewa hakishibishi na ukipewa lazima ukumbushwe....
 
Hawaamini kwenye kuunda diamond au kiba wawili...wanachoamini ni kumshusha mmoja ili mmoja awe dili..
 
Fid Q aliwahi kusema anaandika ngoma kali sana ili hata ikibuma basi aweze kusikiliza mwenyewe ghetto. Bila shaka hii ngoma atakuwa anaisikiliza mwenyewe
Huyu ngosha bado watanzania hawajamuelewa nini anakifanya
 
usiache wewe ni incharge huna spear/ kipaji ka ngwear/kwa mpaji ni ka zawadi aliwagea/flag pepea/alihitaji zaidi ya Maji na mmea…? Ilikuaje wamuache hadi mshkaji ulaji wa drags ukamzoea ..?

Ngosha kammisi ngwea.. ..
 
''nawaona vyura tu kama Snura, hii sura ya muhuni haina Gere''.................................

kweli hip hop sometimes 'inanunua ugomvi'!!
 
Hip hop ni tamaduni (Culture) na tamaduni ubadilika lakn Ngosha bado ameshikilia anachokiamini....!
 
Back
Top Bottom