Miss Mbeya 2019 Angelah Deocress, ajinyakulia Taji la Miss na Zawadi ya Pikipiki

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Hatimaye Mshindi wa Miss Mbeya 2019 amepatikana, Angelah Deocress ndio mshindi wa taji la miss Mbeya kwa msimu huu, ikumbukwe mashindano haya huandaliwa na kituo cha redio cha Dream. FM kila mwaka kutoka mkoani Mbeya.

Shindano hilo lilifanyika usiku wa tarehe 3 Tughimbe Hall, Mafyati Mbeya

Miss mbeya 2019 ni Angelic (mwaka jana alishiriki miss mbeya na aliishia top 10)

1st runner up ni Nelly (mwaka jana alikuwa miss Mbeya no 1)

2nd runner up ni Evengelina peter (mwaka jana alifanikiwa kuingia top 5 ya Miss mbeya)

Hii inatufundisha kwamba tusikate tamaaa! Sasa mkapabane Miss kanda

Mshindi amezawadiwa pikipiki mpya Aina ya TANHERO ambayo Ina uwezo wa kumpatia kipato na hata kutimiza Ndoto zake, waandaji ametoa pongezi kwake na Shukrani kwa wanambeya kwa kushirikiana kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa tukio

Kuhusu zawadi wa Pikipiki Mshindi kasema anashukuru kwani zawadi ni Zawadi, sababu ukubwa wa Zawadi unategemeana na uwezo wa muandaaji. Kwake yeye amesema ni fursa kwani anaenda kujulikana kitaifa na kumataifa. Ndoto yake ni kuwa Miss Tanzania.. Kwasasa anachowaza ni Mashindano yaliyo mbele yake na si Zawadi. Kawashukuru Waandaaji pia.

Sherehe hizi, zilipambwa na Msanii Muhinindi wa Kusini Mbosso Khan.

MY TAKE:

Nawapongeza Waandaaji wa Mashindano ya Miss Mbeya kwani wameonesha Uungwana kwa kuahidi kile kilicho ndani ya uwezo wao na kumkabidhi mshindi hapo hapo, kuliko waandaaji wanaoahidi Makubwa na kuishia kuwadhurumu washindi. Huu ni mfano wa kuiga. Hongereni Dream FM Radio.

UREMBO NI HESHIMA!
90937b4701c576ababf72b99673de268.jpg
81802341a9c1c2bbc2c84bc68b3ca07e.jpg
d4819d8c0b768b7d465d9a5d89c2df19.jpg
464a63eaa298f3767e852766080d9211.jpg

e368852d2ac4f27ca9cdc6b91e2d816a.jpg

Angel Deocress mshiriki no.5 miss mbeya 2019, Katika vazi la ubunifu ,likiwakilisha kilimo cha mahindi mkoani mbeya..
 
Tangia Basilla Mwanukuzi alichukue hilo shindano na kuwapiga majungu kina Hashim Ludenga na kundi lake eti ni wasengerema ndo linamfia sasa.

Mimi aliniuzi kipindi kile anaanza maneno ya shombo shombo na kunyanyua midomo kama anasunya kwenye press nikajua huyu ni kichwa maji hajui alitendalo. Yaani shindano linatoka kwenye zawadi za magari na mapesa kisha tunakuja kwenye boda boda.

Yaani miss tz ishajifia kabisa sasa maana hakuna mtu atakaye kuja kuwekeza hapo wale kulisponsa hilo shindano mpaka huyu atoke hapo ana gundu.
 
Nipe ufafanuzi hapa chini:

Miss mbeya 2019 ni Angelic (mwaka jana alishiriki miss mbeya na aliishia top 10)

1st runner up ni Nelly (mwaka jana alikuwa miss Mbeya no 1)
Hata sikuusoma uzi zaidi ya heading

Sijui hata ina maana gani...sielewi masuala ya umiss yanavyokwenda kabisa,kwanza sijui nimefikaje hapa
 
Hata sikuusoma uzi zaidi ya heading
Sijui hata ina maana gani...sielewi masuala ya umiss yanavyokwenda kabisa,kwanza sijui nimefikaje hapa

Okay, nimeona hao washindi kwamba walishawahi kugombea miaka iliyopita.

Najiuliza kama inaruhusiwa kugombea kama ulishindabl nyuma.
 
Tangia Basilla Mwanukuzi alichukue hilo shindano na kuwapiga majungu kina Hashim Ludenga na kundi lake eti ni wasengerema ndo linamfia sasa.

Mimi aliniuzi kipindi kile anaanza maneno ya shombo shombo na kunyanyua midomo kama anasunya kwenye press nikajua huyu ni kichwa maji hajui alitendalo. Yaani shindano linatoka kwenye zawadi za magari na mapesa kisha tunakuja kwenye boda boda.

Yaani miss tz ishajifia kabisa sasa maana hakuna mtu atakaye kuja kuwekeza hapo wale kulisponsa hilo shindano mpaka huyu atoke hapo ana gundu.

Basila Mwanukuzi form 6 alipata zero.
 
Back
Top Bottom