1993 Simba ilishiriki fainali ya Kombe la CAF sio la Shirikisho

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
ANAANDIKA EMMANUEL MALIMA

TWENDE NA DATA
MICHUANO ya Kombe la CAF, ilikuwa ni michuano maalumu ya kila mwaka, iliyoanzishwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kwa kuzishirikisha timu zilizoshika nafasi za pili katika ligi za nchi wanachama na hivyo kushindwa kupata tiketi ya kushiriki mashindano maalumu yaliyokuwepo kwa wakati huo, kwa maana ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Washindi.
Michuano hii ya Kombe la CAF ilianzishwa mwaka 1992, kwa kuiga mashindano ya European UEFA Cup. Kombe la zawadi kwa michuano hii lilipewa jina la aliyekuwa mfanyabiashara tajiri, mmiliki wa vyombo vya habari na mwanasiasa wa Nigeria, marehemu Moshood Abiola, kwa vile ndiye aliyeamua kulidhamini kwa wakati huo.
Jumla ya timu 31 zilishiriki kwa mara ya kwanza mwaka huo 1992, ambapo timu ya kwanza kunyanyua taji la ubingwa ilikuwa ni Shooting Stars F.C ya Nigeria iliyoifunga SC Villa jumla ya mabao 2-0 katika fainali.
Michuano hiyo ilichezwa kwa miaka 11 tu kuanzia 1992 hadi 2003 ilipofutwa rasmi, huku timu ya JS Kabylie ya Algeria ikiwa na historia ya kipekee Afrika, ya kutwaa taji hilo mara tatu mfululizo, ilipofanya hivyo miaka ya 2000, 2001, 2002 hivyo kulichukua jumla na kulihifadhi kabatini.
Raja Casablanca ya Morocco, yenyewe ndio klabu ya mwisho kutwaa taji hilo mara ya mwisho mwaka 2003 ilipoiadhibu Cotonsport de Garoua ya Cameroon kwa mabao 2-0, kabla ya michuano hiyo KUFUTWA RASMI mwaka
huo.
Narudia tena KUFUTWA RASMI, mwaka 2003. Historia iko hivyo na hata takwimu zinasema hivyo kuwa baada ya mwaka 2003, hakuna tena bingwa wa kuanzia mwaka 2004 hadi sasa hii ikiwa na maana kuwa ukomo wa Kombe la CAF uliishia mwaka 2003.
Mwaka huo huo 2003 CAF ikaanzisha mashindandano mengine ambayo yaliua Kombe la CAF na lile la Washindi na kuwa Kombe la Shirikisho ambalo ndilo hili la sasa.
Kuhusu Simba kucheza fainali za Kombe CAF ni kweli ilishiriki mwaka 1993 ikatolewa na Stella Abidjan kwa kufungwa mabao 2-0 hapa hapa 'Shamba la bibi'.
Hata hivyo hiyo haikuwa michuano ya Kombe la Shirikisho. Ukiangalia
takwimu, Simba ilishiriki Kombe la CAF mara mbili tu. Mara ya kwanza ndio hiyo ilipofika fainali mwaka 1993 na ya pili ni mwaka 1997 ilipotolewa raundi ya kwanza kwa kufungwa na AFC Leopards kwa jumla ya mabao 4-1. Haikushiriki
tena Kombe la CAF. Hata hivyo kwa mujibu wa takwimu, kwenye Kombe la Shirikisho, Simba imeshiriki mara 6, hatua kubwa ikiwa ni Robo Fainali ya mwaka jana ilipotolewa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwa penalti.
Ilianza kushiriki mwaka 2007, ikaishia raundi ya awali, 2010 – raundi ya pili, 2011 – mtoano, 2012 – raundi ya pili, 2018 – raundi ya kwanza, 2021–22 – robo fainali.
 
Mbona Kuna watu Wanasema kuwa Kombe la CAF ndiyo la shirikisho,wakijenga kuwa ni baada ya kuunganishwa Kombe la Washindi na Kombe la CAF!?

Which is which!!?
 
Kombe la CAF sio la Shirikisho, haya ni mawili tofauti. Lilikufa mwaka 2003. 2004 yakaanza mashindano mengine kwa kuunganisha Kombe la CAF na la Washindi. La Washindi lilianza mwaka 1975 hadi 2003, la CAF lilizuka 1992 hadi 2003. Mwaka ambao Simba anacheza fainali na Stella Kombe la CAF, kule Kombe la Washindi ubingwa ulikwenda kwa Al Ahly. Sasa kama wanadai yaliunganishwa bingwa wa mwaka huo 1993 alikuwa ni Stella Abidjan ama Al Ahly ili kuendeleza historia.
 
Nashukuru Kwa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom