Misri wadai kutumia maji ya mto nile 90% ni haki yao: je ni haki??

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
Kwa mujibu wa BBC nchi ya misri imedai kutumia maji ya mto nile ni haki yake na haiwezi kuruhusu haki hiyo ipokonywe na nchi kama Kenya, Tanzania na Ethiopia ambapo mto huo una vyanzo vyake.

Waziri wa maji wa Misri amesema, serikali yake haiwezi, kukubali kupeana haki yake ya kutumia asilimia 90 ya maji ya mto Nile kuambatana na mkataba uliotiwa saini nchini Sudan mwaka wa 1959.

Mkataba huo umepingwa vikali na mataifa ambayo mto huo una vyanzo vyake kama vile Ethiopia, Tanzania na Kenya.

Wakuu mimi nashindwa kuwaelewa hawa waarabu, hivi wana haki gani ya kutumia maji ambayo chanzo chake ni afrika mashariki na wadai sisi wenye vyanzo tusitumie?

Hapa napendekeza tuongeze mabomba ya maji kutoka ziwa victoria tupeleke maji Singida, Tabora, Dodoma na Manyara ili wakome hawa waarabu wasio na akili.

Kwa nini serikali za EA zinashindwa kutumia maji kwa raha tuone waarabu wale watafanya nini? Vita yenyewe hawawezi wale na kama wanaleta fyoko tunampa miradi hiyo Israel tuone watasema nini!!!
 
unaongelea serikali za africa mashariki ipi?...hii ya kenya inayoipinga tanzania kuuza pembe za ndovu ijiendeleze kiuchumi au ipi hiyo?...anyway mie pia sielewi hawa waarabu kwann wanakosa hata lepe la busara..tunatakiwa tuwasaidie kuwafundisha adabu na busara kwa kutumia maji yetu ziwa victoria yatakayobaki ya kwao yatafuata bonde la mto nile kisha tuone wataishi vipi?...mbona sijasikia tanzania ikisema mafuta yaliyoko huko msisiri kwao na sie tuna share nayo?...mkataba wa mwaka gani huo?..1959...enzi za mkoloni?...nadhani na karl peters anatakiwa akomalie mikataba yake ya berlin ya 1886 Before Colonial era
 
Maji siku zote ni uhai na yemeleta vita kubwa sehemu zote duniani. Ni jambo linalohitaji diplomasia na sio nguvu na jiografia ya nchi husika. Misri hawakuchagua wao kuwa jangwani, na wala hawakuuchimba mto nile ili upite kwenye nchi yao, kama ambavyo na sisi hatukutengezeneza mito wala maziwa. Hivyo hatuna budi kukubaliana.

Ni sawa na maumbile, kuanzia miguu hadi kichwa, kila kimoja kipo mahali pake na kwa kazi yake. Jambo la msingi ni jinsi gani ya kuvitunza vyote kwa pamoja. Mathalani kwetu sisi tunaoishi huku Maketi tunanawa uso kila siku, ila hatuogi kila siku.
 
mh hapasina data za kutosha ila najua hawa waarabu ni wajeuri so wanatumia kigezo cha kiburi na jeuri yao akuna lingine
 
unaongelea serikali za africa mashariki ipi?...hii ya kenya inayoipinga tanzania kuuza pembe za ndovu ijiendeleze kiuchumi au ipi hiyo?...anyway mie pia sielewi hawa waarabu kwann wanakosa hata lepe la busara..tunatakiwa tuwasaidie kuwafundisha adabu na busara kwa kutumia maji yetu ziwa victoria yatakayobaki ya kwao yatafuata bonde la mto nile kisha tuone wataishi vipi?...mbona sijasikia tanzania ikisema mafuta yaliyoko huko msisiri kwao na sie tuna share nayo?...mkataba wa mwaka gani huo?..1959...enzi za mkoloni?...nadhani na karl peters anatakiwa akomalie mikataba yake ya berlin ya 1886 Before Colonial era

Kama sio hiyo mikataba, basi wangekuwa na uhuru wa kutumia maji kama sehemu nyingine yoyote ya afrika, kwani hakukuwa na Tanzania wala kenya na misri. Kwani haya mataifa si yamezaliwa kwa mikataba hiyo hiyo?
 
Hizi ndio issue ambazo ningetegemea Mr. Membe angeshughurikia badala ya kupoteza muda na wacomoro wasiozidi idadi ya wasukuma wa Mwanza tu. What happen kwa misemo ya kiukombozi "MAJI NI UHAI"? Jamani watu wetu wanaangamia kwa kukosa maarifa nimequote from Bible, kuna haja gani ya kuomba ruhusa kwa waarabu kuhusu kutumia maji ya Ziwa Victoria, kama kuna mkataba si waseme nani alisign huo mkataba, hebu wampe hiyo Wizara Bwana Pombe Magufuli maana yule bwana aangalii kunyanzi. Au basi wampe Morani maana nae alijitahidi ndio bomba likaja mpaka Shinyanga. Lakini Babu Chenge ushasikia kuongelea kitu kama hicho? yaani vitu vingine bwana si bora Kibonde na Captain wanatupunguzia STRESS kiliko hawa MAJAMAA WANAOKUTANAGA DODOMA KUCHOMA NYAMA NA KUPIGA MEZA Mungu awabariki wala sitaki Kuwalaani.
 
membe hawezi kuongea chochote hapa. akiongea tu, urafiki na mkuu utaisha, si unakumbuka yaliyomkuta Lowasa baada ya comment zake kuhusu maji ya mto Nile pale walipoanza kupeleka maji yake kwenye mikoa ya kaskazini kwenye ule mradi kikwete alienda kuzindua muda si mrefu? ukitaka kugombana na kikwete, ongelea jambo lolote kuhusu nchi za kiislam, urafiki unaisha. Misri haina haki yoyote kutuambia sisi tufanye hivyo, lakini kwasababu marais wetu ndo hivyo tena, tutabaki na ukame singida, shinyanga, dodoma na mikoa mingine, tukiachia waarabu kutumia maji. hapohapo hat urafiki na israel hatuwezi, wakati misri anao uwezo kusambaratisha nchi zote hizi tano kwa mpigo akiamua kuanzisha vita, Israel angekuwa rafiki yetu mkuuu, lakini ndo hivyo tena, viongozi wetu wanaona bora waarabu kuliko waisrael. siku zote ni kutoa laana juu ya israel tu. waarabu wenyewe hawajawahi kutoa msaada wowote kwa Tanzania, zaidi ya kujenga misikiti ya Osama, na kufadhili ugaidi. ukimuweka mtu mwenye kicha kigumu awe rais, mtaburuzwa mpaka mkome. nafikiri hapo ndipo penye hekima ya watanzania, hasa katika uchaguzi huu ujao.
 
Uganda wanaweza kuuita Idd Amin River au Mukede River katika eneo la nchi yao na kuudivert ikiwa EAC wataamua kufanya hivyo. Misri Bonde wanalodai ni la kwao.

And is TZ using Nile river. We are using Lake viktoria water. With this sense Egypt is using Lake Viktoria water which is not their right. The water that flow in the nile valley doesn't come from nile river it comes from Lake viktoria and other sources. Suppose those small sources are sealed in Ethiopia and sudan, the blue and white ?Nile? and if the names are changed?
 
Back
Top Bottom