Elections 2010 Misikiti nayo yaanzisha mkakati kuhusu uchaguzi mkuu ujao!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Waislamu nao wameamua kujipanga ili kuhakikisha kuwa Rais, wabunge na madiwani hawachaguliwi kwa misingi ya kidini.

Ikiwa ni counter attack dhidi ya kanisa wanazuoni wa kiislamu pamoja na mashekhe 15 wameunda jopo ambalo pamoja na mambo mengine litaratibu na kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi mkuu ujao kwa maslahi ya waislamu! Jopo hilo lilizinduliwa katika hoteli ya Starlight, Dar tarehe 21/06/2009. Mratibu wa jopo hilo, Sheikh Mohamed Idd alikemea ubaguzi wa kidini katika masuala yote ya uchaguzi.

Hata hivyo, japokuwa sababu zilizotolewa na jopo la wanazuoni hao na masheikh zinaweza kuonekana kuwa ni hofu yao dhidi ya kasi ya maandalizi ya Kanisa katika uchaguzi ujao lakini uzofu unaonyesha kuwa kama malengo ya jopo hilo yatakuwa kama yalivyo, linaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa, maana katika chaguzi zilizopita, hasa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, misikiti mingi ilishutumiwa kwa kuwapigia debe wagombea wa chama fulani cha siasa.

Licha ya makanisa hayo kushutumiwa kuendesha kampeni kwa ajili ya wagombea mbalimbali, lakini hali ilikuwa tofauti na kampeni zilizodaiwa kufanywa misikitini, ambazo kwa asilimia kubwa, zilihusisha chama kimoja huku kanisa likishutumiwa kutumiwa na vyama mbalimbali!

Source: Nyakati, Juni 28-Julai 4, 2009.
 
Counter attack dhidi ya????? They have started with a wrong foot kwa sababu inaonekana lengo lao ni kujibu mapigo ya.... na si kutoa elimu ya uchaguzi kama wenzao walivyoanza kufanya
 
...wanazuoni wa kiislamu pamoja na mashekhe 15 wameunda jopo ambalo pamoja na mambo mengine litaratibu na kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi mkuu ujao kwa maslahi ya waislamu! ....
Yule Mzee Makwaia wa 'Je, Tutafika?' ya Ch10 hayumo kwenye jopo hilo? Jumanne hii aliu-bias sana mjadala wa kuhusu toleo la Maaskofu wa Katoliki kuhusiana na elimu ya wapiga kura. Nadhani baada ya kuundwa kwa jopo hilo, moja ya watu watakaoshtuka ni Mch. Anthon Lusekelo aka Mzee wa Upako, kwani aliungana sana siku ya mjadala kupinga mpango wa Maaskofu kwa hoja kwamba dini zisiwaongoze waumini, sasa akigundua kuwa na upande aliokuwa anaungana nao umeunda chombo kama kile kile walichokuwa wakikipinga pale Ch10, ndo atajua kwamba kumbe alikuwa anatumiwa bila kujijua !!!
 
Wao wapo upande gani haya makanisa na misikiti maana mwaka 2005 walisema kuwa Mzee wa Kaya ni Chaguo la Mungu leo wanasema nini??
 
Nadhani uchaguzi mkuu ujao utatumika udini na matokeo yake ni kama ifuayavyo

UDINI KWENYE UCHAGUZI +UKABILA + RANGI= VITA BAADA YA UCHAGUZI na ukitaka kujua hii inavyofanya kazi tazama kilichotokea rwanda/kongo ambapo vita kanuni yake ni hii

VITA=UBAGUZI(unaotokana na Udini,urangi,ukabila)

kwa hiyo viongozi wa dini wajue hizo kanuni ili tuingie vema kwenye KUCHINJANA

chao
 
Mimi nafikiri kama lingo ni kutoa ilimu ya uraia na kubainisha wazi umuhimu wa kura ni sawia kabisa.

Lakini kama dini zote zikiwa na malengo tofauti na hapo juu basi hilo ni balaa kuba na ni sawa na kuanza kutega mabomu vichakani tukisubiri 2010 yalipuke
 
Sasa nao wanataka mtu ambaye ataanzisha Mahakama ya Kadhi japokuwa CCM katika Ilani yao wanasema hivyo lakini Waislam wana haki ya kuidai CCM ile Ilani inayosema kuwa wataanzisha mahakama ya kadhi
 
Ndio maana kuna ajenda kila watu wana malengo yao, Makanisa wana lengo lao na hata hawa misikiti nayo ndio hivyo, labda waseme wako upande gani
 
Ndio maana kuna ajenda kila watu wana malengo yao, Makanisa wana lengo lao na hata hawa misikiti nayo ndio hivyo, labda waseme wako upande gani

Lakini kama lengo lao ni moja kutoa elimu kwa wapiga kura bila kuingiza udini, kwanini wasiungane, na wakatengeza muhtasari mmoja wa kutoa hiyo elimu? ( something is cooking up!)
 
Lakini kama lengo lao ni moja kutoa elimu kwa wapiga kura bila kuingiza udini, kwanini wasiungane, na wakatengeza muhtasari mmoja wa kutoa hiyo elimu? ( something is cooking up!)
A good thought! Badala ya kugeuza jambo hili likawa ni vita vya kidini, kwanini wasiungane basi wakaelimisha watu umuhimu wa kuchagua viongozi bora? Kukurupuka bila mpangilio huwa kuna harufu ya shari mara nyingi kuliko facts. Ila,nasubiri!! time will tell.
 
Makanisa na Misikiti imeingiliwa na mambo ya ajabu ajabu sana miaka ya karibuni, sijui ni tamaa, ukosefu wa elimu au ndio mashetani yenyewe yanafanya kazi...!!!
 
Mimi nataka waseme mapema na kudeclare mapema na watu wao na nani wanamunga mkono katika uchaguzi mwakani
 
A good thought! Badala ya kugeuza jambo hili likawa ni vita vya kidini, kwanini wasiungane basi wakaelimisha watu umuhimu wa kuchagua viongozi bora? Kukurupuka bila mpangilio huwa kuna harufu ya shari mara nyingi kuliko facts. Ila,nasubiri!! time will tell.

Hili wazo la kuunganisha matamko ya pande zote mbili ili kuwa na tamko moja nimelipenda. A briliant idea!
 
Ndio maana kuna ajenda kila watu wana malengo yao, Makanisa wana lengo lao na hata hawa misikiti nayo ndio hivyo, labda waseme wako upande gani

Makanisa yanataka kiongozi bora ndio maana waliunga mkono uteuzi wa JK 2005 ambaye ni mwislamu. Sina hakika misikiti wanataka nini au wako upande gani kwenye move yao.
 
Lakini kama lengo lao ni moja kutoa elimu kwa wapiga kura bila kuingiza udini, kwanini wasiungane, na wakatengeza muhtasari mmoja wa kutoa hiyo elimu? ( something is cooking up!)

Of course something is cooking up. Wakristu wametambua kwamba wamezubaa sana hasa kwenye uongozi wa chini kuanzia nyumba kumi kumi hadi udiwani hasa sehemu za mijini. Matokeo yake ni kwamba hawashirikishwi kwenye maamuzi muhimu. Kwa mfano kuna malalamiko kwamba mabilioni ya JK yaligawiwa kwa upendeleo kwa vile wakristu hawako kwenye uongozi wa serikali za mitaa. Lengo la semina hizi ni kuwahamasisha wakristu wachangamkie uchaguzi wa 2010 la sivyo watajilaumu.
 
Sasa wanataka nini kama wanajua haya, Mimi sijaona kuwa sababu ya kufanya hivi na sio kusema kuwa watu wote walikuwa upande wa CCM na leo wanataka nini??? Mbona wao walisema kuwa CHAMa cha Mapinduzi
 
Mijadala ya siasa na uongozi haipaswi hata kidogo kuingiza maoni ya kidini, hasa katika jamii kama ya Kitanmzania ambayo, mkururu wa waumini tofauti wanaishi mtaa mmoja. Mara nyingine hata nyumba moja. Uchaguzi unapaswa kuzizngatia uwezo wa wagombea na na sio imani kwa vyovyote vile. Ingetosha kwa viongozi wa dini kuwapa wafuasi wao maadili tu. Sioni ni kwa vipi kiongozi wa dini akaadress issue ya kisiasa na isilete mkanganyiko toka upande wa wafuasi wa imani tofauti. Lets be realistic guys, Tanzania ya leo, ishu za kidini zimekuwa sensitive sana. Wakati fulani hadi inatisha fulani hivi.
 
Yule Mzee Makwaia wa 'Je, Tutafika?' ya Ch10 hayumo kwenye jopo hilo? Jumanne hii aliu-bias sana mjadala wa kuhusu toleo la Maaskofu wa Katoliki kuhusiana na elimu ya wapiga kura. Nadhani baada ya kuundwa kwa jopo hilo, moja ya watu watakaoshtuka ni Mch. Anthon Lusekelo aka Mzee wa Upako, kwani aliungana sana siku ya mjadala kupinga mpango wa Maaskofu kwa hoja kwamba dini zisiwaongoze waumini, sasa akigundua kuwa na upande aliokuwa anaungana nao umeunda chombo kama kile kile walichokuwa wakikipinga pale Ch10, ndo atajua kwamba kumbe alikuwa anatumiwa bila kujijua !!!

Soma sentensi ya kwanza kabisa kabla ya kukurupuka. Kwa mujibu wa hilo jopo ni kuwa watahakikisha kama viongozi hawachaguliwi kutokana na imani zao.

Sasa Lusekeo atajihisi vipi disapointed? mie nadhani ndio wameungana na Mchungaji kulaani jitihada zinazoandaliwa za kuweka Uongozi (Chama) mbadala ikiwa CCM either wasingetengua uamuzi wao kuhusu misamaha ya kodi, au watathubutu tena kuongelea masuala ya Mahkama ya Kadhi na OIC!
 
Back
Top Bottom